Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

HALI ILIVYO JUU YA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO WAKIKE MKOA WA MOROGORO.

 

Nchini Tanzania umri wa balehe ni kipindi kinachoambatana na hatari zaidi kwa wasichana, hasa kwa wale waishio katika mazingira magumu, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuongeza na kuendeleza uimarishaji wa uelimishaji kuhusu usawa wa kijinsia, haki na maendeleo yao ya wasichana.

Ili kuisaidia Serikali katika kuelimisha kundi hili lililopo kwenye hatari zaidi, vyama vya kiraia, jamii, wazazi, walezi, viongozi wa dini, viongozi wa kimila, wasichana na wavulana wenyewe wanapaswa kushiriki kikamilifu kila mmoja kwa sehemu yake, ili kukabiliana na changamoto zinazo wazunguka wasichana.

Mkoani Morogoro nimezungumza na baadhi ya wasichana walio katika umri wa rika balehe, kusikia wanafahamu nini kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia, Bakita Andrea mkazi wa Manispaa ya Morogoro ni msichana mwenye umri wa miaka kumi natatu (13) mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi saba saba “A” iliopo Manispaa ya Morogoro, anaelezea vitendo vya ukatili.

“Ukatili ni unyanyasaji wa kijinsia kwakuwafanyisha kazi ngumu zisizo endana na umri wao kuwapiga, kuwanyanyasa na kuwatenga, ukatili huwakuta sana watoto wakike, wengine hufanyiwa ukatili na wazazi wao, ndugu zao jamaa na marafiki n ahata walimu wao. Nakumbuka juzijuzi shule ya Mazimbu alijinyonga mwanafunzi wa darasa la tano kwa kufanyiwa ukatili na babayake aliharibika sehemu zake za siri kwasababu alikuwa akibakwa na babayake” Amesema.

Aidha Bakita anasema madhara yanayoweza kujitokeza kwa binti alie fanyiwa ukatili, “Ukatili wa namna hiyo huleta madhara kwa mtoto wakike kwa kumuharibia sehemu za siri nakumfanya awe hayupo makini darasani kwa sababu akiwa darasani mudawote nimtu wakuwaza nikirudi nyumbani usiku kazi kwa baba ataanza kuni fanyia vitendo vya ukatili”.

Bakita akapaza sauti yake kwaniaba ya wasichana wengine kwa Serikali kuhusu watu wanao fanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wakike, “Serikali ikomeshe vitendo vya ukatili na itoe adhabu kali kwa wale wanao wafanyia watu vitendo vya ukatili”.

Hata hivyo Maria Mussa yeye ni mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Uhuru iliopo katika Manispaa ya Morogoro, anaeleza anayo yafahamu juu ya ukatili wanao fanyiwa watoto hasa wakike.

“Nakumbuka kulikuwa na watoto watatu waliokuwa wakiishi na bibi, babu na binamu yao, kumbe binamu yao akawa kila siku anaingia kwenye chumba cha hao watoto watu nyakati za usiku wakiwa wamelala na kuwa fanyia ukatili kwa kuwarawiti na kuwambia wakipiga kelele nawaua”.

Maria akatoa ushauri kwa jamii hususani wazazi, “Wazazi wawe wanawalinda watoto na wawe wanakaa nao watoto karibu wenyewe kwa sababu watoto wakienda kulelewa na watu wengine ndio wanawafanyia ukatili” Amesema.    


John Kabambala-TKT/UnnewsKiswahili-Morogoro.

Post a Comment

0 Comments