Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

WANAFUNZI NA WALIMU WAELEZEA MANUFAA, KUKAMILIKA MRADI WA MADARASA YA UVIKO19

 

 

                          Chumba cha Darasa la Kidato cha kwanza B'' Sumaye Sekondari Manispaa ya Morogoro.

Wanafunzi wa Shule za Sekondari Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania wameeleza kunufaika na Mkopo wa riba nafuu Trilioni 1.3 ambao Tanzania iliupata mwaka 2021 kutoka Shirika la Fedha Dunia - IMF kwa kuelekeza  sehemu ya Fedha katika uboreshaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19, ikijenga vyumba vya madarasa 12,000 vilivyogharimu shilingi Bilioni 240 kwa lengo la kupunguza msongamano shuleni sambamba na kujikinga na ugonjwa wa Uviko 19.

Katika kuonesha Taswira halisi Mwandishi wa Habari Hamad Rashid, amefanya ziara ya kutembelea Mradi uliokamilika wa vyumba vya madarasa ya Uviko 19 katika Shule za Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Manispaa ambayo imejenga jumla ya vyumba vya madarasa 86 na kuandaa Makala ifuatayo.

Ziara yangu imeanzia Shule ya Sekondari Sumaye iliyopo Kata ya Bigwa nakutana na Wille Victor Mwanafunzi wa kidato cha kwanza, alisema anafurahi kusomea katika madarasa ya Uviko19 na manufaa anayoyapata ni makubwa.

“haya madarasa ya Uviko19 yameninufaisha cha kwanza katika upande wa Viti na madirisha, mwanzo ilikua wanafunzi wanakaa zaidi ya 50 ndani ya Darasa moja lakini saivi tunakaa ka nafasi na madirisha yanapitia hewa safi, hata kusoma Mwanafunzi inakua rahisi kumuelewa Mwalimu” alisema Wille Victor.

Ofisini kwa Makamu mkuu wa Shule ya Sekondari Sumaye, Mwalimu Msokelo Baruti nilifika na alieleza namna walivyonufaika na Mradi huu wa madarasa ya Uviko 19.

Baruti alisema “hapa shuleni tumenufaika kwa kujengewa Vyumba viwili vya madarasa, viti na meza zake Mia moja Mwaka jana tulitoa wanafunzi wa Kidato cha Nne 164, Mwaka huu tumepokea zaidi ya wanafunzi 200 unaweza kuna jinsi tulivyokuwa na uhitaji”

Ziara yangu ikahamia Shule ya Sekondari Lupanga Kata ya Kilakala ndani ya Darasa la kidato cha kwanza baada ya kukaribishwa na Wimbo wa Shule nilimhoji mwanafunzi mnufaika wa Kidato cha kwanza, Grace Marema ambapo pamoja na mambo mengine alisema, madarasa ya Uviko yamepunguza utoro Shuleni.

“Kwenye adha ya utoro imesaidia wanafunzi wengi kutotoroka kwa sababu mnapokua mmeachiana nafasi ni rahisi Mwalimu kujia namba ya wanafunzi nani yupo na nani hayo kwa hivyo inakua ni ngumu mwanafunzi kutoroka, kuliko mwanzo ambapo kulikua na msongamano wa wanafunzi darasani” alisema Grace

Neema ya kujengewa madarasa ya Uviko 19 imekuja wakati sahihi Mkuu wa Shule ya Sekondari Lupanga Mwalimu Flora Ndunguru alisema.

“Kiukweli tumepokea kwa furaha kubwa Lupanga Sekondari tumejengewa madarasa Sita na kila darasa lina viti na meza 50 jumla ya katika maradasa yote ni viti na meza zake 300, hii ni kutokana na wingi wa wanafunzi tulionao, tulikua tumepangiwa wanafunzi wanatakiwa kuripoti Kidato cha Kwanza Mwaka 2022, 277 na walioripoti ni wanafunzi 230” alisema Mwalimu Flora.

Baada ya Flora Ndunguru ikafika wakati wa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Gabriel Paul ni Afisa Elimu Sekondari.

“Katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro tulipokea jumla ya Fedha 1, 720,000,000, tumejenga jumla ya vyumba vya madarasa 86 katika Shule 21 zilizonufaika ambapo ndani yake tumejenga Shule mpya Nne za Sekondari ambazo ni Mazimbu, Mkundi, Tungi na Shule ya Sekondari Mbuyuni Modern” alisema Gabriel Paul.

Ujenzi wa madarasa ya Uviko 19 umezingatia viwango vyote vya Serikali, alisema kaimu Mhandisi wa Majengo Halmashauri ya Manispaa Morogoro, Injinia Juma Gwisu.

Gwisu alisema “tulikua na Fomu maalumu ya kuhakikisha kwamba kila hatua ya ujenzi tunakagua na kabla ya kuanza ujenzi fundi anajaza na msimamizi anajaza, hivyo hivyo na katika vifaa tulikua hatuwezi kupeleza Tofali eneo la Ujenzi (site) tukishajirishisha ndio tunaruhusu ujenzi kuendelea, hii imeleta manufaa mazuri hadi kufakisha vyumba vyote vya madarasa kujengwa kwa kiwango bora”

Ally Machela ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ameeleza jinsi madarasa ya Uviko19 yalivyoleta chachu katika Elimu.

Machela alisema “Kwanza tumeweza kuwapeleka Shule wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa wakati kama agizo la Serikali lilivyoelekeza, na tumefikia zaidi ya Asilimia 90 ya wanafunzi wote wa kidato cha kwanza wamesharipoti Shule”

Machela pia alizungumzia afua za kujikinga na Homa ya mapafu Uviko 19 kwa wanafunzi kwa kusema Jamii sasa imebadilika, watu wengi wanafuata maelekezo ya Serikali ya namna ya kujikinga na Uviko19 na Shuleni kuna miundombinu mizuri inayomuwezesha mwanafunzi kujikingakama kuwepo kwa visima vya Maji vilivyochimbwa na wadau mbalimbali wa Elimu.

Na Hamad Rashid - Morogoro.

 

 

Post a Comment

0 Comments