Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

KUWA NA MAAMBUKIZI YA VVU SIO SABABU YA KUTOKUWA NA MPENZI.

Suala la maambukizi ya virusi vya HIV vinavyo sababisha ugonjwa wa Ukimwi bado linawakosesha usingizi wataalamu wa afya ulimwenguni kote, Tangu ugonjwa wa Ukimwi ulipogunduliwa miaka ya 1980, kumekuwa na fikra mbalimbali kwa baadhi ya wanajamii kuhusu jinsi virusi vyake vinavyoweza kusambazwa, Je maisha ya waathiriwa wa ugonjwa huo katika jamii yakoje hadia sasa? Leo nimepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa waathirika katika Mkoa wa Morogoro.


Hali ilivyo kuwa kwa Marrystella Kagambi:
“Haikuwa halaka na rahisi kwa umri wangu niliokuanao kuelewa umuhimu wa kumeza dawa kwa wakati na kilasiku ukizingatia sikufahamu kwanini ninameza dawa pasipo ukomo, nyakati nyingi sikuwa mfuasi mzuri wa dawa ikiwa dada zangu ambao walikuwa wasimamizi wangu hawakukumbuka kuniambia muda umefika wa kumeza dawa hata mimi sikujali.”

Ni miaka 30 sasa akiishi na hali ya maambukizi ya vvu, binti huyu anaeishi Yespa Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro jina lake Marrystella Kagambi anasema alizaliwa akiwa na maambukizi ya vvu, amegundua kua yupo katika hali hiyo alipofika darasa la sita dada yake alipompeleka kituo cha afya kwa ajili ya kujua hali yake kiafya, akiwa mkubwa mwenye kutambua jambo lolote ndipo alipojua kwanini alikuwa akisisitizwa kumeza dawa pasipo ukomo.
“Kusema kweli nilipo gundua kwamba nimtu ninaeishi na maambukizi ya vvu nilisikitika laki haikuniumiza sana kwa sababu niliyapata tangu kuzaliwa kwangu kutoka kwa mama yangu, tofauti na mtu ambae akipata maambukizi akiwa anajitambua huumiza sana kwani huanza kujiuliza jamii itamtazamaje juu ya mwenendo wa afya yake”.


Unyanyapaa.
Miongoni kati ya changamoto ambazo amewahi kukutana nazo kuhusu unyanyapaa ni shuleni kwa baadhi ya walimu wake wa darasa, akiwa bado shule ya msingi alikuwa na kidonda sikioni chamuda mrefu hakiponi hali ile ilisababisha nzi mranyingi kwenye sikio lake, mwalimu mmoja wakike sikumoja aliniita pembeni ya darasa akamwambia kuanzia kesho asiende tena shuleni hadi kidonda hicho kitakapo pona.

“Nilipo fika nyumbani nilimueleza dada yangu alicho niambia mwalimu dada alichukia sana, kesho yake asubuhi niliambatana nae kwenda shuleni tulipofika wakakaa kikao na mwalimu mkuu na yule mwalimu aliekuwa ameniambia nisiendeshuleni hadi kidonda kitakapo pona, kumbe mwalimu yule hakuwai kujua haliyangu ya maambukizi kiukweli niliruhusiwa nikaendelea na masomo kama kawaida ila sijawahi kusahahu tukio hilo lililo nifikirisha, nikajiuliza kwani mwenye maambukizi hapaswi kuchangamana na watu wengine?”

Aidha Marrystella anasema tangu wakati huo akaanza kua mfuasi mzuri wadawa kipindi cha masomo yake ya shule ya msingi hadi sekondari akamaliza kwa uzuri japo hakufanikiwa kuendelea na elimu ya juu lakini alipata maarifa yakuendesha maisha yake, na huduma zinazotolewa kwenye vituo vya afya wanazipata kwa wakati pasipo shida yeyote kutoka kwa wahudumu na mambo yameboreshwa hakuna tena unyanyapaa wa aina yeyote.

“Nashukuru MUNGU sasahivi wakati mwingine ninachukuliwa na vituo vya afya na hosipitali ya Mkoa kwenda kuelimisha vijana wenzangu kuhusu namna ya kujitokeza kupima afya zao na kuchukua hatua madhubuti kwa wanaogundulika wana maambukizi na hata wasio na maambukizi, tunawashauri maisha ya kuishi baada ya kujua hali zao.”


Mahusiano:
Bi,Kagambi anasema, Ukiwa unaishi katika hali ya maambukizi sio sababu ya kutokuwa na mpenzi..hapana isipokuwa inabidi ufuate ushauri wa wataalamu wa afya ni nyakati gani zinafaakwako kuwa na mpenzi au kama unataka kubeba ujauzito kila hatua, mfano mimi nina mpenzi wangu tunaishi nae hadi sasa na tunatarajia kufunga ndoa nikiwa kwenye hali hii ya maambukizi ya vvu, bahati nzuri na yeye anafahamu kuwa nipo kwenye hali hiyo na tunaishi kwa ushauri wa daktari.

Ushauri:
Hata hivyo Marrystella anaishauri jamii. “ushauri wangu hususani kwa vijana wajitokeze kwenda kujua hali zao za kiafya na wachukue hatua baada ya kupata majibu, huduma kwenye vituo vya kutolea huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi ya vvu zimeboreshwa mno huwezi kujutia ukifika kwa lengo la kupata ushauri, kupima hata kuchukua dawa wasiogope milango ipowazi kuwa na vvu sio mwisho wa maisha.”

Na, John Kabambala.

Post a Comment

0 Comments