Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

ISSA IBRAHIM MGONJWA WA MWISHO WA POLIO TANZANIA

 

Polio ni nini:

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania inatoa ufafanuzi kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa polio kuwa ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho huambukizwa kutoka kwa mtu aliyeathirika kwenda kwa mwingine, kwa kula au kunywa kitu kilicho chafuliwa na kinyesi chenye virusi vya polio. Virusi vya polio vinapoingia mwilini huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara ya kiafya ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa kiungo au viungo na hata kupelekea kifo.

Dalili:

Dalili za awali za ugonjwa wa polio ni pamoja na homa, uchovu, maumivu ya kichwa, kutapika, kukakamaa shingo na maumivu ya viungo, na kundi linalo athirika Zaidi ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano 5.

 Chanjo ya polio:

Nizaidi ya miaka arobaini (45) tangu Tanzania ianze zoezi la utoaji chanjo za kuzuia mlipuko wa ugonjwa polio na zoezi la utoaji chanjo ya kwanza ilianza kutolewa mnamo mwaka 1975.

Lini wagonjwa wa mwisho wa polio waligundulika Tanzania?

Kwamujibu wa Dr. Anthony Kazoka kutoka shirika la afya ulimwenguni (WHO) ofisi za Tanzania nilipo fanya nae mahojiano maalumu kuhusu mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa polio nchini na utoaji chanjo Amesema.

Kwa mara ya mwisho wagonjwa wa polio waligundulika kwenye mikoa mitatu ya Tanzania bara, mgonjwa wa kwanza aligundulika tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani Arusha, Mgonjwa wapili aligundulika tarehe 24 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani Kigoma na mgonjwa wa tatu na wa mwisho aligundulika tarehe 30 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani Mtwara.

Shuhuda wa ugonjwa huu Tanzania ni nani?

Ilikupata uhalisia Zaidi kuhusu changamoto za ugonjwa huu wa polio nimemtafuta mgonjwa wa wamwisho kugundulika na virusi vya polio nchini Tanzania ndugu Issa Ibrahim alie gundulika tarehe 30 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani Mtwara.

“Nilizaliwa Wilaya ya Mtwara vijijini Mkoani Mtwara, wakati nikiwa na umri wa miaka mitatu sikumoja nilienda uani kujisaidia sasa wakati ninarudi ghafla mguu wangu wa kushoto ukaisha nguvu nikadondoka chini, nikajaribu kunyanyuka ikashindikana.

Basi nikapiga kelele za kuhitaji msaada.nikaita mamaaaaa!!!!!!!!!!!!! Mama alikuja alipofika nika mwambia nimeshindwa kutembea akaninyua akajaribu kunisimamisha lakini mguu ukaanza kukakamaa na kuuma sana, akanibeba akanipeleka ndani kunikalisha.

Basi!! Baadae hali ile hikurejea kwenye ukawaida wake baba alipofika mama akamueleza jinsi ilivyo tokea mwanzo hadi mwisho, jambo la kushangaza baba akasema huyu mtoto amelogwa sio ugonjwa wakawaida hakuna haja ya kumpeleka hospitali huko nikupoteza muda na pesa, baba akawa anamwambia mama maneno hayo.

Mama hakunikatia tamaa sasa nimekuwa mtu wa kubebwa wakati wote au wanapo niacha ndipo watakapo nikuta maana siwezi kunyanyua tena mguu na kutembea, siku moja akanipeleka kituo cha afya nilipo pimwa ndio nikagundulika nina polio, ila imeathiri muguu wataalamu wa afya wakamshauri mama niwe nakisaidizi cha mkuu kwamaana ya kutembea na magongo”.

Maendeleo yake yakoje mpaka sasa?

Ninaendelea vizuri maana nilipona polio laikini iliniachia maumivu makali kwenye mguu wangu wakushoto, siwezi kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu nikiwa nimesimama kunawakati ukifika unaisha nguvu ahata kama ninatembea inabidi nisitishe safari nikae kwanza ukipoa ndio niendelee na safari.

Ushauri wake kwa jamii ni upi?

Ibrahim anaishauri jamii kulingana na uzoefu alioupata kupitia ugonjwa wa polio tangu mwaka 1996 na kupatiwa matibabu, japokuwa amebakiwa na ulemavu wa kupooza mguu hayo yote nilisimuliwa na mama yangu baada ya kufikia umri wa kujitambua, “anasema wazazi/walezi wasije kuwa kama baba yangu alie kata kunihudumia na kunipeleka hospitali akisema nimelogwa, hakikisheni mnawapeleka watoto kupata chanjo kila wakati unapofika ilikuepuka ulemavu wa kudumu na hata vifo wakati mwingine”.

Issa Ibrahim yupo wapi kwa sasa?

Ibrahim kwa sasa anaishi Dar es Salaam kwa mama yake mdogo, ambapo hivi karibuni Mh.Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewaagiza watendaji wa Wizara hiyo kumpatia kitengo ndani ya Wizara hiyo Nd.Ibrahim hususani kwenye kitengo cha elimu kwa umma ilikuendelea kuhamasisha chanjo ya polio nchini.

Hali ya mlipuko wa polio kwa sasa ikoje Tanzania?

Hata hivyo Dr. Anthony Kazoka amesema tangu mwaka 1996 hakuna kisa chochote cha mgonjwa wa polio nchini, na hii nikutokana na jitihada za serikali kupitia Wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la afya ulimwenguni (WHO) ofisi za Tanzania kuhakikisha wanadhibiti mlipuko huo kwa kuanzisha kampeini za utoaji chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano. 

Visa vya polio vimepungua kwa zaidi ya 99% tangu 1988, kutoka wastani wa visa 350,000 kwenye zaidi ya nchi 125 zenye ugonjwa huo hadi visa 175 vilivyoripotiwa mnamo mwaka 2019 duniani kote wakati huo Tanzania kukiwa hakuna kisa chochote cha polio tangu mwaka 1996, hatua iliyosababisha\\- WHO kanda ya afrika kuiweka Tanzania kwenye orodha ya nchi zilizo tokomeza mlipuko huo wa polio na kubakia kwenye nchi za Pakistan na Afghanistan.


Na, John Kabambala

Mwandishi wa habari za watoto Tanzania.

kabambalajohn@gmail.com

Post a Comment

0 Comments