Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

KATIBA NA SHERIA YA TANZANIA VINAKINZANA JUU YA UMRI WA KUOLEWA

 

Ndoa za utotoni ni tatizo nchini Tanzania linalo sababisha wasichana kutotimiza ndoto zao hasa za kielimu. Ndoa hizi mara nyingi husababishwa na baadhi ya vifungu vya sheria ya ndoa, hali duni za kimaisha, mila na desturi potofu, ukeketaji na ukosefu wa elimu juu ya madhara ya ndoa za utotoni.

Duniani kote inakadiriwa kuwa na wasichana Zaidi ya milioni 51 wenye chini ya umri wa miaka 18 walio olewa, Ndoa za umri mdogo zimekithiri Afrika Mashariki na Asia ya Kusini, tafiti zinaonesha kwamba kunauwezekano mkubwa kipindi cha muongo ujao zaidi ya wasichana milioni 100 watakuwa wamekumbwa na ndoa za umri mdogo endapo hatua za kuzuia jambo hili hazita chukuliwa hivi sasa.

TATIZO NI NINI?

Tanzania ni moja ya nchi zilizokithiri kwa ndoa za umri mdogo duniani, Kutokana na takwimu za TDHs za mwaka 2015/16 zinaonyesha wasichana 2 kati ya wasichana 5 wanaolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Hii ni hatari na inapelekea idadi kubwa ya wasichana wadogo kupoteza malengo yao, haki zao za msingi na hata wengine kupoteza Maisha.

Leo nimejikita kuangazia nyaraka mbali mbali zilizo wahi kuchapishwa zinavyo zungumza juu ya umri upi ni sahihi wa kuoa au kuolewa nchini Tanzania. 

CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?

Kifungu cha 13 na 17 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ni kinyume cha Ibara ya 12,13 na 18 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inatoa haki sawa kwa wote mbele ya Sheria.

Katika Sehemu ya pili ya Sheria ya Mtoto ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2009, katika mada inayo zungumzia “Haki na Ustawi wa Mtoto” inatoa tafsiri ya neno “Mtoto” kua ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka kumi na nane atajulikama kama mtoto.

 Mkataba wa kimataifa wa haki za watoto wa mwaka 1989 (uncrc) ambao Tanzania imeuridhia kutumika nchini, katika kipengere cha kwanza (1) cha mkataba huu kinamtambua mtoto kuwa ni yule alie chini ya umri wa miaka 18.

Kwamujibu wa chapisho lililo chapshwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), linasema Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 haiwalindi wasichana dhidi ya kuolewa, Sheria hii imekuwa ikipigiwa kelele ifanyiwe marekebisho kwa mda mrefu. 

Tatizo la Sheria hii inaruhusu wasichana wenye miaka 14 kuolewa kwa (ruhusa maalum ya wazazi), inaruhusu wasichana wenye umri kuanzia miaka 15 kuolewa iwapo umbile lao linaonekana kubwa, hali hii ina athari kwa maendeleo ya mtoto wakike, jamii na Taifa.

Utafiti nilioufanya mtandaoni kuhusu mada ilio ongoza kutafutwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia August- October,2022 nchini Tanzania, ni ndoa za utotoni ukilinganisha na mimba za utotoni, mwezi August mimba za utotoni mada hii haikutafutwa kabisa wakati ndoa za Utotoni kwakipindi chote hicho taarifa hiz zilitafutwa zaidi.

  Kwa mujibu wavuguvugu la jitihada za kutetea haki za wanawake na wasichana Tanzania (TAPO) lililo chapishwa mwezi September 2022, linasema “Msimamo wetu, kwa kuzingatia utawala wa Sheria na uwajibikaji wa mihimili yetu ya nchi, sisi kama tapo la wanawake na wasichana Tanzania haturidhishwi na kasi ya mchakato wa kubadilisha Sheria ya Ndoa. 

Aidha, tunapenda kuonyesha msimamo wetu kuhusu kuto kukubaliana na msimamo wa Serikali kusema kwamba mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Ndoa umerudishwa kwa wananchi kabla ya kufanya marekebisho ya Sheria hii. 

Ikumbukwe kuwa Mahakama katika shauri la Rebeca Gyumi iliamuru Serikali kufanya marekebisho ya sheria ndani ya mwaka mmoja na kusahihisha vifungu vya kibaguzi vya 13 na 17 na kuweka miaka 18 kama umri wa chini unaostahili kwa ndoa kwa wavulana na wasichana.

Ucheleweshwaji huu wa kufanya mabadiliko haya muhimu yanawafanya wasichana kuendelea kupitia ukatili wa ndoa za utotoni sababu bado vifungu kandamizi vya Sheria ya Ndoa vinaendelea kuwepo. Na katika kipindi kifupi kati ya Novemba 2021 na Februari 2022 kuna matukio mengi ya wasichana kuozeshwa ambapo mengi yao yamepelekea vifo vya wasichana wadogo yakiwemo\\;

Taarifa ya kujinyonga kwa binti Rebeca Benjamini mkazi wa Mkoa wa Geita, Kata ya Izunya, Wilaya ya Nyang’hwale mwenye umri wa miaka 17 kulikosababishwa na msongo wa mawazo sababu ikiwa ni athari za kuolewa katika umri mdogo. 

‘’Rebecca amefariki dunia baada ya kujinyonga hadi kupoteza maisha kwa kutumia Kamba iliyosukwa kwa chandarua kwenye kenchi ya nyumba yake, chanzo alikuwa alikuwa akilalamika kwamba kwanini kila akiolewa anaachika na tayari alikuwa aeshaachika mara tatu’’ Henry Mwaibabe, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita.

Taarifa ya kisa kilichotokea Mkoa wa Songwe, kijiji cha Ilanga, kata ya Mlale, kilichomuhusisha mtoto wa miaka 16 kumuua mkewe wa miaka 16 kisha kumchoma moto na kumtupa kwenye korongo.  

Pamoja na tukio lililotokea Mkoa wa Kigoma, Kijiji cha Lufubu, Wilaya ya Uvinza, lililomuhusisha binti Mbaru Juakali (17) kulazimishwa kuolewa kwa ng’ombe 13, ambapo baada ya kukataa alipigwa fimbo na baba yake hadi kupelekea kifo chake”.

Baada ya tamko hilo kutolewa na TAPO, Mnamo September 28, Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ilitoa nyarakaka yake yenye kichwa cha habari kinacho sema Taarifa kwa Umma kuhusu Ukusanyaji Maoni ya Maboresho ya Sheria ya Ndoa. 

Hata hivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita bado utafiti wangu unaonyesha taarifa kuhusu ndoa za utotoni zimeendelea kutafutwa zaidi kwa njia ya mtandao nchini Tanzania, ikilinganishwa na mimba za utotoni.

 Kwa mujibu wa nyaraka hiyo ya Serikali iliosainiwa na Dkt.Damas Daniel Ndumbaro (Mb) na Waziri wa Katiba na Sheria, inaonesha Wizara inaendelea kukusanya na kuchambua maoni zoezi hilo likikamilika, Wizara itawasilisha Bungeni mapendekezo ya maboresho ya Sheria husika kwa ajili ya kujadili na hatimaye kupitiashwa. Na zoezi hilo la ukusanyaji maoni linaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na Lindi. Nyaraka hiyo inasema.  

Taasisi ya Msichana Initiative na Twaweza Nisisi, kupitia chapisho lao linalo husu Ndoa za Utotoni Tanzania wanasema, Wanawake wanne kati ya kumi (37%) wenye umri wa miaka 15\\-49 wanaoishi Tanzania vijijini waliolewa wakiwa watoto, ikilinganishwa na wanawake wawili kati ya kumi (21%) wanaoishi maeneo ya mijini.  

NINI KIFANYIKE?

Tapo la wanawake na wasichana Tanzania linapenda kuona yafuatayo ya kifanyika\\;

Wabunge kupitia Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakitekeleza jukumu lao la kikatiba la kuitaka Serikali ilete mswada kwaajili ya mabadiliko ya Sheria ya Ndoa.

Wizara ya Katiba na Sheria kusitisha mchakato wa kukusanya maoni kwa wananchi na kujielekeza kwenye kutekeleza maamuzi ya Mahakama Rufani kama Ilivyoelekezwa kwenye hukumu ya kesi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Rebeca Gyumi.

Shirika la Plan International linashauri vyombo vya habari vichukue jukumu la kutekeleza sharia, Kutetea wanawake kama kiongozi wa jamii.

Nyaraka zilizo husika kukamilisha Makala hii ni, Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Ndoa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Mtoto ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyaraka kutoka Tapo la wanawake na wasichana Tanzania, Msichana Initiative, Twaweza Nisisi, Tamwa, Mkataba wa Kimataifa wa haki za Mtoto (uncrc).

Na, John Kabambala.

Post a Comment

0 Comments