Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

BAADA YA MVUA KUBWA ILIO SABABISHA MAFURIKO MOROGORO

 

                                                                                                 

Wakati mataifa yote ulimwenguni yakitatizika kuzuia ongozeko la joto duniani,madhara ya mabadiliko ya tabianchi tayari yanadhihirika wazi katika maeneo mbalimbali kamavile  Njaa, Ukame na Mafuriko yanayoharibu  maisha ya mamilioni ya watu na kuwaweka katika hatari zaidi ya kukabiliwa na njaa, kukosa makazi, matatizo ya kiafya nahata kupelekea vifo vya watoto na wazee wasio weza kujiokoa wenyewe.

“Usiku ule kuanzia majira ya saa sita sitausahau, ulikuwa niusiku wa kuamkia January 13, 2023, mvua kubwa ilinyesha isiokuwa na miungurumo,radi wala upepo, kwa takribani masaa 7 hivi, ndio muda mvua ile iliutumia kunyesha, Manispaa ya Morogoro ilionekana kwa mwanga wa taa za umeme tu, nasio taa za magari barabarani, bilasha hata magari hayakuweza kuendelea na safari zake za usiku kama ilivyo kawaida siku zingine kusafiri usiku.

Haiukuwa rahisi kudhani kwamba maji ya mvua ile yangejaa ndani ya nyumba kiwango cha kimo cha futi tano vyumbani hata sebuleni,  kwa sababu nikiwa kitandani nilijua tu ni mvua ya kawaida”  Mwanabibi Sefuchuto miongoni mwa wa athirika wa mafuko Manispaa ya Morogoro.

Ninapo yaona mabaki ya madufutari na vitabu vyangu hivi najisikia uchungu, kwani mafuriko yaliingia chumbani kwetu usiku wa manane hata mama mdogo alisinzia fofo wakati bibi anagonga mlango kutuita tufungue, mimi ndio nilie anza kuamka, niliposhusha miguu chini ya kitanda nakanyaga maji kimo cha kufikia kiunoni kwangu.

Ndipo lipo anza kupiga kelele na mama mdogo akaamka nakufungua mlango wakati huo nikaona vitu vikaanza kuelea juu ya maji likiwemo begi langu la madafutari nguo za shule pamoja na viatu, nilikosa masomo kwa kipindi cha siku 10 hivi, lakini pia nilishindwa kuonana na marafiki zangu shuleni na kucheza pamoja, lakini sasa nimesharejea shuleni kuendelea na masomo huyo ni Samira Msemwa mwanafunzi anae soma darasa la sita shule ya msingi Azimio.

TATIZO LA MAFURIKO:

Tatizo huaribu miundo mbinu, makazi ya binadamu kamavile majengo ya nyumba, kusababisha njaa, magojwa nahata vifo kwa watoto wadogo, wazee na wanawake wasio weza kujiokoa wenyewe.

Mvua hiyo ilinyesha maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Morogoro ambapo mikondo ya maji ilitiririsha kiasi kikubwa cha maji yaliyosababisha mafuriko kwenye mitaa ya Azimio kasikazini  katika Kata ya Kihonda pembezoni mwa barabara kuu itokayo Dodoma kuelekea Dar es salaam.

Mafuriko hayo yalizingira makazi ya wananchi kwenye eneo hilo ambapo kwa tathimini ya makazi yalio halibiwa  nizaidi ya kaya 200 zilizingirwa na mafuriko hayo kati ya kaya 2192 kwa mujibu wa ofisi ya mwenyekiti wa mtaa wa Azimio, na kufanya kaya hizo kuhitaji msaada wa makazi, chakula na misaada mingine ya kibinaadamu.

CHANZO KIKUBWA CHA MAFURIKO HAYO:

Mwanabibi Sefuchuto ni mkaazi wa Azimio Kihonda baada ya kufanya mahojiano nae amesema, katika eneo hilo anazaidi ya miaka 20 tangu ahamie na kuishi kwenye makaazi yao hayo, na kila mwaka mvua hunyesha pasipo madhara kama yaliotokea mwaka huu.

“Chanzo kikubwa cha mafuriko hayo anasema ni baada ya ujenzi wa mradi wa reli ya mwendo kasi ulivyo anza, mifereji iliokuwa ikitiririsha maji kwa miaka yote hiyo na madaraja, wameibadilisha mwelekeo wake na mingine imezibwa kabisa, mafuriko yalio bomoa makazi yangu hapa mradi wa mwendo kasi wameweka daraja amabalo lina matundu sita (6) yakutolea maji, na matundu hayo yameelekezwa kwenye makaazi ya watu pasipo kuyatengenezea mtalo mkubwa unao endana na ukubwa wa daraja hilo.

Hivyo basi baada ya mvua kubwa kunyesha maji yalijaa kwenye mfereji wa zamani ambao hata hawakuujengea tangu wakandarasi walipo fanya mabadiliko ya ujenzi wa barabara ya Reli na kuweka madaraja mapya” amesema Mwanabibi Sefuchuto.

MADHARA YALIO JITOKEZA:

Watoto hawakwenda shule kwa kipindi cha karibu siku kumi (10) kwa sababu Vyakula vilisombwa na maji na yamesababisha ukosefu wa chakula cha kutosha, na hata watoto wasinge kwenda shule bila uhakika wa kula ukizingatia shuleni hakuna program ya chakula, vyombo vya ndani, magodoro, kuku walisombwa na maji, madafutari, vitabu, sale viatu vya shule vya watoto, mabegi, na nguo zetu zingine zikafukiwa kwa tope la maji hayo, kama unavyoona sasa ndio ninazifua.

NJIA IPI WALIITUMIA KUJIOKOA:

Unaona kwenye kijumba hiki ambacho kama cha gorofa ndipo tulipo ponea baada ya maji kujaa ndani kwenye vyumba vyote, tuliwachukua watoto tukawapandisha hapa juu na sisi wenyewe tukapanda hapa kusubiria msaada utakao tufikia pengine asubuhi, maana tulikaa hapa kuanzia saa tisa za usiku hadi saa moja  asubuhi sisi wakubwa tukashuka maji yalipo anza kupungua lakini vitu vingi vilikuwa visha sombwa na maji.

Mwenyekiti wa mtaa wa Azimio Ndg, Michael Bendera ameeleza chanzo cha mafuriko hayo kua ni  “mabadiliko ya eneo hili kwenye mtaa wangu, na mabadiliko haya yamesababishwa na ujenzi wa reli ya mwendo kasi,  zamani maji yalikuwa yanapita lakini sio kama ya awamu hii, Mitalo mingi imeelekezwa kupitisha maji kwenye eneo moja, madhara makubwa nikuharibika kwa makaazi ya watu na vyakula kusombwa na maji huku familia kubaki bila dira na watoto ndio walikuwa wahanga wakubwa wa njaa na elimu kwa takribani siku 10”.

Aidha Michael Bendera amesama kabla ya mvua hii kubwa haijanyesha  na ksababisha mafuriko alimfuata afisa mazingira wa Manispaa ya Morogoro kumuonyesha na kumueleza namna ya kuchimba na kuujengea mtalo maji ili hata mvua itakapo nyesha pasiwe na madhara kwa makazi ya wananchi, lakini hakuna hatua yeyote iliochukuliwa kupitia ofisi ya mazingira zaidi ya miezi sita sasa.

“Hata baada ya mafuriko afisa mazingira alikuja nikaenda nae hadi kwenye eneo hilo la mtalo uliosababisha madhara kwenye makazi ya wananchi, ilikuona tena uwezekano wa kuuongeza kina na kuujengea na afisa mazingira  mwenyewe alipokanyaga kwenye tope lililotuama viatu vilibaki humo,  richa ya kujionea hayo yote hakuna hatua yeyote mpaka sasa nina uhakika endapo mvua kubwa itanyesha tena kama sio kufa watu basi uharibifu mwingine utatokea”Alisema Michael Bendera.

Aalie kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini Albert Msando alisema “Chanzo cha mafuriko hayo sio ujenzi wa Reli ya mwendo kasi bali ni ujenzi holela usiofuata mipango miji”.

              SULUHISHO LAKE NILIPI:

Mwanabibi Sefuchuto matarajio yake na kilio chake kipo kwa mamlaka husika za serikali kuona ni njia gani itatumika kuhakikisha mtalo huo unatafutiwa ufumbuzi kwa kujengewa kuelekea mto ngerengere.

“Ofisi ya mazingira itekeleze ahadi zake juu ya kuongeza kina cha mtalo huo na kuujengea mwanzo wa daraja la mwendo kasi hadi mto ngerengere kama ambavyo wananchi wamtaa wa Azimio wamekubariana, na kama serikali haitaki kuchimba na kujengea mtalo huo wananchi wamsha pitisha kuchanga Tshs, 10,000/= kwaajili ya kununu mafuta ya greda litakalo chimba mtalo huo”, alisema Michael Bendera.

Kauli ya serikali kupitia kwa alie kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini Albert Msando, "ni kwamba wananchi wamejenga kwenye vyanzo vya maji, hivyo wanapaswa kuhama".

Na, John Kabambala-Morogoro.

Post a Comment

0 Comments