Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

CHAKULA NIMOJA YA SABABU YA UKATILI KWA WATOTO.


Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa FAO, linaonesha takribani asilimia 70 ya wakazi wa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania wanategemea kilimo kama njia ya kujipatia kipato sambamba na chakula na uhakika wa lishe bora.

Ingawa hali hiyo imekuwepo myakanenda myaka rudi, sasa ni tofauti kwa miaka ya hivi karibuni mabadiliko ya tabianchi yamekuwa ni mwiba mchungu ndani ya sekta hiyo ya kilimo na kuibua changamoto nyingine katika jamii hasa familia zenye kipato cha chini, ukosefu wamvua za kutosha katika misimu sahihi ya kilimo, husababisha upungufu wa chakula na baa la njaa katika familia nyingi na wahanga wakubwa wa janga hili ni watoto, wanaolazimishwa kufanyiwa vitendo vya ukatili ili wapate chakula kila siku.

TATIZO NI KUFANYIWA UKATILI WATOTO.

Matukio ya kubakwa, mimba na ndoa za utotoni, kulawitiwa, kuchomwa moto mikono watoto, kuunguzwa mikono na maji ya moto hata kuchapwa kupita kiasi, yanaendelea kuripotiwa siku hadi siku katika familia nyingi, vyombo vya ulinzi na usalama, mashirika ya kutetea haki za binadamu na hata viongozi wa dini macho na fikra za waliowengi hudhani tatizo ni kupolomoka kwa maadili kwenye jamii husika.

Jambo hili linapaswa kuangaliwa kwa upana wake kila mmoja kwa ngazi ya familia,jamii na taifa kwa ujumla wake juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, ikiwa chakula hakuna nyumbani, hakuna uhakika wa kupata kazi inayoweza kuingiza kipato kunauwezekano mkubwa wa familia hiyo kuwa na migogoro isiyo isha na kupelekea kusambalatika kwa familia hiyo na watakao athirika zaidi ni watoto maana watakosa mahitaji muhimu yakilasiku kama vile chakula na malazi.

Jedwari hili linaonesha uhalisia wa matukio hayo hasa mimba za utotoni katika Mkoa wa Morogoro, mwezi Julai-Septemba 2022.

CHANZO MJAWAPO CHA UKATILI KWA WATOTO NI NINI:

Kwa mujibu wa takwimu hizo kutoka ofisi ya afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro za mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2022 zinaonesha kwamba, Miongoni mwa sababu zinazo sababisha ongezeko la matukio haya ni umasikini wa kipato cha kutosha pamoja na ukosefu na uhakika wa chakula katika familia, hivyo watoto wanapokosa uhakika wa kupata chakula nyumbani ni rahisi kushawishiwa kwa vipande vidogo vya fedha na kufanyiwa ukatili hasa watoto jinsi ya kike kufanya ngono pasipo ridhaa yao.

Moorine Lwakatare ni msimamizi wa mradi wa kilimo hifadhi unaotekelezwa Mkoani Kigoma na shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa FAO nchini Tanzania ,anasema FAO kupitia mradi wake wa Ushirikiano wa Pamoja Kigoma (KJP) wameamua kuhuisha kikosi kazi cha taifa kinacho shughulikia kilimo hifadhi ili kupambana na mabadiliko ya tabianchi hasa kwa kuwaelimisha wakulima, mabadiliko hayo yanaathari kubwa kupungua kwa chakula kwenye familia nyingi nchini Tanzania.

“Mambo tunyo yaangalia katika kikosi kazi hiki cha taifa moja ni, kuidhinisha yale yaliyomo kwenye ripoti ya kitaifa kuhusu maeneo ambako Kilimo Hifadhi kinatekelezwa, Pili kukubaliana kwa pamoja maeneo ya msingi yatakayojumuishwa kwenye mifumo ya kitaifa na kikanda kuhusiana na Kilimo Hifadhi.

Tatu kujenga uelewa miongoni mwa wajumbe wa Kikosi Kazi Cha Kitaifa kuhusu kilimo hifadhi na kusaka mbinu za kupanua usambazaji wa mbinu hizo za kilimo na nne, kuandaa mpango kazi na bajeti kwa ajili ya majukumu ya kikosi kazi hiki, ili kufikisha elimu hii kwa wakulima kwa ajili ya kulima kwa faida na kupata chakula cha kutosha kitakachoweza kumfikisha mkulima katika msimu mwingine wa kilimo pasipo upungufu wowote kwenye kila kaya.

Katika kufikia malengo hayo tutakuwa na majukumu mahsusi ikiwemo kuandaa orodha ya Washiriki Wakuu Wa Kilimo Hifadhi Katika sekta binafsi na ya umma walio mstari wa mbele kusongesha teknolojia za kilimo hifadhi hapa Tanzania” alisema Moorine Lwakatare.

Joseph Makoye nimkulima kutoka katika kijiji cha dakawa Wilayani Mvomero anasema juu ya mabadiliko ya hali ya hewa amegeukia kilimo cha bustani ya nyaya kulingana na kilimo cha mazao ya mahindi kushindwa kuvumilia ukame.

“Niliandaa shamba hili hapa nilipo kwa ajili ya kupanda mahindi mwezi wa kumi na moja kama ambavyo ilivyo kawaida ya mvua za vuri, lakini mvua haikunyesha kwa wakati ikaja kunyesha mzi wa kumi na mbili nayo sio ya kulidhisha nikapanda hatimae mahindi yamekauka, nikaamua kupanda nyanya ambazo naweza kumwagilia na ninakuwa na uhakika kiasi furani cha kuvuna hata kidogo kuliko mahindi.

Pakiwa na maji kidogo ya kumwagilia kwenye la mahindi wakati wa jua kali unapo mwagilia mahindi yanaweza kudumaa na kushindwa kubeba kwa sababu unyevu utakua mdogo tofauti na mazao ya mbogamboga na nyanya, najua baada ya miezi miwili na nusu naweza kuanza kuvuna nya kidogo kidogo nakwenda kuuza ili nipate pesa ya kunua chakula cha familia ” amesema Joseph Makoye.

Dr.Kizito Mwajombe yeye ni afisa kilimo kutoka katika shirika la Sustanable Agriculture Tanzania (SAT) Mkoa wa Morogoro anasema kilimo wanacho wafundisha wakulima wengi nikulima kilimo hai ambacho hakitumii kemikali nyingi, bali watumie mbolea ya asili na kulima kitaalamu ili kupata uhakika wa chakula na mazao mengi zaidi hata akiba ya biashara kulingana na mabdiliko ya tabianchi pamoja na kulinda afya ya binadamu.

Wakulima wadogowadogo tunawafundisha zaidi kilimo cha mazao ya muda mfupi kamavile  mboga mboga ambayo huchukua siku kumi na nne hadi siku tisini, yanakuwa tiyari kuvunwa na kuuzwa” amesema Dr.Kizito Mwajombe.

UTATUZI WA JAMBO HILI NI UPI:

Moorine Lwakatare Wakulima sasa wanapaswa kukubaliana na mabadiliko ya tabianchi na mbinu zinazopendekezwa kutumia katika kilimo kama ambavyo shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa FAO lilivyo anza kuhamasisha kilimo hifadhi, ilikuendelea kupata mazao ya kutosha na kuondoa njaa katika familia, kwani janga hili linawasukuma watoto wadogo kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa ahadi ya kupewa fedha na chakula.

Wakulima tunao tegemea mvua tuanpaswa kuzingatia mbinu za wataalamu, hasa kilimo hifadhi ambacho hakisumbui udogo mara kwa mara, kulima kwa mzunguko na kuweka matandazo katika mazao ili kutunza unyevu unyevu, Joseph Makoye anasema.

Serikali kupitia Wizara ya kilimo na mashirika yanayo jishughulisha na kilimo kamavile FAO, WFP, SAT nawengine, wanapaswa kushirikiana ili kuipeleka elimu ya kilimo hai na kilimo hifadhi kwa kila mkulima kwaajili ya kupambana na baa la njaa kwenye kaya, Dr.Kizito Mwajombe.



Na, John Kabambala-Morogoro.

Post a Comment

0 Comments