Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MABADILIKO YA HALI YA HEWA SABABU YA MAGONJWA NA VIFO KWA WATOTO

Mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la joto yameongeza ueneeaji wa baadhi ya magonjwa yanayotokana na maji na vidudu vya magonjwa, na kupunguza uzalishaji wa chakula kwa baadhi ya watu walio katika mazingira magumu duniani kote, Kuna uwezekano mkubwa kwamba hasara za kiafya zinazosababishwa na dhoruba na mafuriko zitaongezeka karne hii ikiwa hakuna hatua za kukabiliana nazo.

Na katika jambo hili waathirika wengi wa janga hili ni watoto ambao seri zao bado hazijakomaa kuhimili misuko suko ya mawimbi makubwa ya joto, mvua kubwa, mafuriko na magonjwa yasio zoeleka kuwapata watoto, karne hii yanawapata.

Hatua za kukabiliana na hali ya hewa ili kulinda afya na kukabiliana na mafuriko ni pamoja na upangaji bora wa matumizi ya ardhi, uhamasishaji wa jamii, kupunguza hatari ya kupata huduma muhimu kama vile maji, nishati na chakula, na hatua za kusaidia kaya zilizo hatarini, hali ya tahadhari ya mapema kwa jamii hasa walio na makazi kwenye mikondo ya maji na vimbunga waweze kuchukua hatua za kuhama katika maeneo hayo ili kuepusha athari za kiafya na vifo.

TATIZO

Tatizo ni ongezeko la joto, ukame, mafuriko baridi kali na magonjwa yasio ya kawida kwa watoto, ripoti ya Unicef iliotolewa mwishoni mwa mwaka 2022, inaonesha kwamba mwaka 2020, karibu watoto milioni 740  sawa na mtoto 1 kati ya 3 ulimwenguni waliishi siku 83.54 zenye joto zaidi lenye nyuzi joto 35°C, na ripoti hiyo ya Unicef inaonesha kwamba, Ifikapo 2050 itafikia hali ya juu ya utoaji wa hewa chafu kwa takriban digrii 2.4 za ongezeko la joto, takwimu hii inatarajiwa kuongezeka hadi takriban milioni 816  sawa na watoto 2 kati ya 5 watakuwa wenye hatari zaidi.

Jedwari hapa chini linaonesha zaidi.

CHANZO

Sababu kuu ya ongezeko la tatizo hili duniani ni gesi chafu itokanayo na viwanda, ongezeko la idadi ya watu hutajwa pia kama sababu mojawapo, shughuli za maendeleo ya binadamu zinazo sababisha kuharibu mazingira na ukataji miti hovyo, vyombo vya moto kama vile Ndege, magari, pikipiki na vifaa vitumiavyo umeme majumbani, jambo lingine ni ukataji miti kwenye misitu pasipo kurejeshea miti mingine, hivyo moja kwamoja binadamu hutengeneza jangwa lisilo la asilia.

Tofauti ya hali ya hewa inahusishwa na usambazaji wa kijiografia, Magonjwa yanayoenezwa na ambayo yanajulikana kusababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa ni pamoja na malaria, dengue, homa ya bonde la ufa, homa ya manjano, mzunguko wa mafuriko na ukame huongeza magonjwa yanayosababishwa na maji kama vile typhoid na kipindupindu.

Leonard Kitindi msimamizi miradi kutoka shirika la CONASU anasema mabadiliko ya hali yahewa ni janga la kitaifa na kidunia, na jambo hili huathiri maeneo yote na viumbe vyote, kwa upande wa binadamu waathirika wakubwa zaidi ni watoto ambao kingazamili yao hazijakomaa kuhimili mawimbi mabdiliko ya hali yahewa.

 sisi kama CONASU baada ya kugundua chanzo cha tatizo hili, tumeanza kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji, kwa kupanda miti,kurejeshea maeneo ambayo yalisha katwa na kubuni njia nyingine za fursa za kibiashara zilizopo kwenye maeneo ya jamii, ilikujipatia kipato nasio kukata miti kama njia ya kujipatiakipato, mfano tuna mradi wa kurejesha miti aina ya mikoko kule Bagamoyo Mkoani Pwani” amesema Leonard Kitind.

Kwa mijibu washirika la afya ulimwenguni WHO, katika kipindi cha miaka 10  nchini Tanzania tayari kumeripotiwa matukio ya ugonjwa wa malaria hasa katika maeneo ya nyanda za juu ambayo kijadi yalikuwa hayana mbu na malaria kama Tanga, Kilimanjaro, Iringa, Kagera na Mbeya, miongoni mwa mengine, ambako hayakuwa yameenea hapo awali.

Malaria na kipindupindu ni miongoni mwa masuala muhimu ya afya ya umma hasa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na miongoni mwa wanawake wajawazito, uwezekano wa kuugua malaria mara nne zaidi kuliko wastani wa wakawaida jambo hili linashuhudiwa kuwa ni moja ya visababishi vya mabadiliko ya hali yahewa.

Kwa upande wa Daktari bingwa wa watoto Theopista Masenge kutoka chama cha madaktari bingwa wa watoto Tanzania (PAT) amesema athari ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa watoto nikubwa kuliko jamii inavyo ichukulia, mfano kwa sasa kunamagonjwa mbalimbali ambayo huwapata watoto kwa kujirudia rudia na mengine hayakuzoeleka katika jamii.

Hali ya joto,baridi kali,mafuriko yasababishwayo na mvua kubwa, ukame na upungufu wa maji safi na salama yanapozidi huongezeza magonjwa yasio eleweka kwa watoto, mfano kwa mujibu wa ripoti ya masuala ya afya ilio tolewa hivi karibuni ya mabadiliko ya hali ya hewa ya asili inaonesha kwamba “Zaidi ya nusu ya magonjwa yanayojulikana ya binadamu yanaweza kuchochewa na mabadiliko ya hali ya hewa”. Dr. Theopista Masenge.

Kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyozinduliwa jijini New York Marekani mwishoni mwa mwaka 2022 na shirika la UNICEF ,inaonesha kwamba watoto milioni 559 kwa sasa wanakabiliwa na joto Kali ulimwenguni kote.

Hali hiyo inategemewa kuwa mbaya zaidi ifikapo mwaka 2050, watoto wote duniani ambao wanakadiriwa kuwa bilioni 2.02 watakuwa wameathiriwa na mawimbi tofauti ya joto kali bila kujali wapo kusini au kaskazini mwa dunia, na vile vile bila kujali ongezeko la joto litakuwa katika kiwango cha wastani wa nyuzi joto 1.7 katika kipimo cha Selsiyasi au kiwango cha juu cha nyuzi joto 2.4 katika kipimo cha Selsiyasi.

Ripoti hiyo inaionesha Tanznia kuwa nimiongoni mwa nchi zilizo kwisha onja janga hilo la mabadiliko ya hali ya hewa hasa kuongezeka kwa joto na kuwaathiri watoto, ambapo kwa kipindi cha mwaka 2020 zaidi ya watoto milioni tano sawa na asilimia kumi nasaba waliathirika na joto kali, na inakadiriwa kuongezeka zaidi ifikapo mwaka 2050 kama jedwri linavyo onyesha hapa.

 

 

 

 

Tanzania

MWAKA

WATOTO WALIO ATHIRIKA KWA MAWIMBI YA JOTO.

 

ASILIMIA

MUDA WA MAWIMBI YA JOTO

ASILIMIA

2020

5.2 million

17%

-

-

 

WATOTO WATAKAO ATHIRIKA KWA MAWIMBI YA JOTO.

 

MUDA WA MAWIMBI YA JOTO WATOTO WATAKAO PITIA.

 

2050

35.4 million

100%

26.3 million

74%

 
Asha Juma mkazi wa Bigwa Manispaa ya Morogoro yeye anazaidi ya miaka 50 anasema kila mwaka unapo isha, hali inabadilika na mabadiliko haya yanawasumbua zaidi watoto wadogo, “kilasiku unakuta mtoto na mama yake wapo hospitali asubuhi mchana na jioni, ukiingia ndani ya nyumba ambayo inawatoto utakutana na mabox tofauti tofauti ya dawa za watoto, kwa sababu leo ana ugonjwa huu na kesho ana ugonjwa huu kila ugonjwa una aina ya dawa yake, hivyo haya mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri zaidi hiki kizazi tofauti na enzi zetu” 

                           

                           KIPI KIFANYIKE KUREJESHA HALI YA AWALI:

Ripoti ya UNICEF imeshauri kwamba:- kila nchi lazima ibadilishe huduma muhimu za kijamii WASH, afya, elimu, lishe, ulinzi wa kijamii ili kuwalinda watoto na vijana, ikiwa nipamoja na utungaji wa sera maalumu na miongozo juu ya athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa.

Bi, Asha Juma anashuri, Serikali na wanasiasa wanapaswa kuchukua hatua za maksudi na sio kungojea tena, maana hakuna dunia nyingine isipo kua nihii pekeyake, udhibiti wa uchafuzi wa hewa kwenye viwanda, uchomaji misitu nk.

“Hili siojambo tena la kuingalia na kusubiria Serikali kuweka amri bali, ni kila mmoja wetu kuchukua hatua maana mabadiliko ya hali ya hewa hayachagui pakuharibu, tupande miti, tupunguze matumizi ya kukata kuchoma mioto kwenye misitu yetu ya asili na tuvilinde vyanzo vyetu vya maji” Leonard Kitindi.

Dr. Theopista Masenge yeye anashauri kila mwananchi apande miti kuzunguka maeneo yake yakuishi, mashamba yake lakini pia kuna ulazima wa kupima afya mara kwa mara familia nzima na hasa watoto, ilikubaini endapo kuna ugonjwa wowote na kuchukua hatua mapema.

Na, John Kabambala-Morogoro.

Post a Comment

0 Comments