Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

UGONJWA WA SURUA NI HATARI KWA WATOTO KAMA HAWAKUPATA CHANJO

 

SURUA NI NINI?: Surua ni ugonjwa hatari sana unaoambukiza unaosababishwa na virusi, kabla ya kuanzishwa kwa chanjo ya surua mwaka wa 1963, magonjwa makubwa ya mlipuko yalitokea takriban kila baada ya miaka 2-3 na Surua ilisababisha wastani wa vifo milioni 2.6 kila mwaka.

Zaidi ya watu 140,000 walikufa kutokana na surua mwaka 2018 - wengi wao wakiwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5, licha ya kuwepo kwa chanjo salama na yenye ufanisi.

SASA HALI IKOJE KUHUSU CHANJO YA SURUA?

Nimefanya mahojiano maalumu na mtaalamu wa chanjo kutoka Manispaa ya Morogoro  Dr.Philipo  Bwisso amesema, Surua husababishwa na virusi kwa kawaida hupitishwa kupitia mguso wa moja kwa moja na kupitia hewa, Virusi huambukiza kwa njia ya upumuaji, kisha huenea mwilini, Surua ni ugonjwa wa binadamu na haujulikani kutokea kwa wanyama.

DALILI ZA UGONJWA WA SURUA NI ZIPI?

Nimezungumza na Dr.Philipo  Bwisso mtaalamu na Mratibu wa Chanjo kutoka Manispaa ya Morogoro amesema, miongoni mwa dalili za ugonjwa wa surua ni kama vile homa kali, ambayo huanza siku 10 hadi 12 baada ya kuambukizwa na virusi, na huchukua siku 4 hadi 7, kikohozi, baada ya siku kadhaa hupata upele, na huendelea kwa siku 5 hadi 6, na kisha huisha. Vifo vingi vinavyohusiana na surua husababishwa na matatizo yanayohusiana na ugonjwa huo, matatizo makubwa hutokea zaidi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5, au watu wazima zaidi ya umri wa miaka 30.

KUNA MATATIZO YEYOTE HUMPATA MGONJWA WA SURUA?

Matatizo makubwa zaidi ni upofu, maambukizi ambayo husababisha uvimbe wa ubongo, kuhara na upungufu wa maji mwilini, magonjwa ya kuambukiza kama vile pneumonia, Surua ina uwezekano mkubwa wa kuwapata watoto wadogo wenye lishe duni, hasa wale walio na upungufu wa vitamini A, au ambao kinga zao zimedhoofika kutokana na VVU/UKIMWI au magonjwa mengine.

NANI YUKO HATARINI?

Dr. Philipo  Bwisso anabainisha zaidi kuwa ni Watoto wadogo ambao hawajachanjwa wako katika hatari kubwa zaidi ya surua na matatizo yake, ikiwa ni pamoja na kifo, Wanawake wajawazito ambao hawajachanjwa pia wako katika hatari, Mtu yeyote asiye na kinga (ambaye hajachanjwa au hajapata chanjo lakini hakupata kinga) anaweza kuambukizwa.

Surua inaendelea kutokea hasa katika nchi nyingi za Afrika na Asia, ambapo idadi kubwa (zaidi ya 95%) ya vifo vya surua hutokea katika nchi zenye kipato cha chini kwa kila mtu na miundombinu dhaifu ya afya.

Sophia Mgeta ni mkaazi wa kijiji cha Dumila katika halimasahauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro na ni baba wa watoto wawili, amenieleza namna alivyo anza kuona dalili za ugonjwa wa Surua kwa mtoto wake, “Tulianza kuona mtoto wetu mkubwa anapata homa kasha upele ulio samba mwili mzima jambo ambalo lilinisababisha nimpeleke kwenye kituo cha afya cha Roma kilichopo hapa Dumila.

Baada ya kfika huko daktari alivyo mpima na kumpatia huduma akatuuliza huyu mtoto wenu aliwahi kupewa chanjo ya Surua ? Tukamjibu hakuwahi kuchomwa sindano ya Surua, alitwambia kuwa mtoto ameugua ugonjwa wa Surua kwa sababu hajawahi kupata chanjo ya Surua, hivyo nimuhi sana na nilazima mtoto apewe chanjo ya Surua hatua kwa hatua”Alisema Sophia Mgeta

SURUA INAAMBUKIZAJE?

Chapisho la WHO limebainisha kwamba, Surua ni mojawapo ya magonjwa yanayoambukiza zaidi duniani. Huenezwa kwa kukohoa na kupiga chafya, kugusana kwa karibu kibinafsi au kugusana moja kwa moja na ute ulioambukizwa wa pua au koo.

Virusi hubaki hai na huambukiza hewani au kwenye nyuso zilizoambukizwa kwa hadi saa 2. Inaweza kuambukizwa na mtu aliyeambukizwa kutoka siku 4 kabla ya kuanza kwa upele hadi siku 4 baada ya kutokea kwa upele.

Milipuko ya surua inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko ambayo husababisha vifo vingi, haswa kwa watoto wachanga, wenye utapiamlo, katika nchi ambazo ugonjwa wa surua umeondolewa kwa kiasi kikubwa, visa vinavyoagizwa kutoka nchi nyingine vinasalia kuwa chanzo muhimu cha maambukizi.

KUPITIA CHANJO YA SURUA KUNA MATAKEO YEYOTE?

Kwa mujibu wa chapisho hilo lililo chapishwa Mwezi March, 2023, na Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika inaonesha kwamba, linasema Chanjo ya Surua imekuwa na matokeo chanya katika kupunguza vifo vya surua, kama chati inavyo onesha hapa.

MATIBABU YAKE NI YAPI? Milipuko ya ugonjwa surua inaweza kupunguzwa kupitia huduma ya ambayo inahakikisha lishe bora, unywaji wa maji ya kutosha na matibabu ya upungufu wa maji mwilini unaopendekezwa na WHO, Suluhisho hili linachukua nafasi ya maji na vipengele vingine muhimu vinavyopotea kwa njia ya kuhara au kutapika.

Watoto wote waliogunduliwa na surua wanapaswa kupokea dozi mbili za virutubisho vya vitamini A, wakipewa muda wa saa 24 tofauti, matibabu haya hurejesha viwango vya chini vya vitamini A wakati wa surua ambayo hutokea hata kwa watoto walio na lishe bora na inaweza kusaidia kuzuia uharibifu wa macho na upofu, Virutubisho vya vitamini A pia vimeonyeshwa kupunguza idadi ya vifo vya surua.

NJIA GANI YAWEZA KUTUMIKA ILI KUZUIA UGONJWA WA SURUA?

Dr. Philipo  Bwisso anasema wazazi au walezi wa watoto hawapaswi kabisa kuacha kuwapeleka watoto kiliniki ilikupatiwa chanjo ya Surua, tena kwa dozi kamili ikiwa nipamoja na kukamilisha chanjo zingine zinazotolewa kwa ajili ya kumkinga mtoto dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Sita sahau jinsi ambavyo mtoto wetu alivyo tusumbua wakati wote nikulia tu, Nawashauri ndugu, jamaa, marafiki na wazazi walio na watoto au ambao wanatarajia kupata watato nimuhimu kuzingatia chanjo kzote zinazowahusu watoto, tuwapeleke kwenye vituo vya afya ilikulinda afya zao,alisema Sophia Mgeta

Na, John Kabambala-Morogoro.

Post a Comment

0 Comments