Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MIKUNDE CHANZO CHA LISHE BORA KWA MTOTO

 

Tanzania, mazao jamii ya mikunde yanashika nafasi ya pili kwa ulaji, ikiwa nyuma ya mazao ya nafaka. Mara nyingi mazao haya ya mikunde yamekuwa yakiliwa kama mboga pamoja na nafaka, baadhi ya mikunde kama kunde na maharagwe, majani na matawi yake yamekuwa pia yakiliwa kama mbogamboga.

 Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linatafsiri kuwa mikunde ni jamii ya mimea ya kunde ambayo imekaushwa, inajumuisha aina zote za mbaazi, dengu, kunde, choroko, njugu mawe na maharagwe.

Mikunde, karanga na mbegu za mafuta ni vyanzo vya protini ambavyo ni vya bei nafuu, na vyanzo vizuri vya madini ya chuma, zinc, fosforasi, magneziamu, vitamini B, foleti na nyuzi nyuzi.

"Kote duniani na katika bara la Afrika, kumekuwa na ongezeko la uzalishaji wa mazao haya ya mikunde. Kwa mfano, kwa takwimu za FAO 2014, Tanzania inaongoza Afrika kwa uzalishaji wa maharage (tani milioni 1.2), inaongoza kwa uzalishaji wa dengu (tani 150,000), ni moja kati ya nchi tatu zinazoongoza kuzalisha zao la mbaazi na ni moja kati ya nchi tano zinazoongoza kuzalisha zao la kunde (tani 191,000).

Pamoja na nchi yetu kujitosheleza kwa chakula, bado Tanzania inakabiliwa na utapiamlo ambapo theluthi ya Watoto wamedumaa, theluthi ya wanawake wana upungufu wa damu na theluthi moja ya wanawake wana uzito uliozidi. Njombe, pamoja na kuwa ni moja kati ya mikoa inayoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa chakula nchini, inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya Watoto wenye udumavu asilimia 50.4 kulingana na taarifa za Demografia ya Wizara ya Afya (TDHS 2022)" Hayo yalizungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Juma Sweda, siku ya kilele cha maadhimisho ya Mikunde Duniani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Athony Mtaka ambapo kitaifa yalifanyika Mkoani Njombe.

  Akiongea kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Dr. Nyabenyi Tipo, Afisa lishe kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Bi Stella Kimambo,  alisema Mazao jamii ya Mikunde yanafaida kubwa katika miili ya Bidamu, lakini pia hurutubisha udongo, na mazo hayo nimojawapo ya chanzo cha kupata protini, vitamin na uimalishaji wa kinga za mwili.

TATIZO NI NINI:

Familia nyingi zimekuwa zikiyachukulia mazao ya mikunde kama chakula cha watu masikini na hivyo kupunguza ulaji wake, mlo wa kawaida hauoneshi uwepo wa mikunde, Watu wengi hula maharagwe lakini mbaazi, choroko na dengu hupatikana kwa nadra katika milo ya kawaida, pamoja na kuwa na virutubisho vingi na kuuzwa kwa bei nafuu ukilinganisha na maharagwe.

Tanzania ni mzalishaji muhimu wa mikunde katika ukanda wa Afrika Mashariki, Mwaka 2021, Tanzania inakadiriwa kuwa ilizalisha tani milioni 1.8 ya mikunde na zao hili ni miongoni mwa bidhaa muhimu zinazouzwa kwa wingi nje ya nchi.

Mwaka huo huo, Tanzania iliuza nje ya nchi mikunde yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 269, kutoka Dola za kimarekani milioni 193 mwaka 2020, Karibu asilimia 85% ya mauzo ya mazao haya yamekuwa yakiuzwa nchini  India.

 Pamoja na umuhimu wake kwa upande wa lishe, mwenendo wa ulaji wa mikunde nchini umekuwa ukipungua siku hadi siku, na kusababisha matatizo ya utapiamlo kwa watoto na watu wazima.

CHANZO CHA TATIZO:

Sababu zinazosababisha tatizo hili ni hulka kwa baadhi ya kaya, kama vile tabia za ulaji wa chakula, mabadiliko ya mapenzi ya mlaji, na kushindwa kwa wauzaji kuwianisha sifa za mikunde na mapenzi ya mlaji, idadi ya wanakaya, na upatikanaji wa rasilimali na mengineyo, jambo ambalo linaweza kupelekea ulaji mdogo kwenye familia. 

Kwa sababu hiyo jamii inapaswa kuona umuhimu zaidi katika ulaji wa vyakula vyenye wingi wa protini ili kupunguza utapiamlo, na magonjwa yasiyoambukizwa hasa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (5).

 Afisa kilimo na mratibu wa masuala ya lishe kutoka Wizara ya Kilimo Tanzania Margreth Natai amesema mazao jamii ya mikunde yapo mengi, yanayo paswa kutumika kila siku katika mzunguko wa milo ya kila familia, ili kuwa na lishe bora, ikiwa nipamoja na kuondoa udumavu kwa watoto, kuongeza damu kwa mama wajawazito na hata wasichana walio katika umri wa kuzaa.

 Kwa upande wa mtandao wa mazao jamii ya mikunde Tanzania (TPN) kupitia kwa mratibu wa mtandao huo Ndg. Zirack Andrew, amesema mtandao huo unahamsisha wakulima na jamii nzima kwa ujumla kulima mazao jamii ya mikunde na jinsi ya kuyatumia, kwani yanabidhaa nyingi zaidi ambazo mkulima atanufaika nazo kiuchumi mbali na faida ya kupata chakula bora.

 Kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria Vya Malaria Tanzania wa Mwaka 2022  na Viashiria vya Hali ya Lishe inaonesha kwamba kiwango cha Udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka 5, Tanzania ilikua na asilimia 34% mwaka 2015/16, na asilimia 30% kwa kipindi cha mwaka 2022, ikiwa imepungua kwa asilimia 4 tu kwa kipindi cha miaka 5.

Afisa lishe mtafiti mwandamizi Vumilia Lyatuu kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) amesema Taasisi hiyo inahamasisha wanachi kula kula vyakula ambavyo vinazingatia makundi mbalimbali ya vyakula, na hasa hutoa elimu ya namna ya mapishi bora yasiyo sababisha virutubishi vinavyo takiwa mlaji kuvipata vipotee wakati wakupika, mazao jamii ya mikunde ni miongoni mwa bidhaa muhimu katika afya na lishe ikiwa ni pamoja na kuimalisha kinga ya mwili.

Mkurugenzi wa shirika la People’s Care Initiatives Tanzania ( PCIT) Amina Mgeni wao wanahamasisha program ya chakula shuleni, lengo likiwa ni kuendelea kuongeza idadi ya wanafunzi shuleni kutunza afya zao na kuongeza ufaulu katika masomo, "katika mazao jamii ya mikunde ni miongoni mwa mazao tunayo hamasisha watoto wapikiwe shuleni hasa kupitia mradi wa AGRICONNECT ".

Mmoja wa wanafunzi kutoka kwenye shule ya msingi Itipingi ambayo ni miongoni kati ya shule kumi (10) zinazo nufaika na mradi AGRICONNECT unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), na program ya chakula shuleni Janeth Silvath amesema ladha ya chakula wanacho pikiwa kilicho changanywa kwa mazao jamii ya mikunde ni nzuri na kila lishe ya kutosha  “Utoaji wa Chakula shuleni ni jambo muhimu sana na nina naomba wazazi na kamati ya shule zingine waanzishe program ya kula chakula shuleni kama hii”. 

SULUHISHO LA TATIZO HILI:

Stella Kimambo-Afisa lishe kutoka FAO.

FAO kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo pamoja na Taasisi za serikali, Mtandao wa Mazao Jamii ya Mikunde Tanzania na wadau wa maendeleo katika wiki ya mikunde Tanzania tuweza kuendeleza yafuatayo 1, kuwajengea uwezo wapishi kutoka katika shule zinazotekeleza mradi wa AGRICONNECT  Mkoa wa Njombe, pia Baba na mama lishe katika Suala la Mapishi mbalimbali ya mazao jamii ya mikunde,2) Wanafunzi wa Shule za Msingi zinazotekeleza programu ya Utoaji Chakula Shuleni Mkoa wa Njombe, kushirikishwa zaidi kwa wanafunzi kufanya chemsha Bongo, kuchora picha mbalimbali kwa kutumia mazao jamii ya mikunde” amesema Stella Kimambo .


Hata Wizara ya Kilimo Inapendekeza kwamba; 

-Wizara kutoa kipaumbele kwa mazao ya mikunde kwa kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora na viuatilifu ili kuongeza uzalishaji na tija

-Wizara kufanya mapitio ya Mkakati wa Mikunde wa mwaka 2016 -2020 ili kuingiza masuala mapya yanayojitokeza na ili kuendana na hali ya sasa.

-Wizara kuendelea kuhamasisha jamii umuhimu wa kuzalisha mazao ya mikunde na kuhamasisha matumizi yake

-Wizara kuendelea kusimamia na kutoa taarifa za masoko (ya ndani na nje) kwa mazao ya mikunde ili kuwasaidia wakulima kufanya biashara zenye tija.

Maadhimisho haya yafanyike kila mwaka ili kuhamasisha jamii kuzalisha na kutumia mazao haya muhimu kiafya, kiuchumi na kimazingira.

Na, John Kabambala-Njombe.

Post a Comment

0 Comments