Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI SULUHU KWA WATOTO WAKIKE

 

Picha na Kheel Center/Flickr

Hebu nikurejeshe nyuma kidogo kuhusu historia fupi ya kuanzishwa kwa Siku hii ya Wanawake Duniani, Mnamo Machi 25, 1911 Kiwanda cha nguo cha Kampuni ya Triangle Waist cha New York Marekani, kiliungu kwa moto ambao uiligharimu maisha ya wafanyakazi 146 vifo hivyo vilitokea chini ya dakika 20 tu, na wengi wakiwa ni  wahamiaji vijana.

Baada ya Vita kuu ya pili ya dunia, Machi 8 ilianza kusherehekewa katika nchi kadhaa, Mnamo 1975, Umoja wa Mataifa ulianza kuiadhimisha siku hii kama Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Miaka miwili baadaye, Desemba 1977, Baraza Kuu lilipitisha azimio la kutangaza Siku ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Wanawake na Amani ya Kimataifa kuadhimishwa siku yoyote ya mwaka na Nchi Wanachama, kwa mujibu wa mila zao za kihistoria na kitaifa.

Tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa na mashirika yao wamefanya kazi bila kuchoka ili kupata usawa wa kijinsia duniani kote na matokeo makubwa yamepatikana: mwaka 1995 Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji, ramani ya kihistoria iliyotiwa saini na serikali 189, ilizingatia maeneo 12 muhimu ya wasiwasi, na kujumuishwa kwenye Lengo namba 5 la malengo endelevu ya kudumu ya Umoja wa Mataifa “Ili Kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana wote” katika Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.

Waliokufa kwa janga hilo la moto, wengi walikuwa wasichana wenye umri kati ya miaka 14,15,16 na 17, idadi yao ilikuwa 146 vifo hivyo vilitokea chini ya dakika 20,hao ni walioshindwa kujinasua kutoka kwenye moshi na moto huo, hili likiwa ni moja ya majanga mabaya zaidi tangu kuanza kwa Mapinduzi ya Viwanda nchini Marekani, kwa mujibu wa Smithsonian Magazine, bofya link hii ilikusoama zaidi. https://www.smithsonianmag.com/smart-news/american-garment-workers-who-helped-inspire-international-womens-day-180962364/#gXHV6kiTelvQEssi.99   .

Miongoni mwa wasichana waliofariki katika ajari hiyo ya moto ni Kate Leone alikuwa na umri wa miaka 14 wakati moto huo ulipotokea. Mzaliwa wa Marekani, alikuwa ameishi Marekani kwa maisha yake yote, Alizikwa kwenye makaburi ya Calvary mnamo Machi 28, 1911, bofya link hii ilikusoama  https://trianglefire.ilr.cornell.edu/victims/72.html

Na, Rosaria Maltese alikuwa na umri wa miaka 14 wakati moto huo ulipotokea. Mzaliwa wa Italia, alikuwa ameishi Amerika kwa miaka 4. Alizikwa kwenye makaburi ya Calvary mnamo Machi 28, 1911, hawa wote walikuwa wanafizikia, bofya link hii ilikusoama https://trianglefire.ilr.cornell.edu/victims/82.html .

NCHINI TANZANIA HALI IKOJE?

Siku hii ya Wanawake Duniani wanawake na wasichana ulimwenguni pote hutumia siku hii kuzungumzia changamoto na vikwazo wanavyo kumbana navyo, katika maeneo ya kazi, shuleni na hata nyumbani ambapo nchini Tanzania wasichana wankabiriwa na ndoa za utotoni ambacho nikikwazo kikubwa katika maendeleo ya msichana mwenyewe,familia na taifa kwa ujumla wake katika nyanja ya afya na uchumi.

Katika kuyawasilisha hayo kwa niaba ya Watoto Nancy Kasembo ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamuhuri ya Muungano Tanzania, alipozungumza nami kuelekea siku ya maadhimisho ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika March 8 ya kila Mwaka, juu ya umri upi ni sahihi kuoa/kuolewa, Sisi kama viongozi wa baraza la watoto Tanzania, Wizara ya Katiba na Sheria haijatushirikisha moja kwa moja kutoa maoni yetu juu ya umri upi ni sahihi wa kuoa/kuolewa, isipokuwa tunatoa maoni yetu kupitia vikao vyetu ambavyo tuna kaa na Wizara ya Maendele ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi maalumu” .

MATATIZO YANAYO WAKUMBA WATOTO WAKIKE NI YAPI?

Kupata mimba kabla ya wakati, hatari ya kukumbwa na matatizo kipindi cha ujauzito na wakati wa kujifungua, Vifo vya ghafla, Utapiamlo, Wasiwasi na mafadhaiko, viwango duni vya elimu ya msingi na ujuzi wa kusoma na kuandika, Ndoa za utotoni huendeleza umaskini, kuingia katika maisha ya matarajio duni, hatari kubwa ya vurugu katika familia, unyanyasaji, na vifo vya mapema.

SIKU HII NI SULUHU YA VIKWAZO KWA WANAWAKE NA WASICHANA?

Mchakato wa kuitafuta haki ya kutoozeshwa chini ya umri wa miaka kumi na nane (18) kwa watoto wakike, safari hii ilianzishwa na mwana harakati wa kutetea haki za watoto wakike nchini Tanzania mnamo mwaka 2016 Rebeca Gyumi, Na hapa nimemtafuta Wakili kutoka katika Taasisi ya Msichana Initiative Lucy Gidamisi yeye anaanza kwa kuelezea mchakato huu na hatua zilipo fikia hadi sasa…..Lucy Gidamis….. https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678136765--less-file-Lucy-Gidamisi-Wakil.mp3 

Nimezungumza na Dr. Rose Reuben Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), nilimuuliza ni jambo lipi ambalo mnatamani kulizungumza juu ya kuwa tetea watoto wakike ili Sheria ya ndoa iweze kubadilika katika kipindi hiki cha maadhimisho ya Wanawake Duniani?….Dr. Rose Reuben..  https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678214319--less-file-Ros.mp3

Na huu ucheleweshwaji unasababishwa na nini……Dr. Rose Reuben…https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678138822--less-file-Dr.Rose-Reuben-.mp3 

Ndoa za utotoni ni tatizo nchini Tanzania linalo sababisha wasichana kutotimiza ndoto zao kielimu, Ndoa hizi mara nyingi husababishwa na hali duni za kimaisha, mila na desturi potofu na ukosefu wa elimu juu ya madhara ya ndoa za utotoni.

Nancy Kasembo mwenyekiti wa baraza la watoto la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, anaiona siku ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani kuwa ni mkombozi kwa watoto wakike, ambayo huazimishwa tarehe 8 /03 ya kila mwaka…. Nancy Kasembo… https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678137406--less-file-Nancy-Kasembo-.mp3  

Nancy nilimuuliza je, Wizara ya Katiba na Sheria nchini, imekwisha washirikisha moja kwa moja juu ya kutoa maoni ya umri upi ni sahihi kuoa/kuolewa kwa motto?......... Nancy Kasembo… https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678137506--less-file-Nancy-Kasembo-.mp3  

 Wizara ya Katiba na Sheria iliwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria kwa kuweka masharti ya kuusawazisha umeri wa kuoa/kuolewa na kuwa miaka 18. Hata hivyo umri wa Chini wa kuolewa Ulipendekezwa kuwa miaka 15 endapo masuala yafutayo yatazingatiwa, jambo hili limefanya nimtafute mataalamu ili kutoa ufafanuzi juu ya kipengele namba tano cha mambo yanayopaswa kuzingatiwa, kinacho sema “Dktr.Amethibitisha Mtoto anauwezo wa kuingia kwenye ndoa?”

 Daktari anathibitishaje kuwa mtoto anauwezo wa kuingia kwenye ndoa?  Swali hili nimemuuliza Theopista Jacob yeye Dktr. Bingwa wa masuala ya watoto kutoka chama cha Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania (PAT)……. Dktr. Theopista Jacob… https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678137609--less-file-Theosita-Jaco.mp3   

Kwa mujibu wa ripoti iliotolewa na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) iliopewa jina la “MAENDELEO JUU YA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVUya  mwaka 2022,inaonesha kwamba haki ya elimu kwa wasichana ni muhimu kwa kila mtu katika nyanja ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ukuaji wa uchumi na ustawi, kila mwaka wa ziada wa masomo unaweza kuongeza mapato ya msichana akiwa mtu mzima kwa hadi asilimia 20.

Ripoti hiyo iliolenga kuonesha usawa wa kijinsia katika Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambapo wasichana kutoka kwenye kaya maskini zaidi na katika maeneo ya vijijini mwelekeo haujawa sawa, miongoni mwa maeneo hayo ni Nchini Tanzania hali bado inaonesha kuwa chini, kama ambavyo chati inaonesha hapa.

Sampuli ya nchi 29 zilizo na Takwimu za hivi karibuni kwa wasichana wanaomaliza shule ya sekondari kwa jinsia, kwa wasichana maskini wanaotoka vijijini na wasichana matajiri wanaotoka mijini ni asilimia 11.5 hadi 72.2, hivyo katika siku za maadhimisho ya Wanawake Duniani ya kila mwaka ni lazima dunia ifahamu kwamba kundi la watoto wakike wanahitaji kuondolewa vikwazo na kutimiziwa haki zao za msingi ikiwemo ya kupata elimu, ripoti hiyo imesema.

KWA NINI WIZARA YA KATIBA NA SHERIA IMENDA KUKUSANYA MAONI MIKOA HII?:

Mikoa iliowekewa rangi ya njano ndio mikoa kunako kusanywa maoni juu ya umri upi ni sahihi wa kuoa/kuolewa,na iliowekewa rangi nyekundu ndio yenye namba kubwa juu yandoa za utotoni. Shinyanga (asilimia 59),Tabora (asilimia 58),Mara(asilimia 55),Dodoma (asilimia 51) ,Lindi (asilimia 48),Mbeya (asilimia 45),Morogoro (asilimia 42),Rukwa(asilimia 40),Ruvuma (asilimia 39),Mwanza (asilimia 37),Kagera (asilimia 36),Mtwara (asilimia 35), Manyara (asilimia34), Pwani (asilimia 33),Tanga (asilimia 29), Arusha (asilimia 27),Kilimanjaro (asilimia 27),Kigoma (asilimia 26), Dar es Salaam (asilimia 19),na Iringa (asilimia 8).

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI INALETA SULUHU KWA WATOTO WAKIKE:

Katibu na muwakilishi wa baraza la watoto la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutokea Zanzibar, Abubakar  Koke anasema siku hii nimuhimu sana kwa taifa la Tanzania, hii ndio siku maalumu ya kupaza sauti na kuidai haki ya mtoto wakike ambae ndio mama wakesho, “Ndoa za utotoni zina madhara kiafya na kiuchumi serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ikusanye maoni zaidi kutoka kwa watoto wenyewe nasio kama ilivyo sasa na pia ifike hadi kwenye Mikoa ilio na idadi kubwa ya matukio ya Ndoa za utotoni”.

Nancy Kasembo anasema sisi watoto kupitia baraza la watoto la Jmuhuri ya Muungano wa Tanzania tunamatumaini kwamba kupitia siku ya wanawake duniani, viongozi wa majukwa yan wanawake,mashirika ya kutetea haki za watoto wakike, Serikali na wadau mbali mbali watapaza sauti juu ya kuhakikisha kwamba vifungu vya sharia ya ndoa vinavyo ruhusu mtoto wakike kuolewa chini ya umri wa miaka 18, vinaondolewa.

Tunatamani kuona Serikali ikitenda haki ya kufanyia maboresho ya vifungu vya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971, na itekeleze maamuzi ya mahaka kama ambavyo iliatoa hukumu dhidi ya kesi ya Rebeca Gyumi , Dr. Rose Reuben.

Kwa sababu kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Ubunifu na teknolojia ya usawa wa kijinsia” Taasisi ya Msichana Initiative tunaihamasisha jamii kutumia majukwaa ya mtandaoni ya kijamii kupaza sauti za watoto wakike, kama ambavyo sisi tunatumia mitandao yetu ya kijamii njiamojawapo ya kuzungumza na watoa maamuzi juu ya maboresho ya Sheria ya Ndoa.

Na, John Kabambala.

Post a Comment

0 Comments