VISA JUU YA ADHABU YA VIBOKO KWA WANAFUNZI SHULENI.
Na, John Kabambala-Morogoro. Mwezi September hautasahaulika kamwe kwenye familia ya Eradius, uchungu, simanzi, vilio, masikitiko na huzuni vilitawala katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera vikitokea katika Shule ya Msingi Kibeta, halikuwahi kutokea kabala tukio kama hili na hapakuwa na mwenye uzoefu na kifo kitokanacho na adhabu ya viboko Shuleni, sio tu kwenye familia hiyo! Ila hata kwa jamii na walio kuwa wanafunzi wenzake.
Kwa muda mrefu kumekuwa na matukio mbali mbali ya athari ya viboko kwa wanafunzi mashuleni kama vile kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu hadi vifo, miongoni kati ya matukio yalio sikitisha zaidi ni lile la kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius wa Shule ya Msingi Kibeta, Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, tukio hili lililotokea Mwezi September Mwaka 2018, kifo kilichotokana na adhabu ya viboko aliyopata kutoka kwa mwalimu tena akiwa shuleni.
Vivyo hivyo tukio jingine linalo husishwa na adhabu ya viboko ni la Mwanaidi Ally, mwanafunzi wakike aliekuwa akisoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Saba saba iliopo Mkoani Mtwara, Mwanafunzi huyo alikuwa na umri wa miaka kumi nasita (16), kifo cha mwanafunzi huyo kilitokea mwezi Desemba Mwaka 2022, ambapo uhai na ndoto zake zikazima ghafla kama mwanga wa umeme unavyo katika ghafla bila taarifa, hayo ni baadhi ya matukio ya vifo kwa wanafunzi yalio husisha adhabu ya viboko.
Mwongozo wa kutoa adhabu mashuleni chini ya kifungu cha 61 (1) (v) cha Sheria ya Elimu sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002 ambao unampa mamlaka Waziri wa Elimu kutunga kanuni za Masuala mbalimbali zitakazokidhi utekelezaji wa masuala ya Sheria hiyo.
Miongoni mwa kanuni zilizotungwa ni pamoja na The Education (Corporal Punishment) Regulation G. N. 294 ya mwaka 2002. Kanuni hizi zinatoa mwongozo, ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa kiwango gani.
“Kanuni ya 3 (1) inasema adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhamu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya Viboko itatolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko vinne (4) kwa tukio lolote.”
Sheria
imempa mwalimu mkuu wa shule husika mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko au
kukasimisha mamlaka yake kwa umakini mkubwa kwa mwalimu yeyote kutoa
adhabu hiyo, Mwalimu anayechaguliwa kutoa adhabu atakua na mamlaka ya kutoa
adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika.
Kanuni ya (5) inataka kila adhabu ya Viboko inayotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya kutolewa kwa adhabu hiyo sharti iwekwe kwenye kitabu yaani (Kumbu kumbu), ikitaja jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na Mkuu wa shule.
LENGO LA STORI HII NI NINI?
Ni, kuikumbusha Serikali kupitia Wizara ya Elimu
kusimamia ipasavyo mwongozo wa Adhabu Shuleni, kupitia kanuni ya 3 (1) na
Kanuni ndogo ya (2) ya adhabu, kwani ukweli
usiofichika ni kwamba, mwongozo wa adhabu hii tajwa hapo juu hutekelezwa
kinyume cha kanuni zilizowekwa aidha kwa kutokujua au kwa kujua ila kwa
kupuuzia.
KWA NINI ADHABU YA VIBOKO SHULENI IENDELEE?
Kwa utamaduni ulio jengeka nchini Tanzania kataka
malezi ya mtoto nilazima viboko vipewe kipaumbele, suala hili hufanyika kwenye
jamii mbalimbali kwa lengo la kumbadilisha mtu mwenye tabia zisizo faa Shule, kwenye
familia, jamii, baadhi ya Walimu
wanaunga mkono kuwa adhabu ya viboko iendelee kutolewa Shuleni kwa sababu zipi?
Mwalimu Paschal Martine kutoka Shule
ya Sekondari Kisemwa iliopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoa wa
Morogoro aliniambia…Sauti…
ADHABU YA VIBOKO SHULENI
SIO TIBA KWA WENYE TABIA MBAYA:
Rosemary
Budala Mwalimu wa Shule ya Msingi Mvuha iliopo katiaka
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, yeye anakataa juu ya kuendeleza
adhabu ya viboko kwa wanafunzi Shuleni kama tiba ya wanafunzi wenye tabia mbaya,
sikiliza hapa mahojiano yake …Sauti…
HAKI ELIMU INAMTAZAMO UPI JUU YA ADHABU YA VIBOKO SHULENI?
Taasisi ya Haki Elimu nimoja kati ya wadau wakubwa kwenye sekta ya Elimu nchini, na tutakubarina kwamba wameweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta hiyo, kupitia miradi na kampeni zake juu ya maboresho ya sera na miongozo ya Elimu Msingi na Sekondari nchini, ufuatiliaji wa Taasisi katika Sekta ya Elimu imekuwa ikizichungulia na kuzichambua nyaraka kwa yasio tekelezwa wakati yameelezwa ndani yake.
Kupitia mazungumzo kati yangu na Mshauri Mwelekezi
kutoka Taasisi ya Haki Elimu, Dkt.Wilberforce
Meena juu ya adhabu zinazotolewa kwa Wanafunzi Shuleni, ameniambia kwamba,
“ Sio lazima mwanafunzi achapwe viboko ili ajutie kosa lake, ziko njia nyingi
muhimu Mwalimu anaweza kuzitumia ili mwa nafunzi ajutie kosa lake kupitia
adhabu hiyo atakayo pewa kuifanya.
Mfano,
Shule nyingi nchini zinamaeneo ya wazi tena hadi mashamba kwa baadhi ya Shule,
mwanafunzi apewe adhabu hata ya kuhudumia bustani ya miti,maua,kuku kwa muda
furani akiwa yeye peke yake, au apewe mazoezi mengi kuliko kawaida, nasio
kuchapwa viboko kwa kiango kilicho pitiliza wakati mwingine hata bila ruhusa ya
Mkuu wa Shule, kama ambavyo Mwongozo wa kutoa adhabu mashuleni chini ya kifungu cha 61 (1) (v) cha
Sheria ya Elimu sura ya 353 marejeo
ya mwaka 2002 inavyo sema”.
MTANDAO WA ELIMU TANZANIA UNASEMA (TENMET):
Juhudi zaidi ziongezwe katika kuhamasisha utetezi wa vitendo vyote vya kikatili vinavyofanywa kwa mtoto na kuviweka hadharani ili sheria ipate kuchukua mkondo wake, Serikali na mashirika mbalimbali yatoe elimu kwa walimu na wazazi kuhusu kanuni ya viboko mashuleni na utoaji wa adhabu mbadala kwa watoto.
Hata hivyo mwongozo wa utoaji wa adhabu ya viboko shuleni usambazwe shule zote na kila mwalimu apate nakala, ili Walimu waendelee kukumbuka mara kwa mara kuwa wana wajibu wa kumlinda mwanafunzi anapokuwa shuleni na nje ya shule, kwani Mtoto ana haki ya kulindwa, kuendelezwa, kuishi, kushirikishwa na kutobaguliwa, tunatoa wito kwa wadau wote wa watoto tushirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha mtoto anapata haki zake na anafahamu wajibu wake.
Baada ya tukio la kifo
cha
Sperius
Eradius aliekuwa mwanafunzi wa Shule
ya Msingi Kibeta iliopo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera,mnamo mwezi Machi,
Mwaka 2019, Mahakama Kuu ya Kanda ya
Bukoba ilimuhukumu kunyongwa hadi kufa Mwalimu Respicius Patrick baada ya kupatikana na hatia ya kumuua alie kuwa mwanafunzi
wa Shule ya Msingi Kibeta na kumuachia huru mwalimu Herieth Gerald baada ya
kutopatikana na hatia.
NJIA IPI ITUMIKE KULETA SULUHU YA CHANGAMOTO HII:
Mtandao
wa Elimu Tanzania (TENMET) umechapisha kwenye tovuti yake mambo yanayo paswa kuzingatiwa kuhusu utoaji
wa adhabu shuleni, mojawapo ni Vyombo vya habari vizidi kujikita zaidi kwenye
habari za uchunguzi na kuibua vitendo vyote vya ukatili na kuhabarisha umma juu
ya namna bora za kumlinda mtoto, na kila mwananchi atambue kwanza ulinzi wa
mtoto ni jukumu la kila mmoja bila kuangalia wadhifa, jinsia, kabila, dini au
mahali, sambamba na mafunzo kwa waalimu juu ya malezi ya watoto na utoaji wa adhabu
mbadala.
Haki Elimu kupitia kwa Mshauri Mwelekezi Dkt. Meena anasema viboko sio tiba ya mwanafunzi mwenye tabia mbaya, bali viboko vinaweza kumjengea usungu mtoto na chuki kwa mwalimu husika, matokeo yake hataweza kuwa naumakini darasani mwisho wake nikushindwa kufaru masomo, hasara kwa mafamilia na taifa kwa sababu taifa linaendelea kuzalisha watu wasio kuwa na utambuzi na maarifa juu ya elimu.
Mwalimu Rosemary Budala kutoka Shule ya Msingi Mvuha amesema, ni vyema kurejea kwenye kanuni zinazowaongoza walimu kwenye utendaji kazi wao wa kila siku na kuhakikisha walimu na wazazi wanauwelewa vya kutosha na kutekeleza kanuni ya utoaji adhabu ya viboko mashuleni.
0 Comments