Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

JUMA LA ELIMU 2023: TENMET INAHAMASISHA UCHANGIAJI WA UBORESHAJI ELIMU

 

Maadhimisho ya Juma la Elimu nchini Mwaka 2023, yamelenga kuongeza hamasa kwa umma, wadau wa Elimu na Serikali kuchangia katika uboreshaji wa Elimu nchini ikiwemo miundombinu ya Elimu na kuzingatia makundi maalumu kupata Elimu.

Hayo yalielezwa na Mratibu wa kitaifa wa maadhimizo ya Juma la Elimu Tanzania, Mkurugenzi wa Mtandao wa Elimu Tanzania –TEN/MET, Ochola Wayoga katika uzinduzi wa Juma la Elimu uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mvuha katika Kata ya Mvuha Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro vijijini.

“Maadhimisho haya yanatarajia kuongeza uelewa kwa umma, juu ya umuhimu wa uchangiaji uboreshaji wa Elimu lakini namba mbili kuhamasisha Serikali kuzingatia makundi yaliyokosa fursa kama watoto wenye ulemavu, watoto wa kike, kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na lengo la Tatu ni kuhamasisha na kukumbusha Jamii, Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na wadau mbali mbali wa Elimu kuhumu umuhimu wa uchangiaji wa Elimu” alisema Ochola Wayoga...https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1682151231--less-file-OCHOLA-WAYOG.mp3 

Katika Juma la Elimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro timu ya TenMet kwa kushirikiana na Serikali ya Wilaya na wadau mbalimbali wa Elimu ili kutambua changamoto za walimu na wanafunzi, walitembelea Shule walizopangiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, wakati huo huo wanamtandao wa TenMet walishiriki katika shughuli nyingine zitakazobainika kulingana na uhitaji, pia walifanya Vikao na kamati za Shule, walimu, wanafunzi, wazazi na wadau mbalimbali kwa kuzingatia mada kuu yenye kaulimbiu isemayo, Tuboreshe uwekezaji wa rasilimali za ndani kwenye Elimu kwa maendeleo endelevu.

Huu ni Mwaka wa 17 kufanyika maadhimisho ya Juma la Elimu nchini Tanzania.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Juma la Elimu, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebecca Nsemwa aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alizungumzia eneo aina ya rasilimali inayotakiwa kuwekezwa katika Elimu na jinsi Taifa linavyoweza kuendelea.

Nchi yeyote ili iendelee inahitaji kuwekeza kwenye Elimu bora, Elimu hiyo ni lazima itolewe kwa usawa wa kijinsia na jumuishi na kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wanafunzi, ili tufanikiwe ni lazima wadau wote wawajibike katika nafasi zao na pia ili tufikie lengo la kuwa moja kat yka Nchi za kipato cha kati hakuna budi Taifa Kuwekeza katika Elimu kwa watu wake na sehemu muhimu ya kuanzia kuwekeza katika rasilimali watu ni Elimu ya awali na Msingi kwa watu wote bila kuwaacha nyuma watoto wa kike” alisema Rebecca Nsemwa....https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1682151367--less-file-REBECCA-NSEMW.mp3 

Kwa upande wake Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Mvuha, Elia Simon anayesoma Kidato cha pili akihojiwa na Tanzania Kids Time alisema maadhimisho ya Juma la Elimu kwao yanafaida kubwa kielimu na kuendeleza vipaji.

Elia Simon alisema “Maadhimisho haya yana sapoti katika maisha ya Mwanafunzi kukuza vipaji, kwa mfano kwenye kuigiza, kujiamini na kujieleza mbele ya watu kama walivyofanya walioongea kingereza, unajua mwanafunzi anavyojifunza vile unajua kabisa huyu anajua hiki na hiki hakiwezi kwa hivyo inasaidia kuwaelewa vizuri wanafunzi”... https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1682151500--less-file-MWANAFUNZI-MVUH.mp3 

Katika maadhimisho hayo ya Juma la Elimu, pia lilizinduliwa Darasa la awali katika Shule ya Msingi Mvuha, ambalo ni Darasa linaloongea lenye vifaa na zana mbali mbali za kusoma na kujifunzia kwa wanafunzi.

Akizungumzia Darasa hilo Mwalimu wa Shule hiyo, Rosemary Bundala alisema “yani atakachojifunza Mwanafunzi kwanza ataipenda Shule, kingine kiwango chake cha Elimu kitakua kwa mfano hili Darasa la awali linaloongea ambalo limezinduliwa leo, lina zana nyingi za Mwanafunzi kujifunzia litaongeza ari ya watoto kupenda Shule, watajifunza kwa kutumia Picha, maneo na zana zote zilizomo kwake inakua rahisi kuelewa”.

Nchini Tanzania Juma la Elimu kitaifa limezinduliwa tarehe 17/4/2023 na linatarajia kufikia kilele tarehe 21/4/2023, katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro vijijini.


                     

                         KWA NINI MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU     

 Maadhimisho ya Juma la Elimu (Global Action Week for Education-GAWE) ni tukio la alama kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayojishughulisha na Elimu duniani kote kama wito wa haraka na wenye nguvu kwa Mataifa, viongozi wa ulimwengu na jumuiya ya kimataifa kulinda Elimu katika Dharura na huadhimishwa kila ifikapo Juma la mwisho la mwezi wa Nne hadi wa Tano kila mwaka tangu mwaka 2000.

TEN/MET INAVYOHUSIKA KATIKA JUMA LA ELIMU.

TEN/MET ni mtandao wa kitaifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na Elimu nchini Tanzania, hadi sasa TenMet ina wanachama wapatao 184 nchi nzima.  TEN/MET inatazamia mfumo wa kitaifa wa Elimu ambao kila mtoto wa Kitanzania ana nafasi ya kushiriki katika elimu bora, dira hiyo imetajirika kupitia dhamira yake ya kuratibu na kuimarisha asasi za kiraia nchini Tanzania kupitia mitandao, kujenga uwezo, utafiti na utetezi.

Kwa miaka 17 sasa TEN/MET kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine wa Elimu nchini wamekuwa wakishiriki kutimiza wito wa kuadhimisha Juma la Elimu (Global Action Week for Education-GAWE) nchini Tanzania.

Soma zaidi kuhusu TenMet: https://tenmet.or.tz/about-us/

 

 Post a Comment

0 Comments