Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TMDA INAVYO SHUGHULIKIA AFYA ZA WATOTO:

 

UTANGULIZI:

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

 UMUHIMU WA AFYA YA WATOTO:

Taifa linapaswa kulindwa na miongoni mwa vitumuhimu ni matumizi ya madawa na vifaa tiba na vitendanishi vinavyo tumika kwa watoto, watoto watakapo pewa  au kutumia bidhaa hii ya dawa pasipo kuthibitishwa na mamlaka husika matokeo yake kizazi hicho kunahatari ya kuteketea, hivyo basi ndiomaana, mwaka 2018, TMDA ilifanya ukaguzi wa viwanda vya kusindika vyakula vya nyongeza na maziwa ya watoto wachanga vilivyopo nje ya nchi ili kujilidhisha kabla ya kuruhusiwa kuingiza sokoni.  

MAJUKUMU  YA TMDA KATIKA KULINDA AFYA ZA WATOTO:

TMDA hupokea maombi ya usajili wa vifaa tiba nchini vikiwemo vinavyotumika kwa watoto kutoka kwa wadau mbalimbali walioko ndani na nje ya nchi, Baada ya kupokea maombi hufanya tathmini ya taarifa za ubora, usalama na ufanisi wa Vifaa tiba vilivyowasilishwa na pale inaporidhika na tathmini husika ya vifaa hivyo husajiliwa.

 Upimaji wa sampuli katika maabara.

Maabara ya TMDA hupima sampuli za vifaa tiba kwa lengo la kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wake kabla na baada ya kuruhusiwa kuingia katika soko, Pale inapobainika kwamba kifaa tiba hakikidhi viwango vya usalama, ubora na ufanisi hakipewi usajili na kama kipo sokoni matumizi yake husitishwa na kuondolewa.

 Kudhibiti uingizaji na usafirishaji nje ya nchi.

TMDA hudhibiti uingizaji nchini wa vifaa tiba na Dawa kwa kuwataka waagizaji kuomba kibali cha kuingiza vifaa tiba nchini na kufanya ukaguzi kwenye vituo vya forodha kuhakiki kama waagizaji wamezingatia taratibu za uingizaji vifaa tiba.

 Ukaguzi katika soko na vituo vya forodha.

TMDA hufanya ukaguzi katika vituo vya forodha, maeneo ya biashara ikiwa ni pamoja na maduka, maghala na vituo vya kutolea huduma za afya kwa nia ya kuhakiki usalama, ubora na ufanisi wa vifaa tiba na Dawa, Pale inapobainika kwamba kuna ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu, Mamlaka huchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa onyo, kusitisha kwa muda matumizi ya kifaa tiba hadi marekebisho yafanyike au kufuta usajili wa kifaa tiba kufikisha mtuhumiwa mahakamani pale inapolazimu.

 FAMASI ZINAFANYA NINI KULINDA AFYA ZA WATOTO.

Maeneo ambayo huleta changamoto kubwa kwa jamii ni maduka  ya dawa muhimu, baadhi yao huuza dawa na vifaa tiba vilivyo isha muda wake kwa baadhi yao, kwa nini hutokea hali hii? Je, ni njiagani hutumika kuhifadhi dawa na vifaa tiba kwenye maduka ya dawa? Nimetembelea moja kati ya maduka ya kuuza dawa muhimu Marhaba farmasi iliopo Mkoani Morogoro, na nimefanya mahojiano na Kelvin Magonda huyu ni mfamasia sikiliza mahojiano hayo….https://appfasta.com/tkt/cms/ 

 Mafanikio ya TMDA katika Kulinda Afya za Watoto

CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TMDA KULINDA AFYA ZA WATOTO

Mkuu wa Mawasiliano kutoka TMDA Bi, Gaudensia Simwanza amebainisha  changamoto mojawapo kwa jamii ni ununuzi holela na kutumia dawa bila kufanyiwa uchunguzi au kuelekezwa na daktari, kutumia vijiuasumu kutibu magonjwa yanayotokana na virusi (viral infections) kutumia dozi isiyosahihi au kushindwa kumaliza dozi, kutumia dawa zinazoingiliana kiutendaji kwa pamoja, kwa mfano tetracycline na Magnesium kutumia dawa na pombe. Jambo linguine kubwa ununuzi wa dawa au kifaa tiba kilicho maliza muda wake wa matumizi, na kushindwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika kama vile TMDA.

ELIMU GANI HUTOLEWA NA TMDA KWA JAMII?

Elimu inayo tolewa na TMDA ni kuhusu matumizi sahihi ya bidhaa kupitia shule za sekondari na msingi, makundi mbalimbali ya wananchi na vikundi vya wajasiriamali, Lengo la elimu hiyo ni kuimarisha udhibiti wa sekta hiyo ili kuhakilisha kuwa huduma za usambazaji na uuzaji wa dawa, vifaa tiba  na vitendanishi inatolewa bila kuathiri usalama wa chakula na kusababisha madhara ya kiafya kwa walaji.

 Elimu kwa umma husaidia kuongeza uelewa kwawatumiaji wa bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA na wananchi kwa ujumla katika matumizi sahihi ya bidhaa na kuongeza utii wa Sheria bila shuruti.

 DHIMA ya TMDA  ni Kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

 DIRA ya TMDA ni  Kuwa Mamlaka inayoongoza katika kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa dawa, Vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa nyingine za afya kwa wote.

 FALSAFA ya TMDA ni Kutoa huduma bora za udhibiti katika kulinda afya ya jamii na mazingira kwa kutumia wafanyakazi wenye ujuzi na ari ya kazi.

 USHAURI

Ili kuepuka au kupunguza kutokea usugu wa bakteria unashauriwa kutumia dawa kwa usahihi, Usinunue vijiuasumu kiholela, Usinunue vijiuasumu bila cheti cha Daktari, Hakikisha unafahamu matumizi sahihi ya dawa ulizopewa kabla ya kurudi nyumbani toka kituo cha afya au duka la dawa na  Tumia dozi sahihi kwa kipindi.

 TMDA inawataka watengenezaji, waagizaji na wauzaji wa vifaa tiba kufuata taratibu na kujihakikishia ubora, usalama na ufanisi wa vifaa tiba wanavyonuia kuviuza kwenye soko la Tanzania kabla ya kukaguliwa na kuhakikiwa na Mamlaka, hii itarahisisha udhibiti wa vifaa tiba nchini na kuongeza imani ya watumiaji na wananchi kwa bidhaa zinazouzwa.

 Vile vile, jamii inaombwa kutoa taarifa TMDA au kituo chochote cha afya inapobaini ukiukwaji wa taratibu za utengenezaji, usambazaji, uuzaji na matumizi yasiyo sahihi ya vifaa tiba ili mwisho wa yote lengo la Serikali la kulinda afya ya wananchi wakiwemo watoto liwezekutimia.

Na, John Kabambala-Morogoro.

Post a Comment

0 Comments