Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

CHANJO YA HPV NIMUHIMU KWA WASICHANA TANZANIA

 

Na, John Kabambala-Morogoro. Afrika na kusini mwa Jangwa la Sahara, saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inayoongoza kwa vifo vinavyotokana na saratani kwa wanawake, Afrika Mashariki ina idadi kubwa ya matukio na vifo vinavyotokana na saratani ya shingo ya kizazi na ndiyo saratani inayowapata wanawake wengi zaidi Afrika mashariki, Nchini Tanzania, ndicho kisababishi kikuu cha saratani kwa wanawake wenye umri wa miaka 15-44, na matukio ya kila mwaka na vifo vya takriban 9,772 na 6,695 mtawalia. Taarifa hiyo nikwamujibu wa ripoti ya- Barriers to Human Papillomavirus (HPV) Vaccination of Adolescent Schoolgirls in Morogoro Municipality, ilioandaliwa na  The Muhimbili University of Health and Allied Sciences October, 2021.

 SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI  NI NINI?

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko katika shingo ya kizazi, mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile, inasemekana kuwa ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea. Ripoti ya mwaka 2012 ya shirika la afya duniani 'WHO' inasema kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya Shingo ya kizazi barani Afrika, 50,000 walifariki dunia. 

NINI KINACHOSABISHA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

Taasisi ya Saratani Ocean Road inaonesha, Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99% ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma, baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Miongoni mwake ni Kufanya ngono zembe, Kuwa na wapenzi wengi, Kukoma siku katika umri mkubwa, Utumiaji mafuta mengi katika chakula, Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara, Unene kupita kiasi, Uvutaji sigara, Utumiaji wa pombe kupita kiasi na Historia ya saratani ya matiti katika familia.

Visababishi vingine vya hatari ni ndoa za utotoni, magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na maambukizi ya VVU, upungufu wa vitamini na maambukizi ya HPV, chanjo hii inapotolewa kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 9 na 14, huwalinda dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi.

WATU GANI WAPO KWENYE HATARI ZAIDI?

Wasichana wanao anza ngono katika umri mdogo na wenye umri mkubwa, pamoja na wanaotumia vidonge vya kupanga uzazi kwa mda mrefu, Kuzorota kwa kinga ya mwili husabisha kuongzeka kwa athari ya virusi wa HPV wanaoletekeza kansa ya shingo ya kizazi,Wanaopata ujauzito katika umri mdogo chini ya miaka 17 wapo kwenye hatari Zaidi ya kupata saratani hii.

CHANJO HII ILIZINDULIWA LINI NCHINI TANZANIA:

Kwa mujibu wa WHO Tanzania, kwa mara ya kwanza mwezi Aprili mwaka 2018, Tanzania iliweka historia yakuwa miongoni mwa nchi zinazo tekeleza huduma ya utoaji na usambazaji wa chanjo ya Human Papilloma Virus (HPV) dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana, saratani hii ni yapili kwa wanawake duniani kote, na katika ukanda wa Afrika Mashariki ndio unaoongoza kwa kubeba mizigo ya saratani ya shingo ya kizazi na Tanzania ilikuwa ni kati ya nchi tano zenye viwango vya juu zaidi barani Afrika.

Uzinduzi wa kitaifa wa chanjo ya HPV ulifanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati huo ambae kwa sasa ni Rais wa Taifa hilo, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Wawakilishi wa Nchi wa WHO na UNICEF, pamoja na wageni wengine kutoka mashirika mbali mbali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipokuwa mgeni rasmi alithibitisha dhamira ya serikali ya kuhakikisha lengo la chanjo ya wasichana 616,734 linafikiwa na kuwataka wazazi na walezi kutokosa 'fursa nzuri' ya kupata chanjo hiyo watoto wao kupewa chanjo.

KABLA YA KUZINDULIWA CHANJO YA HPV:

Kabla ya kuzinduliwa kwa chanjo ya HPV, utetezi wa jamii na uhamasishaji ulifanyika katika ngazi zote, Elimu ya HPV ilitolewa kupitia Televisheni na Redio katika ngazi ya Taifa wakati katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kama halmashauri zingine, walimu wa afya kutoka shule za Sekondari na Msingi walipatiwa mafunzo ya chanjo ya HPV ambao nao wangeweza kuhamisha maarifa kwa wanafunzi na wafanyakazi wenzao na kushirikiana kupanga ratiba za chanjo kwa wanafunzi wanaostahiki.

Tangu kuzinduliwa kwa chanjo ya HPV mnamo 2018, katika Manispaa ya Morogoro, chanjo ya dozi ya kwanza na ya pili ya HPV ni 84% na 48% ilifikiwa  Desemba 2019, Utoaji huu mdogo hasa wa kipimo cha pili cha chanjo ya HPV una athari kwa afya ya uzazi ya wanawake vijana ya siku za usoni, na kwa hivyo inahitaji uchambuzi wa kina wa vikwazo vya utumiaji wa chanjo hii mpya iliyoletwa.

 RIPOTI MPYA YA UNICEF KUHUSU CHANJO HII YA HPV:

Ripoti hiyo mpya iliotolewa mwezi April, inaonesha watoto milioni 67 hawakuchanjwa kati ya mwaka 2019 na 202, Idadi ya waliochanjwa ilipungua katika mataifa 112, ikiwemo Tanzania  na Watoto waliozaliwa kabla au baada ya janga la Corona, sasa wameingia kwenye kipindi ambacho wamevuka awamu ya umri wa kuchanjwa , hali inayousisitizia umuhimu wa kuchukua hatua za ziada kuwahudumia waliikosa  na kuzuwia maambukizi ya magonjwa hatari.

Takwimu za UNICEF zinaashiria kuwa kati ya watoto milioni 67 waliokosa chanjo zilizoratibiwa kati ya 2019 na 2021, milioni 48 hawakupokea chanjo yoyote, Watoto walio katika hali mbaya ni wale wa mataifa masikini zaidi ambayo huenda pia yanazongwa na vita namaendeleo duni.

CHANJO HII INASAIDIA NINI?

UNICEF inasema: Chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi (HPV) inasaidia kulinda dhidi ya kansa kadhaa, haswa saratani ya shingo ya kizazi, ambayo inakadiriwa kuwa chanzo cha nne cha vifo vya saratani kati ya wanawake ulimwenguni kote, katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, chanjo ya HPV ilipungua kati ya 2019 na 2021 nchi hizo ikiwe Tanzania licha ya maendeleo yasiyopingika kwa miongo mingi, ya uzingatiaji wa utoaji chanjo, imeendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa utekelezaji wa jambo hilo.

Ripoti hiyo inasema, Utoaji wa chanjo umerudi nyuma, au umedumaa, katika maeneo mengi sana, Tunazidi kuwakosa watoto walio na chanjo za kuokoa maisha, haswa watoto waliotengwa kijamii na maskini zaidi, na hali imekuwa mbaya zaidi wakati wa janga hili, Kushindwa kwa mifumo ya afya kufikia kila mtoto na chanjo kunaonyesha uwekezaji mdogo wa nyumbani katika huduma ya afya ya msingi, rasilimali watu duni kwa afya, na mapungufu ya uongozi katika ngazi na maeneo mbalimbali ya serikali.

Kupungua kwa chanjo katika kipindi chote cha janga hili kunapaswa kuchukua hatua sasa dhidi ya utoaji chanjo na lazima iwe kipaumbele katika miaka ijayo, Ni lazima tuchukue hatua za pamoja ili kuwapata watoto waliokosa chanjo wakati wa janga hili, kujenga upya mifumo na kukabiliana na mapungufu makubwa katika mifumo ya afya, kushindwa kuchukua hatua kutaharibu maisha ya watoto wa leo na vijana na watu wazima wa kesho, na kutarudisha nyuma maendeleo zaidi ya SDGs.

DALILI ZA SARATANI HII NI ZIPI?

Kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni, Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa, Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area), Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana, Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia, Mkojo wenye matone ya damu. 

KIPI UFANYE KUZUIA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote pia Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi, Kuwa na mpenzi mmoja, Usichangie mapenzi na watu wengi, Kula chakula chenye afya hasa vyakula asilia, Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani, Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV, Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo, Epuka matumizi ya Dawa za uzazi wa mpango zenye madhara, Jishughulishe kuupa mwili mazoezi, Punguza unywaji wa pombe na Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani. 

Saratani ya shingo ya kizazi inazuilika au kutibika kabisa endapo itagundulika ikiwa kwenye hatua za awali, hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya yako kwa kadiri utakavyoshauriwa na wataalam wa afya Wanawake wote walio na umri kuanzia miaka 30 na kuendelea wanatakiwa kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, Kumbuka: Wakati wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ni sasa usisubiri hadi uone dalili, fika kituo cha huduma za afya kwa ushauri/mwongozo Zaidi.

 

 

Post a Comment

0 Comments