Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MRADI WA BINTI SHUPAVU UNAVYOSAIDIA KUFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA KIKE

 

Picha ya pamoja baina ya wazazi wa Kata ya Ngerengere na watenda kazi wa Shirika la GLAMI

Na Hamad Rashid. 

Mradi wa ‘’Binti Shupavu’’ unaotekelezwa Mkoani Morogoro na Shirika lisilo la kiserikali la Gilrs Livelihood and Mentorship Initiative (GLAMI), kwa kuwapatia wanafunzi wa Kike Elimu ya Stadi za Maisha ikiwemo kujitambua, umekupokelewa vyema na wazazi na walezi baada ya kuonesha nia ya kumsadidia Binti kukabiliana na changamoto anazoweza kukumbana nazo wakati akiwa Shule.

Shirika la GLAMI linatekeleza Mradi wa Binti Shupavu ikiwa ni njia ya kufanikisha Lengo la Nne la maendeleo endelevu SDG’s linahohusu Elimu, ambapo Jumla ya wasichana 824 wameanza kunufaika na Mradi huo kutoka katika Shule za Sekondari Tisa zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, ambapo Mwezi huu wa Tano limekamilisha Programu ya kufanya vikao na wazazi katika Shule hizo ili kuwajengea uwezo wa malezi kwa watoto wao.

Msimamizi wa Mradi wa Binti Shupavu Mkoa wa Morogoro Einoth Justine alieleza hatua ya Mradi iliyofikiwa kwa sasa pamoja na kufafanua matarajio yao kwa wazazi wa wanafunzi wanufaika.

“Mradi wa Binti Shupavu ni Mradi ambao unajihusisha na mabinti ambao wako Kidato cha kwanza hadi Kidato cha Nne na ni mahususi kwa ajili ya kuhakikisha hawa mabinti wanapata mafunzo ya Stadi za Maisha pamoja na Elimu ya uongozi binafsi, ili kuwasaidia kujitambua, kuweza kubaki Shule na kuhitimu Elimu yao ya Kidato cha Nne na kuendelea mbele zaidi, lakini pia wanafundishwa namna ya kuwa wastahamilivu kuweza kuzikabili changamoto wanazokutana nazo, ambazo kwa namna moja au nyingine zingeweza kuwa kikwazo katika safari yao ya Elimu” Alisema Einoth Justine.

Einoth Justine akiwa anakabidhi zawadi kwa Mzazi Kassim Abdalah katika Shule ya Sekondari Kisemu

Einoth Justine pia aliongeza kwa kueleza matarajio yao kwa wazazi “Tangu Mwezi wa Tatu tumekua na mfururizo wa vikao na wazazi, lengo kuu likiwa ni kuwakumbusha majukumu yao, kusikia kutoka kwako wao wamekua wakifanya nini kumsaidia huyu Binti kuweza kufikia malengo yake lakini pia tutashirikiana nao kwa jinsi gani kama Shirika kuhakikisha tunamsaidia Binti kufikia malengo yake. Matarajio yetu ni kwamba hawa wazazi watakua chachu ya mabadiliko kwenye Jamii zao wakitimiza majukumu yao, kwa watoto wao hasa wa kike lakini pia kufuatilia safari yao ya Elimu na kuona kwa namna gani kwa pamoja tunaweza kuwasaidia hawa mabinti”

Akitoa mchango wake katika kikao cha wazazi na Shirika la GLAMI, katika Kata ya Ngerengere Mzazi Msafiri Lema, alionesha kuvutiwa na aina ya mafunzo waliyopewa na wawezeshaji wa kikao hicho, “kwa kweli mmekuja kutufungua kichwa, kutufungua masikio, tena naenda kuwaambia wale waliokua na udhuru wa kutofika kwenye kikao hiki, jamani tunatakiwa tufanya moja tufanye mbili katika malezi ya mabinti wetu ili tuwe na mabinti Shupavu lakini tuwe na Taifa jipya”

Mmoja wa mabinti wanufaika wa Mradi wa Binti Shupavu anayesoma Kidato cha Tano Shule ya Sekondari Matombo Patricia Lukumay alisema wakati akiwa mkoani Arusha Mradi wa Binti Shupavu umemsaidia kufikia hatua aliypo sasa.

Patricia Lukumay alisema “kupitia Binti Shupavu imenisaidia kujua jinsi ya kutatua changamoto na kukataa vishawishi kwa kusema Hapana kwa kile ambacho nakiona sio sawa kwangu, kingine imenisaidia jinsi ya kuwa na uwezo wa kuhimili changamoto zangu, kama kukata tamaa, kuacha Shule labda kuona Somo flani huliwezi, kuchapwa mwishowe unaona uache Shule hivyo kupitia Binti Shupavu imenisaidia kunipa njia vitu gani vya kufanya pale ninapokabiliwa na changamoto kama kufeli somo flani ikiwemo kuomba ushauri kwa wenzangu au kumuomba ushauri Mwalimu”

Mwanafunzi Patricia Lukumay akifurahia zawadi kutoka GLAMI aliyokabidhiwa na Diwani wa Kata ya Lundi Apia Mkami.

Afisa Elimu Kata ya Ngerengere katika Tarafa ya Ngerengere Lydia Ntapara alieleza matumaini yake kupitia Mradi wa Binti Shupavu.

"Aah mimi kama Afisa Elimu kata kupitia huu Mradi wa Binti Shupavu nitahakikisha nafuatilia kwa ukaribu zaidi, kwani kwangu katika kipengele cha Elimu inanisaidia sana baada ya kujua malengo ya Binti shupavu na jisni tutakavyoshirikia kwa pamoja kumjenga Binti, na pia nitafuatilia zaidi ili nijenge mabinti wengi kama nilivyo mimi na wengine kama kina Mama Samia” Alisema Lydia Ntapara.

Afisa Elimu Kata Lydia Ntapara Kata ya Ngerengere  kushoto na kulia kwake ni Afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Morogoro vijijini Zebedayo Mbamba

Zebedayo Mbamba ni Afisa ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini amekua akishiriki kutoa Elimu ya Haki za Mtoto na Ukatili wa kijinsia katika vikao vya wazazi wa wanafunzi wanufaika wa Mradi wa Binti Shupavu, akihojiwa na muwakilishi wetu alisema, “tumekutana na wazazi wengi ambao wanafunzi wao wanasoma Shule tofauti tofauti katika Halmashauri yetu ya Morogoro vijijini, hakika kwa Elimu tuliokua tunatoa kwa wazazi tumeona inafaida na matunda mengi sana kwasababu mwitikio wa wazazi ulikua mkubwa sana na ni Elimu ambao wazazi wengi wameonesha kuifurahia kwa sababu walikua hawaijui kwa mfano katika eneo langu nilikua nawafundisha juu ya haki za Mtoto ili watambue nini wanapaswa kuzitimiza, wengi walikua wakishangazwa na hivi vitu mfano hasa katika haki ya kumshirikisha Mtoto, kwamba wanapaswa kuwa marafiki wa Mtoto wengi walikua wakishangazwa. Wazazi wengi walifurahia na hiko kitu na walionesha kwamba kumbe walikua wameweka Daraja baina yao na wanafunzi”

             Zebedayo Mbamba akiwezesha wazazi Matombo Sekondari.

Mwalimu Mlezi katika Shule ya Sekondari Matombo Mwanamvua Bakari alisema, mafunzo wanayopewa wasichana Shuleni ni sehemu ya kuwasaidia wazazi katika wajibu wao wa malezi ambapo wanafunzi pia wameyapokea vyema. “

Mwanamvua Bakari alisema “Hawa mabinti wenyewe wako tayari kupokea mafunzo na wamependa sana kwa sababu sehemu kubwa ya haya mafunzo ni sehemu ambayo walezi na wazazi wao hawawezi kufanya na hawajawahi kuyapata kwakweli, kwa hivyo hawa wawezeshaji wa Mradi wa Binti Shupavu wao wamekuja kuchukua nafasi ya Mzazi na Mlezi kwenye kuwapa yale mafunzo ambayo mabinti walikua hawayapati majumbani mwao”

Orodha ya Shule za Sekondari zilizofikiwa na Mradi wa Binti Shupavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro vijijini ni pamoja na Ngerengere, Bwakila chini, Kisemu, Kiroka, Mkuyuni, Fatemi, Gwata na Matombo Sekondari.

Post a Comment

0 Comments