Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

RIPOTI YA ALIVE JINSI INAVYOTUMIKA KUIAMSHA JAMII KUWANOA VIJANA

 

Picha ya Meza kuu uzinduzi wa Ripoti ya ALIVE Ilala

Na, Hamad Rashid. 

Wadau wa masuala ya Elimu na malezi na makuzi ya vijana nchini wamepokea kwa mshtuko matokeo ya upimaji mahili za Stadi za maisha na maadili kwa vijana, baada ya Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation kubaini vijana waliohojiwa wengi wao, viwango vyao vya kujitambua, utatuzi wa matatizo, ushirikiano na Heshima viko chini katika pande zote za Bara na Visiwani.

Katika muktadha huo Ripoti hiyo ya Mradi wa ALIVE katika kipengele cha Utatuzi wa Matatizo Tanzania Bara, imebaini Karibu 6 katika 10 ya vijana hawawezi kutambua uwepo kwa tatizo kutoka kwa mtazamo mmoja na hivyo wanashindwa kutambua suluhisho linalowezekana kutatua tatizo hilo.

Aidha katika upande wa Tanzania Zanzibar kipengele cha “Kujitambua’’ Ripoti imebaini kijana mmoja kati ya watano ndiye mwenye ufahamu wa kujitambua (kutoka katika Kiwango cha 3 cha upimaji), ilhali wengi wanaweza kudhibiti athari zinazotokana na hisia, lakini hawajui njia nyingi ambapo wengine wanaweza kutambua.

MAPOKEO YA RIPOTI KATIKA MAKUNDI MBALIMBALI

Neema Mchau ni Mzazi kutoka Jijini Dar es salaam, alisema alipatwa na mshtuko baada ya kuona hali mbaya ya matokeo ya vijana wa umri wa miaka 13-17, kuwa na viwango vya chini katika suala la Stadi za Maisha na Maadili.

“Kimsingi kama Mzazi nimepokea kwa mshtuko, kwa sababu Ripoti ile imeonekana ina mapungufu mengi kwa watoto wetu, kama mzazi na mdau wa Elimu imenishtua sasa nimejiangalia nikasema, lakini hili ni tatizo lililopo kwenye Jamii yetu na sisi kama wazazi lazima tujitathmini kwamba tumekosea wapi, wale ni watoto bado wako chini yetu na tunahitaji kuwaongoza, niwakumbushe wazazi wenzangu tusiwalee watoto kama Ndege tukawaacha wakazubaa maana wazazi tumekua bize sana kutafuta maisha” Alisema Neema Mchau.

Naye Mwalimu kutoka Skuli ya Mikunguni iliyopo Unguja Asha Mussa Ally alizungumzia matokeo ya Ripoti ya ALIVE na kueleza mbinu zinazoweza kutumiwa na walimu kuwafundisha wanafunzi Stadi za Maisha na Maadili Shuleni. “Ripoti ya ALiVE haikua nzuri kwa sababu Stadi za Maisha kwa wanafunzi ambao tumewafanyia utafiti zilikua chini kabisa, na kuna vipengele vingi ambavyo vinasababisha hali hiyo kwa upande wa walimu, wazazi na Jamii, kwa hivyo sisi walimu tunachotakiwa ni kuboresha mbinu za ufundishaji darasani na tuweze kuwahusisha zaidi wanafunzi kuliko sisi walimu, mbinu ambazo zitafanya wanafunzi waweze kushirikiana kwa pamoja, kwa sababu kitu kinachoonekana kwa sasa wanafunzi wenyewe kwa wenyewe wanaogopana, kwa mfano ukimsimamisha mmoja kujibu swali mwingine anacheka, kwa sababu hawana uelewa kama kusoma ni kwa pamoja na hata mtu hajui wanatakiwa washirikane”

Katika upande mwingine, Mwanafunzi wa Kidato cha pili Muznati Salim Hamad kutoka katika Skuli ya Sekondari Mikunguni iliyopo Unguja alieleza namna Jamii na Sekta ya Elimu zinavyopaswa kuwajibika kuwafundishwa vijana Stadi za Maisha.“Kwa Stadi za maisha na maadili kushuka kwa wanafunzi au vijana katika mitaa kwa mtazamo wangu mimi, katika ulimwengu mzima hii inakua kutokana na Jamii inavyowaweka vijana wao, kama Jamii imekaa hivi na vijana na wale vijana wataenda hivyo hivyo, kama Jamii itakua haishughulikii Stadi za Maisha maana yake vijana watakua hawana Stadi za Maisha, kama vile kujithamini kwa hivyo, naishauri Jamii ya kwamba masuala haya yawe yanafundishwa sehemu zote za Jamii kwa wazazi na masheha na katika Skuli zetu” Alisema Muznati Salim Hamad.                                                               Mwanafunzi Muznati Salim Hamad.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guluka kwalala Kata ya Gongo la Mboto Augustino Simba alisema, Stadi za maisha ni muhimu vijana wakaanza kufundishwa shuleni kama ilivyo masomo mengine ili kukabiliana na suala la mmomonyoko wa maadili kwa vijana.

Augustino Simba alisema “Elimu kama hii ya Stadi za Maisha isilengwe kwa hawa wa mitaani, iende hadi kwenye Shule za Msingi na Sekondari, kwa sababu kule ndio kwenye jumuiko kubwa la vijana, na matukio mengi yanatokea katika maeneo yale hasa wakati wa mwanafunzi kutoa au kwenda Shule, mimi naomba kwenye Mtaala wa Elimu Somo kama hili liwepo Shuleni na kuwe na walimu maalumu wa kufundisha kama wanavyofundisha masomo mengine, naamini vijana wengi watabadilika kujitambua kwao”

Aidha, akizungumza katika Mahojiano wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya ALiVE Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, muwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dar es salaam Festo Mlimila alipokea vyema suala la Somo la Stadi za Maisha na Maadili kufundishwa katika Shule nchini.

“Nafikiri ni Mradi mzuri kujadili Stadi za Maisha hasa ukizingatia hali ya sasa iliyopo kutokana na mmomonyoka wa maadili kama mnavyosikia kuna masuala mazima ya ukatili wa kijinsia katika Jamii ambao wengine wanakua ni wanafunzi, kama utafiti ulivyofanyika kupima vijana wa umri wa miaka 13-17, Idara ya Elimu ya Msingi na Sekondari kwa ujumla, hili jambo tumelipokea vizuri kupitia Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation na itatusaidia kuwezesha watoto wetu kuwa na maadili mema na waweze kujifunza vyema wanapokua mashuleni” Alisema Festo Mlimila

KINACHOFUATA BAADA YA MATOKEO YA MRADI WA ALIVE

Mipango ya Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation (MZF) sasa ni kusonga mbele katika kuzalisha wataalamu watakaoweza kufundisha Stadi za Maisha kutoka Afrika, alisema Msimamizi wa Miradi kutoka MZF Khadija Shariff alipohojiwa na Tanzania Kids Time Ofisi kwake Mbweni Unguja.

Khadija Shariff alisema “Sasahivi Duniani kuna mwamko mkubwa kuhusu Stadi za Maisha na maadili, hizi ni mahili ambazo zinajulikana Duniani zinahitajika kwa ajili ya kuleta maendeleo makubwa, kwa hivyo wenzetu huko Ulaya na Mabara mengine wameshaanza kuwa na wataalamu wakutosha, jamba ambalo inabidi tuwalete wao hapa kuja kutusaidia sisi”

         Khadija Shariff-Msimamizi wa Miradi-MZF.

Khadija aliongeza kuwaLakini “Sisi kwa sasa tumejikita katika kujenga wataalamu safari hii, ili tuweze Kujitegemea wenyewe tuweze kuzalisha zile mbinu za upimaji ambazo zitakua zinaendana na mazingira yetu na tutafanya hivyo kupitia kitu kinaitwa, ALiVE Accademy itakua chuo ambacho kwa sasa kitaanza kutoa mafunzo yake kupitia njia ya Mtandao”

 

Post a Comment

0 Comments