Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MADHARA YA AHADI ZA WAZAZI ZISIZOTIMIZWA KWA WATOTO:

 

                                                       Picha:un news.

Na, John Kabambala:  Mara nyingi, katika maisha yetu, tunakabiliana na ahadi zilizotolewa na watu wengine. Ahadi hizi zina nguvu kubwa na zinaweza kujenga matumaini na furaha au kuvunja mioyo na kusababisha uchungu hii inakuwa kwa watu wazima na Watoto pia husisimka na kufurahi wanaposikia ahadi kutoka kwa wazazi wao, hata hivyo, wakati mzazi anaposhindwa kutimiza ahadi hiyo, hisia za mtoto zinaweza kujeruhiwa na kusababisha matokeo ambayo yanaweza kuathiri uhusiano wao na mzazi wao.

Hisia za kuvunjika moyo, huzuni, na kutokuelewana zinaweza kujitokeza, Mtoto anaweza kuanza kuhoji nia na upendo wa mzazi wake, wakati mwingine huenda akaanza kuhisi kukosa thamani na kujiona kama mtu asiye na umuhimu kwenye familia yao.

Uhusiano kati ya mzazi na mtoto unaweza kuathirika sana kwa sababu ya ahadi iliyovunjwa. Ikiwa mtoto hajashughulikiwa ipasavyo na mzazi wake, huenda akawa na hasira, kukasirika, au hata kujitenga. Hisia hizo zisizoeleweka na kutokuelewana zinaweza kujenga ukuta kati ya mzazi na mtoto, na hivyo kudhoofisha uhusiano wao wa karibu, Makala hii inaangazia athari za ahadi za Wazazi zisizotimizwa kwa watoto wao:

CHANZO CHA TATIZO:

Likizo ya wanafunzi ni kipindi muhimu ambacho watoto hupata muda wa kupumzika na kufurahia shughuli zisizo za kimasomo. Hata hivyo, baada ya likizo kumalizika, ni muhimu kwa wazazi kuzingatia mambo kadhaa ili kuwawezesha watoto wao kurejea katika utaratibu wa shule kwa ufanisi.

Kumalizika kwa likizo ya wanafunzi ni tukio ambalo hutangaza mwisho wa kipindi cha mapumziko na kurejea kwa shughuli za kawaida za masomo. Likizo hii mara nyingi inajumuisha muda wa miezi kadhaa, ambapo watoto hujihusisha na shughuli za burudani, mapumziko, na kujenga uhusiano na familia zao.

 Hata hivyo, baada ya likizo kumalizika, ni muhimu kwa wazazi kuchukua hatua muhimu ili kuwasaidia watoto wao kurejea katika mazingira ya shule na kujitayarisha kwa masomo yanayofuata, Ilikupata maelezo na ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu ahadi wanazo toa wazazi kwa watoto wao juu ya ununuzi wa vitu vipya nimemtafuta Mwanasaikolojia na Dkt. Wa mama na mtoto kutoka Morogoro, Dkt.Magdalena Kongera.

                                                 Picha ya Dkt.Magdalena Kongera.

SWALI: Wazazi wanapaswa Kufanya na Kuepuka nini wakati wa likizo ya wanafunzi inapo malizika?

Dkt.Magdalena Kongera : “Wakati likizo ya wanafunzi inapokaribia kumalizika na Shule zinapo funguliwa, wazazi wanapaswa kuwa wawazi kwa watoto wao kwanza kuwazoesha watoto wao kuwambia kama nitapata pesa nitakunulia begi jipya, nguo mpya na viatu vipya maneno haya huwakaa zaidi watoto. Mzazi hapaswi kumuonesha mtoto kila sikukuu anunue kitu kipya, maana yake siku ambayo hatapewa kitu kipya kuna mambo mawili moja mtoto anaweza kuathirika kisaikolojia au kujitoa uhai wake”.

SOMA KISA HIKI KUTOKA MOROGORO KWA MWALIMU MATHIAS KITONTO:

Mathias Kitonto: Ni Mwalimu alie hitimu miaka mitatu iliopita katika chuo kimoja  kilichopo Mkoani Morogoro, nimemtafuta ili kunielezea kisa cha mtoto Ally Juma, kisa hicho amewahi kukifahamu kutoka kwa mtoto huyo akiwa Shuleni, jinsi  ahadi ambayo wazazi walishindwa kuitimiza ilivyo athiri maisha ya mtoto huyo” .Mwalimu huyu ameomba kutotumia jina lake halisi pamoja na mtoto huyo kwani kisa hiki kinaihusu familia ya karibu nae.

SWALI: Mwalimu ! Unafahamu nini kuhusu kisa cha wazazi walioshindwa kumtimizia ahadi mtoto wao?

”Nakumbuka kulikuwa na familia moja  Wakati wa likizo, baba na mama walikuwa na mazungumzo mengi kuhusu jinsi  kumpa mtoto wao uzoefu wa kipekee, hususani kumpeleka maeneo ambayo hajawahi kuyafika nan i nadra sana kufika.

Kwa miezi kadhaa, familia hiyo ilipanga safari ya kuvutia kwenda Hifadhi ya Mikumi inayojulikana kwa mandhari yake ya ajabu na wanyama porini mbalimbali. Hata hivyo, siku ya kurudi shuleni ilipofika, wazazi hao wawili walikuwa na msongo wa mawazo. Jioni kabla ya kurudi kijijini, walifanya uamuzi ulioathiri maisha ya mtoto wao, Waliamua kufuta safari hiyo ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Baada ya kuwasili nyumbani, Ally Juma alitarajia kusikia habari njema za safari hiyo. Lakini badala yake, alikaribishwa na habari ya kuvunjiwa ahadi. Alibaki ameduwaa na kuchanganyikiwa. Wazazi wake walijaribu kumfariji, wakisema kwamba safari hiyo ingefanyika wakati mwingine, lakini uaminifu na imani ya Ally Juma kwa wazazi wake vilipungua”.

SWALI: Kuna madhara yeyote ali aliyapata kutokana na kushindwa kutimiziwa ahadi?

Mwl. Mathias Kitonto: “Ndiyo,  madhara ya ahadi za wazazi wakati wa likizo hayakuishia tu kwa hisia za mtoto, yalikuwa na athari kubwa katika maendeleo yake ya kihisia na kiakili, Kwanza, Mtoto huyo  alianza kupoteza imani katika ahadi zilizo kuwa zikitolewa na wazazi wake na alianza kuwa na uoga wa kujenga matarajio yoyote dhidi yao. Hii ilikuwa na athari mbaya kwa uhusiano wake na watu wengine, kwani alikuwa na wakati mgumu kuamini na kuwategemea wengine.

Pili, mtazamo wake kuelekea wazazi wake ulibadilika. Alianza kuhisi kukosa uaminifu na kujitenga nao. Alikuwa na hisia za kujisikia peke yake na kutokuwa na thamani. Hii ilikuwa hatari kwa uhusiano wao, kwani Ali alianza kupunguza mawasiliano yake na wazazi wake na kuweka ukuta kati yao.

Zaidi ya hayo, Ally alianza kukosa hamu na motisha ya kujaribu vitu vipya,  Ahadi ya safari ya kusisimua ilikuwa imechochea hamu yake ya kujifunza na kugundua mambo mapya lakini sasa, hamu hiyo ilizimwa alianza kukata tama, Madhara haya yalitanda kama wingu jeusi juu ya maisha ya mtoto huyo hapo awali alikuwa mvumilivu na mwenye furaha, lakini sasa amekuwa mtu mwenye wasiwasi na aliyejaa hofu, Uwezo wake wa kustawi katika shule umepungua, na urafiki wake na watoto wengine ulidhoofika”. Alisema Mathias Kitonto.

ATHARI ZA AHADI  ZA WAZAZI ZISIZO TIMIZWA KWA WATOTO:

Ikumbukwe kwamba mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu kijiji cha Ikengwa Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma mtoto wa darasa la nnealijinyonga kwa sababu ya wazazi wake kushindwa kumnunulia nguo za sikukuu ya EID, lakini pia katika Manispaa ya Morogoro mtoto mwenye umri wa miaka tisa (9) alijinyonga kwa sababu ya wazazi wake kushindwa kutimiza ahadi  kwa mtoto wao.

MAMBO YA KUEPUKA:  "Wazazi hawapaswi kuwaahidi watoto wao kila likizo au sikukuu kwamba wanunue zawadi au kuwapikia chakula tofauti nakile kilichozoeleka kupikwa nyumbani kilasiku,hata kama uwezekano huo upo wa kutimiza hayo yote wakati mwingine wazazi wanashauriwa wasifanye chochote kipya ilikuwazoesha watoto utofauti wa hali ya maisha  ya kila siku. 

Kwa kufanya hivyo watoto  watazoea kwamba hata sikuku nyumbani mama anaweza kupika chakula chochote na siolazima kwamba kipikwe chakula kipya, hata likizo ikiisha watoto wanweza kuendelea na yunifomu zilezile za tangu likizo ilioisha, sio kila likizo ununue kvipya vyote". Dkt.Magdalena Kongera, alisema.

Baada ya likizo ya wanafunzi kumalizika, ni jukumu letu kama wazazi kuzingatia mambo muhimu ili kuwasaidia watoto wetu kurejea katika utaratibu wa shule kwa ufanisi. Kwa kuweka ratiba thabiti, kusaidia kazi za shule, kukuza ustadi wa kusoma na kuandika, kushiriki katika shughuli za kimwili, na kujenga mawasiliano mazuri na watoto wetu, tunaweza kuwahakikishia mafanikio yao ya kitaaluma na ustawi wao kwa ujumla. Juhudi zetu kama wazazi zinaweza kuchangia sana katika kujenga msingi imara kwa watoto wetu na kuwawezesha kuwa viongozi wa baadaye wenye mafanikio.

Post a Comment

0 Comments