Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAHADHARI YA BARIDI KWA WATOTO KIPINDI CHA MWEZI JUNI-AGOST:

 

                                                                         Picha kutoka -TMA

Na, John Kabambala:Athari za kiafya kwa watoto wakati wa baridi kali nchini Tanzania ni suala linalohitaji umakini. Tatizo hilo linaweza kuwa na athari kubwa kwa afya na ustawi wa watoto. Njia bora ya kukabiliana na hali hiyo ni kuelewa tatizo, kuchunguza chanzo chake, na kutafuta suluhisho muhimu.

Historia ya Baridi nchini Tanzania inatuonesha kwamba,Tanzania  kama nchi nyingine za Afrika Mashariki, hukumbwa na msimu wa baridi kila mwaka. Msimu huu huanzia  mwezi Juni hadi Agosti, na katika maeneo ya juu ya milima ya nyanda zajuu kasikazini kama vile Kilimanjaro na Mbeya, nyanda za juu kusini hali ya baridi inaweza kuwa ya kuvutia. Baridi hii huletwa na hewa kutoka kaskazini mwa jangwa la Sahara na pia kwa sababu ya urefu wa maeneo haya ambayo yanapata joto kidogo kutokana na kuyakaribia mawingu.

Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya hewa iliotolewa mwishoni mwa mwezi Mei 2023 inaonesha kwamba, kusini mwa mkoa wa Morogoro unatarajiwa kuwa nahali ya joto lachini  nyuzi joto 7-16 “Hali ya joto la bahari katika ukanda wa tropiki ya kati ya bahari ya Pasifiki inatarajiwa kuwa ya juu ya wastani, hali inayoashiria uwepo wa El Niño katika msimu wa Kipupwe 2023, hivyo kutarajiwa kusababisha mchango mdogo katika mwenendo wa mvua nchini hususan maeneo ya pwani”. Alisema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a.

Kupitia taarifa hiyo ilieleza athari zinazoweza kujitokeza pamoja na kutoa ushauri kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku, nakushauri jamii kuchukua tahadhari za kiafya dhidi magonjwa yanayoweza kusababishwa na baridi, vumbi na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.

Kupitia taarifa hiyo ya TMA imenisukuma kuandaa makala hii ambayo inaangazia athari za kiafya kwa watoto wakati wa msimu huu wa baridi nchini Tanzania, Baridi ni msimu ambao unaweza kuwa na madhara ya kiafya kwa watoto wadogo nchini Tanzania. Hali ya hewa ya baridi kali inaweza kuathiri vibaya afya ya watoto na kuongeza hatari ya magonjwa mbalimbali. Katika makala hii, tutachunguza historia na athari za kiafya zinazowakabili watoto wakati wa msimu wa baridi nchini Tanzania.

                                                                        Picha kutoka -TMA

DKT. WA WATOTO ANASEMAJE KUHUSU MSIMU HUU WA BARIDI:

Monica Apolo ni Dkt. wa watoto kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili nilimuuliza tutarajie nini kwa kipindi hiki cha msimu huu wa baridi? ” Kwa kipindi hiki cha msimu wa baridi watoto hupatwa na changamoto za magonjwa mbalimbali iwapo wazazi/walezi hawatachukua hatua, watoto wanaweza kusumbulia na Pumu, Mafua makali, Ugonjwa wa Macho na Ugonjwa wa ngozi. Wasimamizi na walezi wa watoto wanapaswa kuhakikisha wanawavalisha ngua nzito, soksi,kofia na wakati wa usiku kuwafunika shuka nzito, ili kuwapatia joto la nyuzi joto 15-25, kama eneo la kusini mwa mkoa wa Morogoro ambako kunatarajiwa kua na nyuzi joto la chini 7-16 kwa mujibu wa taarifa ya TMA  watoto wahakikishiwe usalama wa joto kwa uangaliziDr. Monica Appollo alisema.

ATHARI ZA KIAFYA KWA WATOTO WAKATI WA BARIDI:

Athari za Kiafya kwa Watoto wakati wa Baridi Kali Msimu wa baridi kali unaleta athari kadhaa za kiafya kwa watoto nchini Tanzania, hali ya hewa ya baridi kali inaweza kuathiri mwili wa mtoto na kusababisha magonjwa na matatizo yafuatayo:

1. Mafua Msimu wa baridi kali huambatana na kuongezeka kwa magonjwa ya mafua na influenza. Watoto wadogo wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vinavyosababisha mafua. Dalili za mafua ni pamoja na homa, kikohozi, pua kujaa, na hisia za uchovu. Watoto ambao wana mfumo dhaifu wa kinga wanaweza kuwa katika hatari ya kupata madhara makubwa kutokana na magonjwa haya.

2. Pneumonia: Pneumonia ni mojawapo ya magonjwa hatari yanayosababishwa na msimu wa baridi kali. Hali ya hewa baridi inaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya bakteria na virusi katika mapafu ya watoto. Pneumonia inaweza kusababisha matatizo ya kupumua, homa, kukohoa, na maumivu ya kifua. Watoto wachanga na wale walio na mfumo dhaifu wa kinga wako katika hatari kubwa ya kuathiriwa na pneumonia.

3. Athari za Ngozi: Baridi kali inaweza kuathiri ngozi ya watoto na kusababisha matatizo kama vile ngozi kavu, kukasirika, na kuwasha. Watoto wadogo wanaweza kuwa na mabusha au michubuko kwenye ngozi kutokana na kuvaa mavazi yasiyofaa kwa kipindi cha baridi. Ni muhimu kuhakikisha watoto wanavaa mavazi yanayowalinda vizuri dhidi ya baridi na kutumia losheni za kujikinga ili kudumisha afya nzuri ya ngozi.

4. Maambukizi ya njia ya hewa: Watoto wakati wa baridi kali wanaweza kuwa katika hatari ya kuambukizwa maambukizi ya njia ya hewa kama vile bronchitis na maambukizi ya sikio. Mabadiliko ya ghafla ya joto na hewa kavu yanaweza kuathiri mfumo wa kupumua wa watoto na kuwafanya kuwa rahisi kuambukizwa. Watoto wanaoishi katika mazingira yasiyo safi na wale walio na matatizo ya upumuaji wako katika hatari zaidi.

Annastazia Thomas yeye ni mzazi wa mtoto mmoja mkaazi wa Kata ya Mjimkuu Manispaa ya Morogoro anasimlia changamoto aliowahi kuipitia katika malezi ya mtoto wake kipindi cha msimu wa baridi kama huu, “Nakumbuka nilikua kwetu kijijini na kwa sababu alikuwa mtoto wa kwanza sikuwa naelewa chochote kuhusiana na athari za baridi kwa mtoto mdogo.

Nilipata shida sana kumsaidia mtoto, hadi bibi alipo amka na kuniambia mfunike nguo nyingi kasha bibi aliwasha moto usikuule ili nyumba ipate joto, kwani hatukua na namna ya kumpeleka kwenye kituo cha afya usiku ule, asubuhi ilipofika hali ile ilikuwa imepungua nikampeleka kituo cha afya baada ya kufika dkt.alivyo mpima alisema “mtoto huyu leo asingepata huduma ya afya uwezekano wa kumpoteza ulikuwa mkubwa” kumbe alikuwa na Pneumonia tangu siku hiyo nikawa makini wakati wa baridi kwa mtotoAnnastazia Thomas, alisema.

KIPI MZAZI/MLEZI AFANYE KIPINDI HIKI CHA BARIDI?:

Hakikisha watoto wanavaa mavazi yanayowalinda vizuri dhidi ya baridi, kama vile sweta, jaketi, soksi, na kofia, Epuka mabadiliko ya ghafla ya joto, kwa mfano, kuwaweka watoto ndani ya vyumba vyenye joto kali baada ya kuwa nje katika hali ya baridi, Hakikisha watoto wanapata lishe bora na ya kutosha ili kuimarisha kinga yao dhidi ya magonjwa, Weka mazingira ya ndani safi na salama ili kuzuia maambukizi ya njia ya hewa, Pata chanjo zinazopendekezwa kama vile chanjo ya pneumonia na influenza.

Baridi kali inaweza kuwa na athari mbaya kwa watoto nchini Tanzania. Watoto wadogo wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa kama vile mafua, pneumonia, na maambukizi ya njia ya hewa. Ni muhimu kuchukua tahadhari za kutosha kwa kuvaa mavazi yanayofaa, kudumisha usafi, na kuhakikisha lishe bora kwa watoto. Vilevile, ni vyema kupata chanjo sahihi ili kulinda watoto dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na msimu wa baridi kali. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuhakikisha kuwa watoto wetu wanabaki salama na wenye afya wakati wa msimu huu.

Elimu na uelewa: Ni muhimu kutoa elimu kwa wazazi na walezi juu ya athari za baridi kali kwa watoto na jinsi ya kuchukua hatua za kuzuia. Hii inaweza kujumuisha kufundisha umuhimu wa kuvaa nguo za kutosha, kuhakikisha lishe bora, na kudumisha usafi, wazazi wanapaswa kuhakikisha wanawanunulia majaket watoto wao pamoja na viatu vizito ambavyo vitawasaidia kujinga wakati wa msimu huu wa baridi.

Post a Comment

0 Comments