Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

UTUMIKISHWAJI WATOTO KWENYE MIGODI:

 

HALI ILIVYO.

Na. John Kabambala. Utumikishwaji wa watoto kwenye migodi ni tatizo bado kwa baadhi ya maeneo ya machimbo ya madini nchini Tanzania.  Watoto wadogo wanashurutishwa kufanya kazi ngumu, hatari na ya kutisha katika migodi, badala ya kupata elimu na kufurahia utoto wao. Athari za utumikishwaji huu ni mbaya kwa maendeleo ya kimwili, kiakili, kijamii, na kiuchumi  pia, Watoto hao hukabiliwa na hatari za kiafya, kunyimwa elimu, na wanakosa fursa za kujenga ujuzi na uzoefu muhimu kwa maisha yao ya baadaye.

Kwa kiwango kikubwa kazi wanazo zifanyishwa watoto hawa kwenye maeneo ya migodi ni kubeba mawe, vifusi, kuponda kokoto na hata kuchota maji yanayotumika kwenye shughuli ndogo ndogo za migodini.

TUMEFIKAJE HAPA?

Sababu kuu ya kuendelea kuwepo kwa utumikishwaji wa watoto kwenye migodi ni umaskini. Familia zenye kipato cha chini zinaweza kuona utumikishwaji wa watoto kama njia ya kuongeza kipato chao. Aidha, udhaifu wa mifumo ya elimu na uhaba wa fursa za ajira kwa watu wazima unachangia hali hii, Serikali na jamii kwa ujumla wanahitaji kushirikiana kikamilifu ili kukabiliana na umaskini, kuimarisha mifumo ya elimu, na kukuza fursa za ajira ili kuvunja mzunguko wa utumikishwaji watoto kwenye migodi.

Stefano Gwandumi siojina lake halisi nikijana mwenye umri wa Miaka kumi na tisa mkazi wa Wilaya ya Tukuyu, katika shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini alizianza akiwana na umri wa Miaka kumi na tano tu, nimemkuta kwenye machimbo yajulikanayo kwa jina la merelani yaliopo Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya hapa anazaidi ya mika mitatu kwenye machimbo haya.

Ndg. Gwandumi nilimuuliza mbinu gani huzitumia vijana kupata kazi kwenye machimbo, wangali wanaumri mdogo? anasema lakini kwanza anataja sababu zinazo pelekea vijana kuelekeza mawazo yao kiutafutaji kwenye machimbo, “Umasiki wa familia yetu ndio chanzo cha kuchagua kazi za machimbo, na vijana tuliopo huku kwenye machimbo umri wetu sio sahihi tunao usema kwa muajiri wakati wa kutafuta au kutafutwa kwenda kufanya kazi, ili uchukuliwe lazima useme una umri wa kuanzia miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

Anasema hata Serikali ngazi ya mtaa, kijiji au kitongoji wao huuliza tu! Una mri gani? Ukisema una miaka kumi na nane au zaidi hawafuatilii kutaka kujua zaidi umri wako, kwahiyo wanalidhika na miaka utakayo waambia ndiomaana ukitafuta kwa undani zaidi kiasi furani vijana wanao fanya kazi hapa kwenye machimbo ni wana umri wa utoto.”

Kwamujibu wa ofisi ya Ustawi wajamii Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Takwimu zinaonesha kwamba zaidi ya watoto elfu saba (7000) wanaishi katika mazingira hatarishi na idadi kubwa zaidi kati ya hao hufanyishwa kazi zisizo za staha, zikiwemo za ugongaji kokoto na kwenye machimbo.

Theresia Mwendapole ni afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, alinieleza kuwa hali ya utumikishwaji watoto kwenye maeneo ya machimbo, mashambani na kupasua kokoto bado ni tatizo, wazazi nimojawapo ya sababu kubwa ya utumikishwaji huo hasa kwenye maeneo ya machimbo ya dhahabu na kupasua kokoto, lakini pia wanao miliki mashimo ya dhahabu wakati mwingine huwatafuta vijana wakiume kwaajili ya kuwasaidia kazi, pasipo kufuatilia uhakika wa umri wao.

"Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Chunya mara kadhaa tunafanya ukaguzi kwen ye maeneo yote ya machimbo ambapo hua tukikuta utumikishwaji watoto tunawakamata wamiliki wa mashimo hayo, na kuwafikisha kwenye ngazi zinazohusika kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi" Alisema Theresia.

Umbali wa mita ishirini hivi (20mt) kutoka Shule ya Msingi Itumbi kufika kwenye machimbo yajulikanayo kwa jina la ITUMBI nilipata nafasi ya kufanya mahojiano na mwanafunzi mwenye uzoefu wa kazi za uchimbaji na uchenjuaji madini anae Shuleni hapo, jinalake tunalihifadhi, "kwenye machimbo unaanza kidogo kidogo wakati mwingine unaenda na mzazi wako, mimi nilikuwa ninaenda na mama yangu kumsaidia kuchekecha mchanga wa dhahabu, ikafikia hatua mama akiwa haendi ninaenda mwenyewe kufanya kazi na pesa nilizo kuwa nikipata nampa mama yangu" alisema mwanafunzi huyo.

Utumikishwaji wa watoto kwenye migodi ni tatizo lenye athari za kielimu katika eneo la Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya, kama ilivyo katika maeneo mengine yanayokabiliwa na suala kama hilo, japokuwa wadau na Serikali wanaendelea kupambana kutokomeza jambo hilo.

Watoto wengi wanashindwa kuendelea na masomo yao wanaposhawishika au kulazimishwa kufanya kazi katika migodi, Hii inasababisha kukatishwa tamaa na kuacha shule kabla ya kukamilisha elimu yao na kukosekana kwa elimu kunawaweka katika hatari ya kukosa fursa za ajira bora baadaye maishani.

Amenye Kasambo ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Itumbi, iliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ameniambia sababu mojawapo zinazo sababaisha kuendelea kwa utumikishwaji watoto maeneo ya machimbo, nakushindwa kutolipatia kipaumbele suala la elimu kwa watoto wao. "Anasema wazazi na walezi hutumia watoto wao kwenye kazi za kutafuta kipato, wakazi huo bado niwafanzi jambo hilo ndio husababisha watoto kushindwa kuhudhulia Shuleni hatimae kuacha kabisa masomo".

JE, SULUHISHO NI NINI ?

Ili kukabiliana na tatizo la utumikishwaji watoto kwenye migodi, wadau mbalimbali mfano; Serikali, NGOs, Vyombo vya habari na Wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu kwenye jamii na maeneo ambayo yana hali na vitendo hivyo vya utumikishwaji wa watoto.

SERIKALI:

Kuweka na kutekeleza sheria na kanuni kali zinazolinda haki za watoto na kuzuia utumikishwaji kwenye migodi. Kuimarisha mifumo ya utekelezaji wa sheria na kuongeza adhabu kali kwa wale wanaokiuka haki za watoto na Kuwekeza katika elimu na kuongeza upatikanaji wa elimu bora ili kupunguza ukosefu wa fursa za ajira na kuchochea maendeleo ya jamii.

NGOs (Asasi za Kiraia):

Kufanya kampeni za kuhamasisha umma na kutoa elimu kuhusu madhara ya utumikishwaji watoto kwenye migodi, Kutoa msaada wa kisheria na kisaikolojia kwa watoto walioathiriwa na utumikishwaji huo na kuwasaidia kupata fursa za elimu na maendeleo na Kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kubuni na kutekeleza mipango endelevu ya kuondoa utumikishwaji wa watoto kwenye migodi.

VYOMBO VYA HABARI:

Kuendeleza uandishi wa habari unaolenga kuelimisha umma kuhusu utumikishwaji wa watoto kwenye migodi na kushinikiza hatua za kukabiliana na tatizo hili, Kuangazia visa vya utumikishwaji na kuwasaidia watoto kushiriki hadithi zao ili kuhamasisha hatua za kuzuia na kuondoa utumikishwaji watoto kwenye migodi na Kutoa jukwaa la mijadala na majadiliano kuhusu suluhisho na mbinu za kukabiliana na tatizo hili.

WANANCHI:

Kushiriki katika harakati za kupinga utumikishwaji watoto kwenye migodi kwa kuwajibika kama wazazi, walezi na jamii kwa ujumla, Kuunga mkono miradi na programu za kijamii zinazolenga kutoa fursa za elimu na maendeleo kwa watoto na familia zinazoishi karibu na migodi na Kuwa walinzi na waangalizi katika maeneo yao na kuripoti visa vya utumikishwaji watoto kwenye migodi kwa mamlaka husika.

MWALIMU MKUU:

Tatizo la utumikishwaji watoto kwenye migodi linahitaji hatua za pamoja na ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali, kupitia jitihada za serikali, NGOs, vyombo vya habari, na jamii kwa ujumla, tunaweza kuzuia athari mbaya za utumikishwaji huu na kutoa fursa bora za maendeleo kwa watoto wetu.

Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao za msingi na wanakuwa na mazingira salama na yenye ustawi bora, kwa kuunganisha nguvu tunaweza kufanikiwa kuondoa utumikishwaji wa watoto kwenye migodi na kuunda ulimwengu bora zaidi kwa kizazi kijacho.

Post a Comment

0 Comments