Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

VITA DHIDI YA VVU KWA VIJANA MKOANI MBEYA:


                                                Picha ya Vailet Bukuku:

Na, John Kabambala: Mkoa wa Mbeya, upo nyanda za juu kusini na mpakani kabisa mwa Tanzania na Zambia, ni eneo lenye uzuri wa asili, utajiri wa tamaduni, na historia ndefu na yapekee katika taifa hilo tulivu la Tanzania. Hata hivyo, mkoa huo pia unakabiliwa na changamoto kubwa ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), ambayo yanawaathiri zaidi vijana balehe. Boda ya Tunduma nikati ya njia kuu zinazo tumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kuelekea mataifa jirani ya Afrika Kusini, Zambia,DRC, Rwanda na mengineyo. Ili kuelewa vyema jinsi tatizo hili lilivyo kiasi cha kuathiri jamii na jinsi linavyoweza kushughulikiwa, fuatilia makala hii inayo angazia historia ya VVU tatizo, chanzo na suluhisho lake mkoani humo.

HALI ILIVYO KUWA:

Ilikuwa ni miaka ya 1980 na 1990 ilishuhudia janga la maambukizi ya VVU lilipo anza kuenea kwa kasi zaidi ulimwenguni pote, na Tanzania haikuwa tofauti na mataifa mengine, Giza nene likaanza kuwaandama vijana balehe na watu wazima wa Mkoa wa Mbeya kwa kimya kimya. Ambapo mlipuko wa maambukizi ya VVU, yaani virusi vinavyosababisha Ukimwi, ulikuwa unapata nguvu kwa kasi zaidi na Vijana wakawa ndio waathirika wakubwa wa janga hilo, mkoa huo ukawa kwenye hatari zaidi kutokana na mwingiliano wa watu wa nchi jirani kupitia boda ya Tunduma.

Kwa mujibu wa Takwimu za Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) za mwaka 2020, zinaonesha kwamba Mkoa wa Mbeya upokwenye nafasi ya tatu kwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya UKIMWI hasa kwa vijana walio kati ya umri wa rika balehe kwa asilimia 9.3%, Mkoa wa Njombe ukiwa nafasi ya kwanza kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 11.4% ukifuatiwa na Mkoa wa Iringa kwa kuwa na maambukizi ya asimia 11.3%,

CHANZO CHA MAAMBUKIZI KWA VAILETH BUKUKU:

Wazazi walitengana, Umasikini wa kipato ndani ya familia, Kubakwa, Uhaba wa elimu na uelewa juu ya VVU na njia za maambukizi, Elimu sahihi shuleni au nyumbani juu ya ngono salama na Afya ya Uzazi, hivi ni miongoni mwa vyanzo vya maambukizi ya VVU.

Kufikia miaka ya 2015 hivi, kijana mmoja jasiri aliekuwa shujaa asiyejulikana kwa hali yake kwa shauku kubwa akaanza kutamani kueneza mwanga wa maarifa kuhusu VVU katika jamii ya vijana wa Mbeya. Alijua kuwa angejitokeza wazi kuzungumzia jambo hilo ilikuwa njia nzuri ya kuwasilisha ujumbe unaoweza kugusa mioyo na kubadilisha mitazamo zaidi kwa vijana wa mkoa huo. Hivyo basi, akaamua kuanza safari yake ya kuwaelimisha vijana kuhusu maambukizi ya VVU kupitia historia yenye kuvutia na ya ukweli katika maisha yake, japo ilikuwa ngumu saana kwake na kuaminika kwa vijana wenzake.

Makala hii imejikita zaidi kufahamu mwenendo wa maisha ya kijana huyo jasiri na shujaa aitwae Vaileth Bukuku tunae mzungumzia leo, tangu alipo tambua hali yake ya maambukizi akiwa na umri wa miaka nane (8) hadi leo hii, mchango wake ni upi kwa jamii inayo mzunguka kuhusu elimu anayo itoa kwa vijana kuhusu VVU.

Picha ya wanufaika wa mradi wa Dreams:

SWALI: Vaileth! Unakumbuka nini kabla hujatambua hali yako kiafya?

Vaileth Bukuku:Nakumbuka nikiwa na umri wa miaka nane tu (8) majira ya saa moja usiku hivi nikiwa nyumbani kwetu kijana mmoja nilie mfahamu kama rafiki wa dada yangu alibadilisha historia ya maisha yangu, kutoka kwenye historia yenye furaha hadi kuwa kumbukumbu yenye uchungu, sitasahau. Nakumbuka ilikuwa sikukuu ya pasaka dada yangu aliniacha nyumbani nikiwa na njaa akaenda disko jioni yapata kama saa moja hivi, alikuja kaka mmoja nyumbani ambae alikuwa na mazoea na dada yangu alipofika akaniuliza Vaileth umekula? Nikamwambia hapana sijala akaniambia njoo uchukue pesa ukanunu mchele uje upike, akanipatia shiringi elfu moja nikaenda dukani kununua mchele.

Badae alirudi tena huyo kaka!  Akaniuliza unatamani kunywa soda? Nikamjibu ndio natamani akaniambia twende dukani ukachukue soda, yule kaka hakunipeleka dukani akanipeleka chooni tulipofika chooni akaniambia nivue nguo nikakataa akanilazimisha nakuniambia ukipiga kelele nitakuua, akaniziba mdomo kwa wake wakushoto akanivua ngua kwa lazima, nakunibaka baada ya kumaliza kitendo kile akakimbia niliumia sana baadae nikajivuta kutoka chooni kuelekea ndani, nilishindwa hata kuingia ndani ya nyumba nika lala mlangoni, dada aliporudi usiku sana akanikuta mlangoni akanibeba hadi ndani”.

 SWALI: Dada yako alipo kufikisha ndani alitaka kufahamu nini kutoka kwako?

Vaileth Bukuku: Kwanza alitaka kufahamu kipi kimesababisha hadi damu zitoke kiasi hiki, nikamuelezea kwamba rafiki yako wakiume ambae hua anakuja hapa nyumbani  alikuja jioni muda mfupi tu baada yaw ewe kwenda disiko alipofika aliniuliza kama nimekula au la! nikamjibu hapana sijala, akanipatia pesa yakwenda kununua kilomoja ya mchele, nilipo rudi kutoka dukani akajatena akaniuliza unatamani kunywa soda nikajibu ndio akaniambia twende dukani nikakununulie, hakunipeleka dukani badala yake akanipeleka chooni kufika huko ndio kanibaka”.

SWALI: Baada ya kumuelezea dada yako tukuio lilivyo tokea alifanya nini usiku ule?

 Vaileth Bukuku:Dada alisema nisinge ondoka yawezekana usinge fanyiwa kitendo hiki”, “kisha akachemsha maji yamoto akanikanda akanipatia na panado akanimbia usimwambie mtu yeyote, hili nijambo la aibu sana”.

SWALI: Baada ya kipindi gani ulianza kuona mabadiliko ya kiafya kwenye mwili wako?

Vaileth Bukuku:Baada ya miezi mitatu nilianza kuumwa mara kwa mara vidonda vikaanza kumtoka nikashindwa hata kuudhulia masomo shuleni, siku moja alikuja jirani yetu nyumbani akaniuliza mbona sikuhizi hujikucheza na watoto wenzako nyumbani na sikia hata shuleni huendi unatatizo gani? Aliuliza lakini sikumwambia, kesho yake akarudi tena ikabidi nimwambie ukweli kuwa mimi nina umwa akanichukuwa akanipeleka hospitali tulipofika daktari akamwambia yule mama nenda polisi ukachukue pf3 maana anaonekena huyu binti kunakitendo alifanyiwa mbali na magonjwa ya zinaa anamaambukizi ya virusi vya ukimwi .

Picha ya Mkurugenzi wa -TCSO:

Mnamo mwaka 2016 katika halmashauri ya jiji la Mbeya kupitia Shirika la Tumaini Community Services lenye makao yake makuu Mkoani huo baada ya kuona ongezeko la maambuki ya virusi vya UKIMWI kwa vijana balehe yanashamiri, walianzisha mradi wakuwawezesha vijana kupata elimu ya afya ya uzazi, elimu ya upimaji wa vvu, elimu ya kujitambua na elimu ya uchumi. Na hapa ndipo Vaileth alipo kutana na Shirika hili kupitia mradi wa ujulikanao kwa jina la Dreams yaani (Ndoto).

Kupitia mradi huo unaotekelezwa Mkoani Mbeya kwa halmashauri tatu ambazo ni Mbeya mjini, Kyela na Mbarali kwa ufadhili wa mfuko wa Rais wa Marekani wa harakati za kupambana na UKIMWI, yaani (PEPFAR) kanda ya Tanzania, ambao unalenga kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa vijana kwa kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya vvu, elimu ya kujitambua, na elimu ya kiuchumi.

Wataalamu kutoka shirika hilo walimshauri binti huyo kuwa mfusi mzuri wa matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi na kuendelea kujilinda yeye mwenyewe na kuwalinda wengine ilikutoendelea kuchochea maambukizi mapya kwa jamii, hasa kwa vijana balehe.

Picha ya Kikundi cha Dreams:

SWALI: Ulikuwa na ndoto gani maishani? 

Vaileth Bukuku: Ndoto zake zilikuwa za kusoma na kuwa muhandisi wa kompyuta, japo hakuifikia ndoto hiyo lakini anashukuru mradi wa Dreams kupitia shirika la Tumaini Community Services baada ya kumfikia walimpeleka chuo cha ufundi VETA kujifunza ufundi wa kushona na kompyuta ambapo baada ya kuhitimu walimkabidhi vyeleani na vifaa vingine vya kufanyia kazi, pamoja na mabinti wezake anao wasimamia kwenye kikundi, na sasa wamejiajili wenyewe wanajipatia kipato, na wakiendeleza elimu kwa vijana kuhusu kujikinga na maambukizi ya VVU.

SULUHISHO LA MAAMBUKIZI YA VVU?

Ushauri wake kwa vijana ambao tiyari wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi Vaileth anasema, wafuate ushauri wa wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia muda wa matumizi sahihin ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi, wajilinde na wawalinde wengine wasisambaze virusi vya Ukimwi kwa makusudi kwa wale ambao hawajapima kujua hali zao za kiafya wajitokeze wakapime kujua hali zao ilikuishi kwa Amani na furaha, ilikama hawana maambukizi waendelee kuwa waamifu na wale ambao watagundulika kuwa na maambukizi ya vvu waanze kliniki mapema.

“Mimi tangu nijue hali yangu ya afya nina amani, furaha na nimfuasi mzuri wa dawa na mwaminifu kwa wengine” Alisema Vaileth Bukuku.

Post a Comment

0 Comments