Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

DUNIA YANGU BORA: HAITA SAHAULIKA KWA WASICHANA WA TANZANIA

 




Na, John Kabambala.

Ulipozinduliwa, ulikuwa ni kama mwanga mdogo uliowaka kwenye giza la usawa wa kijinsia na elimu nchini Tanzania. Mradi wa "Dunia Yangu Bora" uliotekelezwa na Shirika la CAMFED ulianza kama ndoto. Ndoto ambayo ilikuwa na nia ya kuwawezesha wasichana wa vijijini kutimiza ndoto zao za elimu na kuinua hadhi zao katika jamii. Hebu tuwe mashahidi wa makala hii ya mafanikio ya mradi huu kupitia macho ya wasichana wa Tanzania.

Ilikuwa asubuhi na mapema, barabara za kijijini zilijaa furaha na matumaini. Tuliokuwa tunaitwa "Washiriki wa Mradi wa Dunia Yangu Bora" Programu ambayo ilijikita kuwezesha Stadi za Maisha, kumbe walikuwa wanawake wa kesho, wasichana wadogo wa vijijini walio na ndoto kubwa. Walifika kwenye shule wakiwa na vijitabu vyao na mioyo yao iliyojaa shauku ya kuya ona matumaini mapya kama wenzao waliokuwa shuleni.

Zamoyoni Selemani alikuwa miongoni mwa wasichana waliochangamka sana. Kwa mara ya kwanza alipokuwa akipitia mlango wa shule, alihisi kama ameingia kwenye ulimwengu mpya. Na hapo ilikuwa ni baada ya kuhitimu masomo yake, na sasa kuanza mpango wa kujitolea kuwafundisha wasichana na wavulana shuleni mambo ya Stadi za Maisha.

MSAADA WA SHIRIKA LA CAMFED

Shirika la CAMFED nchini Tanzania ni moja ya mashirika yanayopambana kuhakikisha yanachangia katika kutimiza malengo ya 17 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa yaani SDGs, Lengo namba 4 linazungumzia elimu bora na lengo namba 5 linazungumzia usawa wa kijinsia, yote hayo yakiwa yanalenga kutomwacha nyuma mtu yeyote katika maendeleo ya ulimwengu ifikapo mwaka 2030. 

Shirika hili la CAMFED lilileta matumaini kwa wasichana kama Zamoyoni Selemani mmoja kati ya wasicha walionufaika na mpango wa Stadi za Maisha ulio anzishwa na Shirika hilo, ulio kuwa ukijulikana kama "Dunia Yangu Bora" liliwasaidia wasichana na hata wavulana, kuwezeshwa elimu ya Stadi hizo za Maisha, na wo waendelee kujitolea kwenye jamii yao, pamoja na hayo, CAMFED ilianzisha vikundi vya wasichana shuleni ambavyo vilijengewa ujasiri wa uongozi miongoni mwa wasichana hao.

MIONGONI MWA WANUFAIKA WA MRADI HUU WANASEAMAJE?

Asha ni mnufaika wa mpango huu wa kujitolea kufundisha vija Stadi za Maisha Shuleni na sasa amekuwa muelimishaji maarufu anayewasaidia wengine kama yeye ambavyo alisaidiwa, kutokana na sababu mbalimbali wamejikuta wakiishi katika mazingira magumu. Asha anasema, “mimi kama msichana nimepitia huko kwa sababu baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari, baba alikuwa na matatizo yaliyompelekea kuugua kwa muda mrefu. Kwa hivyo ikanibidi niende kutafuta kazi, nikaajiriwa.”  

Mpango huu wa Stadi za Maisha na uelimishaji lika kupitia "Dunia Yangu Bora" ulibadilisha maisha ya wasichana hawa wa Tanzania. Kupitia elimu, wasichana walianza kuona fursa nyingi zaidi. Walijifunza kuhusu afya, haki zao, na jinsi ya kusimama kidete dhidi ya ubaguzi na unyanyapaa uliokuwa ukifanywa kwenye jamii yao dhidi ya wasichana. Walijenga ujasiri wa kuwa viongozi wa kesho na kuchangia katika maendeleo ya jamii zao.

ZAMOYONI AMENUFAIKAJE NA SHIRIKA LA CAMFED?

Mbali na elimu alio ipata kupitia uwezeshaji mwingine wa Shirika, alipata elimu ya Stadi za Maisha kupitia mpango wa "Dunia Yangu Bora" uliokuwa ukitekelezwa na Shirika la CAMFED Tanzania ulikuwa kama jua linalong'aa katika maisha ya msichana huyo, kama ambavyo Zamoyoni Selemani alivyo pata nafasi ya kufanya kazi kama mratibu wa miradi ya Shirika hilo kwa Wilaya mbil ikiwemo Wilaya ya Kilosa na Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, na hapa anelezea zaidi.

 miradi yetu imejikita sana katika kumsaidia mtoto wa kike, katika elimu yake lakini hatuishii katika elimu. Vilevile kwa mto wa kike ambaye ameshamaliza shule, tunamwendeleza katika vyuo vya ufundi, lakini pia tunawapeleka katika vyuo vya kati, ngazi ya cheti na diploma, lakini pia wale ambao hawana sifa za kwenda vyuo tunawapa miradi ambayo wanaweza wakafanya biashara zao katika kata zao, hii yote ni kuhakikisha kwamba mtoto wa kike hawezi kuwa tegemezi katika mazingira ya sasa.” Alisema Zamoyoni Selemani.

Kupitia macho yao, tunajifunza kuwa kutoa fursa sawa za elimu na Stadi za Maisha kwa wasichana ni uwekezaji katika mustakabali bora wa jamii na taifa kwa ujumla. Mpango huu ulibadilisha maisha ya wasichana hawa na kuwapa matumaini na ujasiri wa kusimama na kuchukua hatamu za maisha yao. Hii ni simulizi ya mafanikio, na ni matumaini yetu kuwa jitihada za kuwawezesha wasichana zitaendelea kuangaziwa na kusaidiwa ili kujenga dunia bora kwa wote.

TUSIKIE KUTOKA KWA MWALIMU MSIMAMIZI WA MPANGO HUO SHULENI:

Elisifa Nasali ni mwalimu katika Shule ya sekondari Kimamba na pia ndiye mlezi wa wanafunzi wanufaika wa mradi wa CAMFED anasema, wengi kama Zamoyoni na Asha wamenufaika lakini uhitaji bado ni mkubwa, watoto ni wengi ambao wana shida. Ingewezekana tungeongezewa hata namba ya watoto ambao wangepata msaada Wasichana wengi walionufaika na mradi wa "Dunia Yangu Bora" uliotekelezwa na Shirika la CAMFED Tanzania walipata msaada mkubwa ambao ulibadilisha maisha yao kwa njia nyingi muhimu” alisema Mwalimu.

Aidha Mwl. Nasali alisema mradi huu ulitoa ufadhili wa elimu kwa wasichana ambao uliwawezesha kulipia ada za shule, kununua vifaa vya shule, na kufidia mahitaji yao ya kila siku. Ufadhili huu ulikuwa kama daraja lao kuelekea elimu bora na fursa za kujifunza. Wasichana walinufaika na vifaa vya shule kama vile vitabu, sare za shule, na vifaa vingine muhimu. Hii iliwawezesha kushiriki kikamilifu kwenye masomo bila kikwazo chochote.

SHIRIKA LILI WAFANYIA NINI KINGINE?

CAMFED ilianzisha vikundi vya wasichana shuleni ambavyo vilikuwa na malengo ya kuwajengea ujasiri, kuwafundisha kuhusu haki zao, na kuwawezesha kuwa viongozi katika jamii zao. Wasichana walipata mafunzo ya kuendeleza ujuzi wa maisha kama vile stadi za ujasiriamali na uongozi. Mradi ulitoa ushauri na msaada wa kisaikolojia kwa wasichana. Hii ilikuwa muhimu katika kuwasaidia kukabiliana na changamoto za kibinafsi na za kijamii ambazo zinaweza kuwa na athari kwa masomo yao.

CAMFED ilifanya kazi na jamii kubadilisha mitazamo kuhusu elimu ya wasichana. Wasichana waliwezeshwa kusimama kidete dhidi ya ubaguzi wa kijinsia na unyanyapaa wa kijamii unaoweza kuwazuia kufikia ndoto zao. Baadhi ya wasichana walinufaika na ufadhili wa kuanzisha miradi midogo midogo ya kujiajiri. Hii iliwawezesha kujifunza stadi za ujasiriamali na kuwa na njia mbadala za kujipatia kipato.

Kupitia msaada huu, wasichana waliweza kusoma bila vikwazo vikubwa, kujenga ujasiri na uongozi, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii zao. Walipata fursa za kutimiza ndoto zao na kuwa nguvu ya mabadiliko katika jamii zao na taifa kwa ujumla. Mpango wa "Dunia Yangu Bora" ulikuwa mwongozo wa maisha yao na kichocheo cha mafanikio yao.

Hakika CAMFED wasichana wote walionufaika kupitia mpango huu hawata kusahau:

Post a Comment

0 Comments