Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

HISTORIA YA MTOTO ALIE UGUA HOMA YA INI:

 

Nenka Bryiyo

Usiku ule tuli lala na kuamka salama asubuhi....lakini hakuna hata mmoja kati yetu alie hisi kuwepo kwa hali tofauti kiafya kwa mtoto wetu….. nikana kwamba siku hiyo ilikuwa nyeusi  tiii, yenye giza nene isio na huruma wala tumaini hata kidogo….saa chache tu baada ya kupambazuka asuhi, historia ya furaha iligeuka kuwa ya huzuni,,, sitaisahau siku hii, hakika nikumbukizi yenye uchungu…..


Na, John Kabambala: Katika kijiji kidogo kilichopo karibu na mji mkuu wa Tanzania Dodoma, alipo zaliwa msichana mmoja tulie mpa jina la Nenka Bryiyo . Mtoto wa kwanza na wapekee katika familia yao ya mzee Bryiyo Mkoma, baada ya wazazi wake kuhangaika kwa zaidi ya miaka kumi hivi kwenye ndoa yao pasipo kupata mtoto, baadae akazaliwa mtoto wa kike wakamwita “ Nenka”  hakika walimfurahia sana kumpokea duniani. Kuanzia utotoni, Nenka alikuwa na tabasamu la kuvutia na alikuwa na ndoto kubwa za kufikia malengo yake maishani.

Maisha yake ya utotoni yalijawa na furaha na upendo kutoka kwa familia yake. Nenka alikuwa na shauku ya kujifunza na alipenda shule. Aliweka bidii kusoma na kufaulu vizuri katika masomo yake. Pamoja na changamoto za kiuchumi katika familia yao, wazazi wake walijitahidi kuhakikisha wanampa elimu bora ili azifikie ndoto zake.

KIINI CHA MAKALA HII KINAANZIA HAPA: NI KIPI KILIMSIBU NENKA?

Nakumbuka akiwa darasa la tatu (3) maisha yake yalibadilika ghafla wakati Nenka siku isio tarajiwa alianza kuonyesha dalili za kuumwa. Alipata homa kali, uchovu, macho na ngozi yake yakawa na rangi isiyo ya kawaida” alisema Steloy Jaiso mama mzazi wa Nenka.

Wazazi wa huyu mtoto walipatwa na wasiwasi kubwa lakini kwa haraka sana walichukua hatua ya kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi zaidi, maana mtoto huyu alikuwa kama mboni ya macho yao.  

Nenka alihitaji matibabu ya haraka na tena matibabu ya kibingwa. Wazazi wake, ingawa walikabiliwa na changamoto ya kifedha, walifanya kila wawezalo kumkatia bima ya afya ili kumwezesha mtoto wao kupata matibabu yanayohitajika, kwa wakati sahihi bila kujali hali walio nayo ngumu ya kiuchumi.

Baada ya uchunguzi wa kina, daktari alikuja kutuelezea majibu walio yabaini alipo uliza “wazazi wa Nenka wapo?” Mke wangu alipiga kelele sana kwa hofu akidhani kwamba Nenka amefariki..kumbe haikua hivyo daktari alisema mtoto huyu lazima aanzishiwe matibabu kuanzia sasa ili kunusuru uhai wake” Alisema Bryiyo Mkoma baba wa mtoto.  

Bryiyo Mkoma

HOMA YA INI NI NINI?

Ili kupata majibu ya maswali yangu nilimtafuta daktari wa watoto kutoka katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro Dkt. Hawa Ngasongwa, nae anatoa ufafanuzi huu kuhusu homa ya INI. “Homa ya ini ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoingia mwilini kwa binadamu na kusababisha ini kupoteza uwezo wakufanya kazi zake vizuri na kusinyaa na mwishoni kabisa kusababisha saratani inayoweza kupelekea kifo kwa watoto” alisema.

CHANZO CHA UGONJWA HUU NI NINI?

“Aasilimia kubwa kwa watoto ni maambukizi kutoka kwa mama mjamzito mwenye maambukizi haya kwenda kwa mtoto wake mchanga wakati wa kujifungua, Kushirikiana vitu vya ncha kali kama kiwembe,sindano mswaki nk na Kuongezewa damu yenye maambukizi ya homa ya ini”

 DALILI ZA UGONJWA HUU WA INI KWA WATOTO NI ZIPI?

“Hizi dalili zinafanana na maradhi mengine ya Watoto, hivyo  ni muhimu kufanya vipimo haraka mara tu mtoto akionesha dalili hizi, kuna watoto wasioonyesha dalili yoyote, lakini miongoni mwa viashiria vya ugonjwa huu moja wapo ni kuchoka, homa, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu na hata kutapika, manjano kwa manjo na Ngozi ya mwili (jaundice), kuharisha, maumivu ya  tumbo, kupata mkojo wenye rangi iliyokooza (cocacola urine)” Dkt. Ngasongwa

Madhara ya homa ya ini ni makubwa kwa watoto, inashauriwa kupata chanjo mara tu baada ya kupima kama hunamaambukizi ya homa ya ini ili kujikinga. Chanjo hii inasaidia kuandaa mwili kutengeneza kinga dhidi ya ugonjwa huu. Na ili kinga hii iwe thabiti, ni lazima kukamilisha awamu zote za chanjo kulingana na muongozo wa njano hii.

Usiku ule tuli lala na kuamka salama asubuhi....lakini hakuna hata mmoja kati yetu alie hisi kuwepo kwa hali tofauti kiafya kwa mtoto wetu….. nikana kwamba siku hii ilikuwa nyeusi  tii, yenye giza nene isio na huruma wala tumaini hata kidogo….saa chache tu baada ya kupambazuka asuhi, historia ya furaha iligeuka kuwa ya huzuni,,, sitaisahau siku hii, hakika nikumbukizi yenye uchungu”Maneno hayo yalisemwa na Steloy Jaiso.

UTAMKINGAJE MTOTO DHIDI YA HOMA YA INI?

Njia za kujikinga na athari za homa ya ini kwa watoto, ni kupima mama wajawazito na kuwapa chanjo na matibabu na watoto wao mara tu wakijifungua, kujikinga na kuchangia vitu vya ncha kali, kupatiwa damu yenye maambukizi na kuwa na taadhari kwa njia zote za maambukiziDkt. Ngasongwa

Matibabu ya homa ya ini kwa watoto, kama imegundulika mapema na kuanza matumizi ya dawa hupona, Dawa atakazo tumia ni kuliingana na shida ya mtoto kama za kuzuia kutapika, kupoza homa, lishe bora na kupumzisha mwili.

Kuna mionzi (chemotherapy) kulingana na steji ya saratani ya ini Kuna kupandikiza ini (liver transplant), Lishe bora , kula mlo kamili na kupumzika vya kutosha, Mara tu anapoona dalili tu apelekwe hospitali kupata ushauri na matibabu sahihi.

Dkt. Hawa Ngasongwa

                                                  JE HOMA YA INI HUTOFAUTIANA?

Dkt. Hawa NgasongwaNdio, kuna aina ya homa ya ini inapona haraka tu na hata bila matibabu, kuna zingine hupelekea kusinyaa kabsa kwa ini (liver cirrhosis )na kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi, na unaweza umwa tena homa ya ini baada ya kupona ikisabbaishwa na mambo mbalimbali”.

TUREJEE TENA KWA NENKA BRYIYO

Kwa mujibu wa maelezo ya Bryiyo Mkoma  baba mzazi wa mtoto anasema, baada ya miezi kadhaa Nenka Bryiyo nuru ilianza kuonekana katika afya yake akapata nafuu hatimae kupona, msichana huyu  alivutiwa na huduma za afya kutokana na namna madaktari walivyo kuwa wakihangaika kwa upendo na upole kuokoa uhai wake. Hapo ndipo wazo la kuwa mtaalamu wa afya ili aweze kusaidia wengine walio katika hali kama aliokuwa nayo lilipo chipua.  Baada ya kurejea  Shuleni na kuendelea na masomo yake kama kawaida, alijifunza na kuweka bidii kwenye masomo ya afya, na anaendelea vizuri.

Historia ya mtoto Nenka ilikuwa moja ya changamoto kubwa kurejesha afya yake ya awali, lakini pia ni historia ya nguvu, ujasiri, na yenye matumaini. Alipitia wakati mgumu katika maisha yake, lakini kupitia juhudi za Madaktari, wazazi wake, walibadilisha maisha yake na kurejesha furaha maishani mwake na katika familia na jamii yake maana kwa pamoja walionyesha umuhimu wa mshikamano ili kuleta matokeo chanya.

MTAZAMO WA DAKTARI NA WAZAZI KUHUSU HOMA YA INI NI UPI?

Dkt. Hawa Ngasongwa anasema wazazi/walezi wachukue hatua mara baada tu ya kuona hali tofauti kwa watoto wao isio ya kawaida, wapelekwe kwenye vituo vya avya ili wataalamu wakawanyie uchunguzi na kuanzishiwa matibabu kwa ushauri na kwa maelekezo ya mataalamu wa afya. Kwa kufanya hivyo magonjwa yote yaweza kutibika kama sio kuzuilika yasiendelee na kumathiri mtoto.

Sisi hatukusita baada ya kuona hali ya mtoto wetu imebadilika kwa siku hiyo, nilicho mwambia mke wangu chukua bima na umbebe mtoto mgongoni twende kituo cha afya kwa ajili ya kumfanyia vipimo mwanetu. Mimi pia nili beba baisikeli na kuwapakiza kuelekea kituo cha afya, hivyo wazazi wenzangu kuna haja ya kukimbilia kituo cha afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto wetu, kama ambavyo sisi tulifanya na tumejionea matokeo yake Bryiyo Mkoma.

Post a Comment

0 Comments