Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

LIKIZO YA UZAZI KWA MAMA ALIE JIFUNGUA MTOTO KABLA YA MUDA/NJITI

                                       Picha kutoka unnews.

Na, John Kabambala.

Nukuu muhimu ambayo unapaswa kuendelea kuimbuka kupitia usomaji wa makala hii ni kwamba: "Kila mtoto njiti ana thamani na uwezo wa kipekee."  Kwani "Kila mtoto njiti ni kipande cha hazina kwenye jamii yetu." Kuzaliwa kwa mtoto njiti ni changamoto inayohitaji upendo, ujasiri, na msaada kutoka kwa familia, jamii, na serikali. Mtoto njiti ni mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati au na uzito wa chini kuliko wastani. Hali hii inaweza kuwa ya kusumbua na kutisha kwa wazazi hasa kwa wale ndio uzao wao wakwanza, lakini inatoa fursa ya kipekee ya kuonyesha nguvu ya upendo na ujasiri wa binadamu.

Mtoto njiti, mara nyingi huwa na matatizo ya kiafya yanayohitaji uangalifu wa ziada. Wakati mwingine, huenda wakahitaji kuwa kwenye kitengo cha utunzaji maalum kwenye hospitali kwa muda mrefu na Upendo wa Familia ni Nguzo ya Kwanza ya Mafanikio kwa mtoto huyu”.

Mama au wazazi wa mtoto njiti wanapokuwa na upendo wa dhati na subira, wana uwezo wa kufanya maajabu. Mtoto njiti anahitaji upendo mkubwa na uangalifu wa familia yake kwani upendo unaweza kuwa nguvu ya kutia moyo katika kipindi kigumu. Kuwa karibu na mtoto wako, kumtunza, na kumpa nafasi ya kujenga uhusiano wa karibu kunaweza kusaidia katika kupona na maendeleo ya mtoto.

Naam, Makala hii leo inachungulia dirisha la utoaji ruhusa ya likizo ya Uzazi kwa kina mama walio jifu ngua watoto njiti. Pata utulivu wakutosha ilikusoma na kuelewa nyaraka zinasemaje, wabunge wali wahi kuhoji nini juu ya Likizo ya Uzazi, wataalamu wa afya wanashauri jambo gani kuhusu likizo ya uzazi kwa akina mama wanao jifungua watoto njiti.

Tuanzie hapa kwenye Sheria ya Majadiliano ya Utumishi wa Umma Na. 19 ya 2003, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya 2004 Na Sheria ya Asasi za Kazi Na. 7 ya 2004. Hata sharia hizi znyewe zilipo tungwa hazikuwajumuisha kina mama wanaojifungua watoto njiti, zinasema mfanyakazi anastahili likizo ya uzazi ya malipo ya siku themanini na nne (84) au siku mia moja (100) iwapo atajifungua mtoto zaidi ya mmoja katika mzunguko wa miezi 36.

 

SWALI: Je, wakati zinatungwa Sheria hizi hapakuwa na kina mama waliokuwa wakijifungua watoto kabla ya muda wao (njiti), tena ambao ni watumishi wa umma?

Mtoto njiti, mara nyingi huwa na matatizo ya kiafya yanayohitaji uangalifu wa ziada. Wakati mwingine, huenda wakahitaji kuwa kwenye kitengo cha utunzaji maalum kwenye hospitali kwa muda mrefu. Mama na familia wanapokutana na hali hii, wanajikuta katika hali ya kutatanisha, lakini ni muhimu kushirikiana na wataalamu wa afya ili kutoa huduma bora kwa mtoto na kuwasaidia wazazi kuhimili changamoto hizi” Huyo ni Dkt. Haika Mariki kutoka Chama cha Madaktari bingwa wa watoto Tanzania (PAT).

JE, BUNGENI KUNAYAPI?

Mwaka 2019 Juni, Mbunge wa Viti Maalum, ANATROPIA THEONEST Aliwahi kuuliza swali bungeni….Je, ni likizo ya muda gani wamekuwa wakipewa wazazi (watumishi wanawake na wanaume) pale wanapopata watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti?

 

2015-2020

Session 15

Sitting 52

Public Service Management

Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)

450

2019-06-25

Alie kuwa NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA kwa wakati huo Dr. Mary Machuche. Alijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, “Kwa mujibu wa Kanuni H. 12(2) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za Mwaka 2009, mtumishi wa umma mwanamke anapojifungua mtoto hupewa likizo ya uzazi ya muda wa siku 84 mara moja kila baada ya miaka mitatu.

 

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanuni H. 12(3) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009, mtumishi husika anapojifungua watoto zaidi ya mmoja hupewa siku 14 zaidi za likizo ya uzazi na hivyo kuweza kuwa siku 98. Kanuni tajwa haikubanisha muda wa likizo ya uzazi kwa mtumishi anayejifungua mtoto njiti”.

Matukio ya uzazi wa mapacha zaidi ya wawili (triple) na watoto njiti ni nadra kutokea mara kwa mara. Hivyo, Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009 hazikuainisha masharti ya likizo ya uzazi kwa matukio kama hayo. Hivyo, natoa wito kwa waajiiri na wasimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Utumishi na kuomba kibali cha kuongezewa muda wa likizo ya uzazi kwa watumishi wa umma walio chini yao pindi wanapojifungua watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti.

Kwa mujibu wa Kanuni H.13 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009, Mtumishi wa Umma mwanaume hupewa likizo ya uzazi ya angalau siku tano kuanzia siku ya kuzaliwa mtoto ili aweze kuhudumia familia yake. Hata hivyo, iwapo kuna sababu za msingi zinazomlazimisha kuendelea kuhudumia familia kwa ukaribu, mtumishi husika anaweza kuomba ridhaa kwa mwajiri wake ya kuongezewa ili siku kadhaa kuhudumia familia.

Inapotokea mtumishi wa umma kajifungua watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti na kulazimika kuwa na muda wa zaidi wa kuhudumia watoto hao, mwajiri wake anapaswa kuwasilisha hoja kwa Katibu Mkuu (Utumishi) ilia toe kibali cha kuongeza muda wa likizo ya uzazi.

 

 Dkt. Haika Mariki anasema kutokana nachangamoto wanazo zaliwanazo watoto hao ambao hawajatimiza mudawo wakuzaliwa, kitaalamu tunaendelea kuishauri Serikali kupitia bunge waweze kupitisha sharia itakayo walinda na kuwawezesha wamama wanao jifungua kabla ya wakati, na wakiwa waajiliwa waweze kulea watoto wao kwa kipindi cha miezi 6 na kwa baba wa mtoto njiti apewe likizo ya mwezi 1, ili aweze kumsaidia mwezi wake kuhudumia mtoto wao.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inaonesha kwamba kuzaliwa kabla ya wakati ndio sababu kuu ya vifo vya watoto wachanga walio chini ya umri wa miaka mitano, na kuchangia takriban 40% ya vifo vya watoto wachanga. Ikizingatiwa kuwa kila mwaka watoto 336,000 wanaozaliwa kabla ya wakati huzaliwa nchini Tanzania, 11,500 hufariki kutokana na matatizo ya kuzaliwa kabla ya wakati.

Ikumbukwe kwamba Taasisi hii imekuw na mchango mkubwa katika kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati pamoja na mama zao, ikiwemo kuwapatia vifaa muhimu na mahitaji ya lazima baada ya kujifungua wawapo bado hospitali au waliopo nyumbani.

Hata hivyo Taasisi hiyo kwa kushirikiana wadau mbali mbali hivi karibuni wamekuwa wakiiomba Serikali kufanyia marekebisho ya Sheria ya Likizo ya Uzazi hasa kina mama wanao jifungua watoto kabla ya wakati (njiti), kuongezewa muda wa likizo hiyo kufia miezi 6 na mwezi 1 kwa baba wa mtoto huyo, tofauti na ilivyo sasa siku 84 kwa mama anae jifungua mtoto kabla ya wakati na siku 5 kwa baba mwenye mtoto. “Hadi sasa Serikali imetulia kama bahari yenye kina kirefu” Nilini wataiona nuru wazazi wanaojifungua watoto wa aina hii?.

Post a Comment

0 Comments