Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

VIJANA WENYE ULEMAVU NA ELIMU YA AFYA YA UZAZI:


Na, John Kabambala: Hebu tafakari…..ikiwa mtu wa kawaida usie na ulemavu unao onekana….unapata changamoto ya kuelewa nini maana ya afya ya uzazi…na yawezekana kabisa hujui inatolewa wapi na ufanyeje ili uipate… je, vijana wakike na wakiume wenye ulemavu tena maisha yao yote nikushinda nyumbani au kwenye vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalumu wataipataje….?.

Top of Form

Makala hii inaangazia jambo hili muhimu kwa vija balehe katika mkoa wa Morogoro, ambapo utasoma kilicho zungumzwa na vijana wenyewe kutoka kwenye vituo vya kulelea watoto na vijana wenye mahitaji maalumu,Taasisi za vija wenye makao makuu yake mjini Morogoro,  pamoja na Daktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro.

Hadi leo, elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenye ulemavu wa viungo nchini Tanzania imekuwa ikipuuzwa au kupewa kipaumbele kidogo, hili likiwa mojawapo ya makundi maalum yenye nahaki pia ya kuelimishwa jambo hili. Hii imekuwa changamoto kubwa inayowakabili vijana hawa walio nahaki sawa na wenzao wasio na ulemavu kupata elimu na habari muhimu kuhusu afya ya uzazi.

Mara nyingi, vijana wenye ulemavu wa viungo wanakabiliwa na unyanyapaa na ubaguzi kutoka kwa baadhi ya wanajamii hili nijambo lisilo fichika. Hata hivyo baadhi ya watu huamini kuwa watu wenye ulemavu hawana haki au uwezo wa kujihusisha na masuala ya ngono na afya ya uzazi. Hii inaweza kusababisha kukosa kujitambua na haki za kijinsia kwa vijana hawa, na hivyo kupuuzwa kwa elimu ya afya ya uzazi.

Katika maeneo mengi, vijana wenye ulemavu wanakabiliwa na uhaba wa rasilimali za elimu na huduma za afya. Hii inaweza kuwa kutokana na ukosefu wa miundombinu inayowafaa, vifaa vya kujifunzia na kufikia habari, na hata wataalamu wa afya walioelimika kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa njia inayofaa.

Vijana wenye ulemavu hawapati elimu muhimu ya afya ya uzazi katika shule au katika jamii yao. Hii inaweza kuwa kutokana na kutokuwepo kwa programu za elimu ya afya ya uzazi zinazojumuisha mahitaji yao maalum, au hata kutokana na wataalamu wa afya kutokupata mafunzo yanayowawezesha kutoa elimu kwa njia inayofaa kwao.

Kwa muktadha huo wa changamoto nyingi zinazokabiliwa na vijana wenye ulemavu, wakati mwingine elimu ya afya ya uzazi huonekana kuwa kipaumbele cha chini kabisa, hasa wanao ishi kwenye familia zenye kipato cha chini na hata wanao inshi kwenye vituo vya kulelea watoto na vijana wenye mahitaji maalumu. Mambo kama upatikanaji wa elimu bora, huduma za afya, na haki za msingi mara nyingine hayapewi kipaumbele zaidi. Hii inaweza kusababisha kupuuzwa kwa umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya ya jamii, afya ya uzazi kwa vijana wa rika balehe ni muhimu mno elimu hii, kwani katika kipindi hiki vijana hukabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo mimba za utotoni, magonjwa, na utoaji mimba usio salama, ambapo bila elimu muhimu kutolewa zinaweza kuhatarisha maisha na ustawi wao.

Bi. Linda Ngido ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mehayo Centre for Disabled Young People, kituo kinachojihusisha na kuwapatia ujuzi na fursa vijana wenye ulemavu ambaye ameiambia Tanzania Kids Time kwenye mahojiano maalum kwamba hajawahi kuona wataalamu wa afya ya uzazi kutoka serikalini au kwenye asasi za kiraia kufika kituoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu ya afya ya uzazi.

“Kuna wakati ambao wasichana wanafikia umri wa kupata hedhi, ukimuelekeza binti mwenye ulemavu kuhusu kutumia vifaa vya kujistiri hawataki,” anaeleza Bi, Ngido ambaye ni mwalimu kitaaluma. “Wakati mwingine wanavitupa.”

Bi, Ngido haelewi ni kwa nini Serikali na wadau hawajikiti kwenye kuwapatia vijana wa rika la balehe wenye ulemavu elimu ya afya ya uzazi wakati watu hawa pia ni binadamu kama walivyo watu wengine ambao hukua na kuanzisha familia zao.

“Watoto wenye ulemavu nilioanza kuwa nao kwenye kituo hiki, wavulana na wasichana, sasa hivi ni watu wazima, wameoana wenyewe na wana watoto wanasoma,” anaeleza Ngido ambaye alilazimika kuacha kazi yake ya ualimu kufanya kazi yake ya sasa. “Kwa hiyo, siyo kwamba hawa watu wenye hali hii hawawezi kuwa na familia. Hapana, wanaweza.”

Tanzania Kids Time ilitembelea kituo kingine kijulikanacho  Erick Memorial Foundation for Education and Rehabilitation for the Disabled (EMFERD) kituo hiki kipo mkoani Morogoro kinajihusisha na kutoa huduma kwa watoto na vijana wenye ulemavu.

Hapa na kutana na baadhi ya vijana wanao lelewa kwenye kituo hiki, wengi wao wako katika rika balehe ambao ni wenye ulemavu, walikiri kwamba hawajawahi kufikiwa na kupatiwa elimu ya afya ya uzazi, kutoka kwa wataalamu wa afya serikalini au Taasisi zingine za kiraia hali ambayo wanasema inawasononesha na kuwatenga na jamii.

“Hii huduma tunaihitaji kwa sababu watu wenye ulemavu nao wana haki zote za msingi kama vile ya] kuoa au kuolewa,” Benedict Mwenyasi, kijana mwenye ulemavu wa viungo kutoka EMFERD, aliiambia Tanzania Kids Time, “[Wadau] sisi wanatusahau [kutupatia elimu hii].”

                                   
Je,wadau wanaizungumziaje Serikali kushirikiana na wadau wengine wa afya ya uzazi nchini Tanzania kuweka mikakati na kuchukua juhudi za pamoja za kuhakikisha kwamba kundi hili nalo linafikiwa kwenye utoaji wa elimu ya uzazi nchini.

Moja kati ya wadau hawa ni Obed Mtagulwa, mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa Care Youth Foundation, shirika linalojihusisha na kutoa elimu ya uzazi kwa vijana rika balehe.

“Hizo sehemu wanazokaa watu wenye mahitaji maalum huwa tunaenda kwa ajili ya kutoa huduma ya misaada pekee yake, bado hatujafika kupeleka elimu ya afya ya uzazi,” anakiri Mtagulwa. “Kuna haja kubwa sana ya kuwapa elimu [watu hawa].”

Nikabisha hodi ofisi yam ganga mkuu wa mkoa kitengo cha afya ya uzazi nakutana na daktari bingwa wa afya ya uzazi Hospitalini hii ya rufaa Morogoro Dkt. Deodata Ruganuza yeye anaanza kwa ameonya kwamba endapo wadau hawataweka kipaumbele kwenye kuwapatia watu wenye ulemavu elimu ya afya ya uzazi haki za msingi za watu hao zitakuwa hatarini kukiukwa.

“Tusipoweka kipaumbele katika hili kundi, [vijana walemavu walio katika rika balehe] watakuwa wanakosa kitu cha muhimu sana kwao na kwa familia zao watakazoanzisha,”

Ni haki ya kila kijana, bila kujali ulemavu wake, kupata elimu sahihi kuhusu afya ya uzazi. Elimu hii inawawezesha kujitambua, kujilinda na kujiamulia katika masuala yanayohusu miili yao. Ni muhimu kwa jamii kuondoa unyanyapaa na ubaguzi, kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za elimu na huduma za afya, na kuhakikisha kuwa elimu ya afya ya uzazi inatolewa kwa njia inayojumuisha mahitaji ya vijana wenye ulemavu.

Hii itasaidia kujenga jamii yenye uelewa zaidi na yenye haki kwa kila mmoja, Dk Ruganuza aliiambia Tanzania Kids Time kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake mjini Morogoro.

 

Post a Comment

0 Comments