Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

ELIMU YA STADI ZA MAISHA NI MKOMBOZI KWA WASICHANA TANZANIA.

Mkurugenzi wa Camfed, Viongozi kutoka Wizara ya Elimu, Ofisi ya Rais-Tamisemi na Kamati ya Halmashauri ya Malinyi itakayo simamia program ya Stadi za Maisha Shuleni wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mkutano. 

Na, John Kabambala:

Mwaka 2013, Tanzania ilishuhudia mwanzo wa mabadiliko makubwa katika elimu ya msingi na sekondari kupitia mradi wa kusisimua ulioanzishwa na Shirika la CAMFED (Campaign for Female Education). Mradi huu ulikuwa na lengo la kuboresha stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike na kuwapa fursa zaidi za elimu na ujifunzaji. Makala  ya mradi huu inaanza na jitihada za CAMFED kuleta mabadiliko chanya katika elimu na maisha ya wanafunzi wa kike nchini Tanzania.

Kwa muda mrefu, wanafunzi wa kike nchini Tanzania wamekutana na changamoto nyingi katika kupata elimu bora na kufikia malengo yao ya elimu. Hali hii ilitokana na sababu kama vile umaskini, mila na desturi potofu, na upungufu wa rasilimali za elimu. CAMFED, ni  shirika la kimataifa linalofanya kazi katika nchi kadhaa za Afrika, lilichukua hatua kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na wadau wengine kuanzisha mradi wa Stadi za Maisha kwa Wanafunzi wa Kike kwenye shule za Sekondari.

Sophia Leonard yeye nimnufaika wa program mbalimbali zinazo wezeshwa na Shirika la Camfed Tanzania, na amepata mafunzo na kuhitu ya kuwa muwezeshaji wa Stadi za Maisha kwa vijana Shuleni, anasema kupitia elimu anayo wafundisha vijana shuleni tangu Mwaka  2014 kwa zaidi ya miaka nane (8) kwenye Shule ya Sekondari “KUTUKUTU” iliopo Wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro . Sasa Wlimu, Ofisi za Elimu na Jamii zinashekhlekea mavuno mazuri ya elimu hiyo ya Stadi za Maisha kwa watoto wao, Maana kiwango cha taaluma kimeongezeka kuliko ilivyo kuwa kabla.

ELIMU YA STADI ZA MAISHA  KWA VIJANA HUCHOCHEA NINI HASA?

Kuandaa Wanafunzi kwa Maisha Baada ya Shule:

Elimu ya stadi za maisha inawasaidia wanafunzi kuwa tayari kwa maisha baada ya kumaliza masomo yao. Kupitia kujifunza stadi za maisha kama vile ujasiriamali, uongozi, ujuzi wa kujitegemea, na mawasiliano, wanafunzi wanaweza kuwa na uwezo wa kufanikiwa katika kazi zao na kuchangia katika maendeleo ya taifa. Na Serikali inapaswa kusimamia ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata mafunzo haya muhimu katika shule za sekondari.

Kujenga Jamii yenye Ujuzi na Ubunifu:

Stadi za maisha hufundisha wanafunzi jinsi ya kutatua matatizo, kuwa wabunifu, na kuwa na uwezo wa kubadilika katika mazingira mbalimbali. Kwa kusimamia elimu hii, serikali inaweza kusaidia kuunda jamii yenye watu wenye ujuzi na ubunifu, ambao wanaweza kuchangia katika kukuza uchumi na kuleta mabadiliko chanya katika nchi.

KUHUSU CAMFED, TANZANIA NA MALENGO YA DUNIA (SDGs):

Mkurugenzi wa Camfed Nasikiwa Duke akiwasilisha taarifa ya namna program ya Stadi za Maisha ilivyo pokelewa mbele ya kikosi kazi cha Taifa. 

Kupunguza Umaskini na Ukosefu wa Ajira:

Nchini Tanzania, kama yalivyo maeneo mengine duniani, ukosefu wa ajira na umaskini ni changamoto kubwa. Kwa kuwapa wanafunzi  Elimu ya stadi za maisha, serikali inaweza kuwasaidia kuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe au kushiriki katika shughuli za uzalishaji kwa muda mfupi baada ya kumaliza masomo yao. Hii inaweza kupunguza ukosefu wa ajira na kusaidia kupunguza umaskini katika jamii.

Kuimarisha Maadili na Uongozi:

Elimu ya stadi za maisha pia inajumuisha mafundisho ya maadili na uongozi. Wanafunzi wanajifunza jinsi ya kuwa raia wema na viongozi bora katika jamii. Kwa kuwekeza katika elimu hii, inaweza kuchangia katika kujenga jamii inayozingatia maadili na uongozi wa heshima.

Kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs):

Tanzania, kama sehemu ya jumuiya ya kimataifa, imejiunga na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Baadhi ya malengo haya yanahusu elimu na ustawi wa jamii kama vile lengo No. 4 na 5. Kusimamia elimu ya stadi za maisha ni njia mojawapo ya kuchangia katika kufikia malengo haya, kama vile kuboresha elimu kwa wote, kukuza usawa, na kuhakikisha maisha bora na usawa wa kijinsia.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa washirika hilola Camfed nchini Tanzania Bi, Nasikiwa Duke anasema wakati mradi huo wa Stadi za Maisha unaanza walizifikia Shule 365 za Sekondari lakini hadi kufikia mwaka huu wamezifikia Shule 466, ambazo zina nufaika na program ya Stadi za Maisha.

CAMFED  iliwezesha elimu ya mafunzo ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike ili kuwajengea ujuzi wa kujitegemea, kujitambua, na kushiriki kikamilifu katika jamii. Hii ililenga kuwawezesha kuwa viongozi na wabunifu katika maisha yao. Na ilifanya kwenye jamii ili kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu elimu ya kwa watoto wa kike na kuondoa mila na desturi potofu zinazoweza kuzuia upatikanaji wa elimu kwa wasichana Alisema bi, Nasikiwa Duke.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu Ndg.Mussa Mnyeti akielezea jinsi Serikali kupitia Wizara hiyo itakavyo simamia program ya Stadi za Maisha Shuleni.

Kwa upande wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Nilimuuliza Ndg.Mussa Mnyeti nikwa namna gani Program hii ya Stadi za Maisha kwa wanafunzi ina umuhimu kwa Serikali?  Programu hii inachochea maeneo kadhaa ikiwemo kukuza Uongozi na Ujifunzaji, na inasisitiza uendelezaji wa uongozi na ujifunzaji wa wanafunzi wa kike kupitia kwa walimu walezi na vikundi vya wanafunzi Shuleni. Hii imeendelea kusaidia kujenga ujasiri na uwezo wa kushiriki katika masuala ya elimu na kijamii kabla na baada ya kuhitimu masomo yao ya elimu ya Sekondari.

Programu hii ya Stadi za Maisha ni mkakati unaoisaidia Serikali kupambana na mdondoko kwa wanafunzi hasa wakike, kwani kumekuwepo na changamoto nyingi zinazo wakumba watoto wakike ikiwa ni pamoja na kukatisha masomo kwa sababu ya mimba za utotoni na changamo za kimazingira.

Hivyo kupitia mpango huu ambao unahusu kuwafundisha vijana Stadi za Maisha wakiwa bado shuleni, ninaamini kabisa Serikali inauunga mkono, na kumuandalia mazingira mazuri kwa watendaji kazi ilikwamba mdau huyu wa elimu ambae ni Camfed aweze kufikia shabaha ilio kusudiwa Alisema Ndg. Mnyeti.

Kupitia jitihada hizi, za Stadi za Maisha ziliwezesha mabadiliko makubwa katika maisha ya wanafunzi wa kike nchini Tanzania. Wanafunzi wengi wa kike walipata fursa ya elimu bora na kujifunza stadi muhimu za maisha ambazo zilikuwa muhimu katika kujenga mustakabali wao. Pia, program hii iliongeza uwepo wa wanawake katika nyanja za uongozi na uvumbuzi.

Matokeo chanya yalio tajwa na mkurugenzi wa shirika la Camfed Tanzania yanathibitishwa na Mkuu wa divisheni ya Elimu Sekondari kutoka halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Bi, Salama Ndyetabura ambapo anasema kupitia ofisi yake imefanikiwa kurejesha wanafunzi walio kuwa wamekatiza masomo kwa sababu mbalimbali, kamavile mimba za utotoni, mazingira magumu na kwa sababu ya mifarakano ya wazazi.

Kupitia program ya Stadi za Maisha shuleni imefanikisha wanafunzi wengi kujitambua na kuchochea ufaulu mkubwa kwa wanafunzi, hasa katika idara ya elimu Sekondari katika halmashauri ya Chalinze. Kwa mujibu wa malengo ya program hii ya Stadi za Maisha kwenye Shule za Sekondari nchini shirika kwa kushirikiana na Seriikali linatarajia kufikia asilimia 85% ya Shule zote ifikapo mwaka 2030, ikiwa nimoja ya njia ya kuunga mkono Malengo  17 ya Maendeleo Endelevu ya kudumu ya Umoja wa Mataifa SDGs.

Serikali ina jukumu kubwa la kusimamia elimu ya stadi za maisha katika shule za sekondari nchini Tanzania. Kufanya hivyo kutachangia katika kuandaa wanafunzi kwa maisha baada ya shule, kuimarisha uchumi, kupunguza umaskini, kukuza maadili na uongozi bora, na kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Ni muhimu kwa serikali kuwekeza katika rasilimali na sera za kuboresha elimu hii ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata stadi za maisha muhimu kwa maendeleo yao binafsi na ya taifa kwa ujumla Alisema Bi, Salama Ndyetabura.

Post a Comment

0 Comments