Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

POLIO: MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA POLIO KWA WATOTO TANZANIA:

 


Na, John Kabambala: 

Tukio la mwezi Julai mwaka 1996 lililo tokea Mkoani Mtwara, kumuhusu Issa Ibrahim halitasahaulika kamwe, lilikuwa la mwisho na likaiweka Tanzania kwenye nafasi ya kufunga ukrasa wa kuwa na wagonjwa wa Polio, hali hii iliifanya nchi kupeperusha bendera ya hakuna POLIO Tanzania.

Njoo nami kuyafahamu mengi zaidi kupitia Makala hii: Leo tunazungumzia Tatizo la Ugonjwa wa Polio, Chanzo na Suluhisho lake nchini Tanzania, karibu usome Makala hii naamini hautajutia muda wako, maana utapata mambo mapya kuhusu POLIO kwa watoto ambao ndio wahanga wakubwa wa ugonjwa huu tunao uzungumzia leo. Yamkini hukuwahi kuyasikia machache kati ya mengi nilio kuandikia kwenye Makala hii, kutoka kwa alie wahi kuugua ugonjwa huo na wataalamu kutoka –WHO Tanzania.

Issa Ibrahim alikuwa kijana mchangamfu na mwenye furaha, akicheza na marafiki zake kila siku. Hata hivyo, bahati mbaya, siku moja Issa Ibrahim alianza kuhisi maumivu makali ya misuli, na muda mfupi baadaye, alishindwa kutembea. Mama yake, alishtushwa na hali ya kijana wake na haraka wakampeleka hospitalini.

Baada ya uchunguzi wa daktari, ilibainika kuwa Issa Ibrahim alikuwa ameambukizwa ugonjwa hatari wa polio. Ugonjwa huu unaosababishwa na virusi unaweza kusababisha ulemavu wa kudumu au hata kifo. Issa Ibrahim alilazwa hospitalini kwa wiki kadhaa, akifanyiwa matibabu ya kurejesha nguvu katika misuli yake. Ingawa alipata nafuu polepole, ugonjwa wa polio uliacha athari za kudumu kwenye miguu yake, akibaki na ulemavu wa kutembea.

Hapa anasimlia zaidi Nilizaliwa Wilaya ya Mtwara vijijini Mkoani Mtwara, wakati nikiwa na umri wa miaka mitatu sikumoja nilienda uani kujisaidia sasa wakati ninarudi ghafla mguu wangu wa kushoto ukaisha nguvu nikadondoka chini, nikajaribu kunyanyuka ikashindikana.

Basi nikapiga kelele za kuhitaji msaada.nikaita Mamaaa!!!!! Mama alikuja alipofika nika mwambia nimeshindwa kutembea akaninyua akajaribu kunisimamisha lakini mguu ukaanza kukakamaa na kuuma sana, akanibeba akanipeleka ndani kunikalisha.

Basi!! Baadae hali ile hikurejea kwenye ukawaida wake baba alipofika mama akamueleza jinsi ilivyo tokea mwanzo hadi mwisho, jambo la kushangaza baba akasema huyu mtoto amelogwa sio ugonjwa wakawaida hakuna haja ya kumpeleka hospitali huko nikupoteza muda na pesa, baba akawa anamwambia mama maneno hayo.

Mama hakunikatia tamaa sasa nimekuwa mtu wa kubebwa wakati wote au wanapo niacha ndipo watakapo nikuta maana siwezi kunyanyua tena mguu na kutembea, siku moja akanipeleka kituo cha afya nilipo pimwa ndio nikagundulika nina polio, ila imeathiri muguu wataalamu wa afya wakamshauri mama niwe nakisaidizi cha mkuu kwamaana ya kutembea na magongo Alisema Issa Ibrahim.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania inatoa ufafanuzi kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa polio kuwa ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho huambukizwa kutoka kwa mtu aliyeathirika kwenda kwa mwingine, kwa kula au kunywa kitu kilicho chafuliwa na kinyesi chenye virusi vya polio. Virusi vya polio vinapoingia mwilini huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara ya kiafya ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa kiungo au viungo na hata kupelekea kifo.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kwamba “Napenda nichukue fursa hii kuwataarifu kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau wa afya UNICEF, WHO na HPS tutakuwa na Kampeni maalum ya utoaji wa chanjo ya matone dhidi ya Polio (nOPV2) kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka nane (8). Kampeni hii itafanyika kwa siku nne (4) kuanzia tarehe 21 – 24 Septemba, 2023 katika Mikoa sita (6) inayopakana na nchi zenye mlipuko wa Polio ambayo ni Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya”

“Lengo la kampeni hii ni kuwafikia watoto 3,250,598 waliozaliwa baada ya mwaka 2016 ili kuwakinga dhidi ya Kirusi cha Polio aina ya pili (Polio Virus Type 2) kinachoweza kusababisha ulemavu wa kudumu.  Kwa Mkoa wa Rukwa tunatarajia kufikia watoto 391,883 Kagera 729,387 Kigoma 884,477 Mbeya 614,346 Katavi 227,862 na Songwe 402,643” amesema. 

Dalili za Ugonjwa huu wa Polio kwa Mtoto ni Zipi?:

Dalili za awali za ugonjwa wa polio ni pamoja na homa, uchovu, maumivu ya kichwa, kutapika, kukakamaa shingo na maumivu ya viungo, na kundi linalo athirika Zaidi ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano 8.

WAGONJWA WA MWISHO WA POLIO WALIGUNDULIKA LINI HAPA TANZANIA:

Kwamujibu wa Dr. Anthony Kazoka kutoka shirika la afya ulimwenguni (WHO) ofisi za Tanzania amesema. “Kwa mara ya mwisho wagonjwa wa polio waligundulika kwenye mikoa mitatu ya Tanzania bara, mgonjwa wa kwanza aligundulika tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani Arusha, Mgonjwa wapili aligundulika tarehe 24 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani Kigoma na mgonjwa wa tatu na wa mwisho aligundulika tarehe 30 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani Mtwara”.

MAENDELEO YA ISSA IBRAHIM YAKOJE MPAKA SASA?

“Ninaendelea vizuri maana nilipona polio laikini iliniachia maumivu makali kwenye mguu wangu wakushoto, siwezi kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu nikiwa nimesimama kunawakati ukifika unaisha nguvu ahata kama ninatembea inabidi nisitishe safari nikae kwanza ukipoa ndio niendelee na safari”.

USHAURI WAKE KWA JAMII NI UPI?

Ibrahim anaishauri jamii kulingana na uzoefu alioupata kupitia ugonjwa wa polio tangu mwaka 1996 na kupatiwa matibabu, japokuwa amebakiwa na ulemavu wa kupooza mguu hayo yote nilisimuliwa na mama yangu baada ya kufikia umri wa kujitambua, “anasema wazazi/walezi wasije kuwa kama baba yangu alie kata kunihudumia na kunipeleka hospitali akisema nimelogwa, hakikisheni mnawapeleka watoto kupata chanjo kila wakati unapofika ilikuepuka ulemavu wa kudumu na hata vifo wakati mwingine”.

ISSA IBRAHIM YUPO WAPI KWA SASA?

Ibrahim kwa sasa anaishi Dar es Salaam kwa mama yake mdogo, ambapo hivi karibuni Mh.Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewaagiza watendaji wa Wizara hiyo kumpatia kitengo ndani ya Wizara hiyo Nd.Ibrahim hususani kwenye kitengo cha elimu kwa umma ilikuendelea kuhamasisha chanjo ya polio nchini.

HALI YA MLIPUKO WA UGONJWA WA POLIO KWA SASA IKOJE TANZANIA?

Dr. Anthony Kazoka amesema tangu mwaka 1996 hakuna kisa chochote cha mgonjwa wa polio nchini, na hii nikutokana na jitihada za serikali kupitia Wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la afya ulimwenguni (WHO) ofisi za Tanzania kuhakikisha wanadhibiti mlipuko huo kwa kuanzisha kampeini za utoaji chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano. 

Visa vya polio vimepungua kwa zaidi ya 99% tangu 1988, kutoka wastani wa visa 350,000 kwenye zaidi ya nchi 125 zenye ugonjwa huo hadi visa 175 vilivyoripotiwa mnamo mwaka 2019 duniani kote wakati huo Tanzania kukiwa hakuna kisa chochote cha polio tangu mwaka 1996, hatua iliyosababisha- WHO kanda ya afrika kuiweka Tanzania kwenye orodha ya nchi zilizo tokomeza mlipuko huo wa polio na kubakia kwenye nchi za Pakistan na Afghanistan.

Picha kutoka un news

SULUHISHO LA UGONJWA HUU NI CHANJO YA POLIO:

Kwa bahati nzuri, suluhisho la ugonjwa wa polio liko na limekuwa likifanya kazi kwa mafanikio kote ulimwenguni - ni chanjo ya polio. Chanjo hii ni ya kuaminika na salama na inatolewa kwa watoto wachanga kwa awamu kadhaa. Inalinda dhidi ya aina tatu za virusi vya polio na imekuwa ikipunguza kesi za ugonjwa huu kwa kasi.

Programu za utoaji chanjo zimeendeshwa kwa ushirikiano wa mashirika ya kimataifa na serikali za kitaifa, na juhudi hizi zimefanya ugonjwa wa polio kuwa nadra sana katika sehemu nyingi za dunia ikiwemo Tanzania. Kwa kuchanjwa watoto wote, tunaweza kufikia lengo la kutokomeza kabisa ugonjwa wa polio. Mwaka huu Serikali kushirikiana na wadau wa maendeleo kama

Post a Comment

0 Comments