Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

ELIMU YA AFYA YA UZAZI:NI SILAHA YA KWANZA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA VVU KWA VIJANA

 

Wanufaika wa mradi wa Dreams:

Na, John Kabambala:

Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) bado ni changamoto kubwa nchini Tanzania, na vijana wenye umri wa rika balehe hasa wasichana wanakabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa VVU. Elimu ya afya ya uzazi ni muhimu sana katika kuzuia maambukizi ya VVU kwa vijana, kwani inawawezesha kujifunza na kuelewa njia za kujikinga, kujenga uhusiano wenye afya, na kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yao ya uzazi. Makala hii inalenga kuchambua umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi katika kuzuia ongezeko la maambukizi ya VVU kwa vijana wa rika la vijana balehe nchini Tanzania.

Tuanzie Mkoani Mbeya, ambako Shirika sililo la kiserikali, Tumaini Community Services linatekeleza mradi wa ‘Dreams’ yaani ‘Ndoto’ katika Halmashauri ya Mbeya mjini, Kyela na Mbarali mkoani Mbeya kwa ufadhili wa mfuko wa rais wa Marekani wa harakati za kupambamba na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania, lengo likiwa kuwawezesha vijana balehe elimu ya afya ya uzazi, elimu ya kujitambua na elimu ya kiuchumi ili kupunguza maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, ambapo mpaka sasa zaidi ya vijana elfu 30 wamefikiwa na mradi huo kwa Wilaya hizo tatu.

Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) bado ni changamoto kubwa nchini Tanzania, na vijana wenye umri wa balehe wanakabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa VVU. Elimu ya afya ya uzazi ni muhimu sana katika kuzuia maambukizi ya VVU kwa vijana, kwani inawawezesha kujifunza na kuelewa njia za kujikinga, kujenga uhusiano wenye afya, na kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yao ya uzazi. Makala hii inalenga kuchambua umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi katika kuzuia ongezeko la maambukizi ya VVU kwa vijana wa rika la balehe nchini Tanzania.

Sababu zinazo weza kusababisha vijana hawa kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI miongoni mwazo ni Ukatili wa Kijinsia, Vijana wa rika la balehe wanaweza kuwa katika hatari zaidi ya kubakwa au kulazimishwa kufanya ngono bila kinga, ambayo inaweza kusababisha maambukizi ya VVU.

Ujinga na Kutojua, Vijana wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu VVU na njia za kujikinga, na hivyo wanaweza kuchukua hatari bila kujua, Ubaguzi na Unyanyapaa, Ubaguzi na unyanyapaa kuhusu VVU vinaweza kufanya vijana waogope kupima na kutafuta huduma za afya.

Tatu Mwambungu kutoka Wilayani Kyela ni mnufaika wa mradi wa Dreams unaotekelezwa mkoani Mbeya na shirika la Tumaini Community Services anaeleza sababu anazofikiri kuwa ni visababishi vinavyowaweka matatizoni vijana balehe hasa wa kike, anasema ni kutokana na kukosa elimu sahihi ya afya ya uzazi akisema kwamba wanafika umri wa kubalehe lakini hawana elimu hiyo, “tunakuwa hatujui kutokana na jamii yetu wanaficha au wzazi wanaficha vile vitu ambavyo binti anatakiwa kuvijua akishakua amebalehe”.

Wanufaika wa Mradi wa Dreams.

Je, Kuna umuhimu na ulazima kiasi gani vijana kufundishwa elimu ya Afya ya uzazi?

“Elimu ya afya ya uzazi inaweza kutoa vijana maarifa na ufahamu kuhusu VVU, njia za maambukizi, na jinsi ya kujikinga. Vijana wanapoelewa hatari, wanakuwa na msukumo wa kuchukua hatua za kuzuia. Kujifunza Njia za Kujikinga, Elimu hutoa taarifa za kina kuhusu njia za kujikinga na VVU, kama vile matumizi ya kondomu na kupima VVU mara kwa mara.

Kukuza Uhusiano wa Afya,Vijana wanaweza kujifunza jinsi ya kujenga uhusiano wa afya na kuzungumza na wenza wao kuhusu masuala ya ngono na afya ya uzazi. Hii inaweza kusaidia katika kuzuia maambukizi ya VVU. Kutoa Elimu ya Kupima VVU, Elimu ya afya ya uzazi inaweza kutoa mwongozo kwa vijana kuhusu umuhimu wa kupima VVU na kutafuta matibabu mapema, na pia kuhusu upatikanaji wa vituo vya kupima VVU” Tatu Alisema.

Dkt. Steward Kilumile ni Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Miyombweni kilichopo Wilaya ya Mbarari anasema elimu kuhusu afya ya uzazi inayotolewa kwa vijana anaona inaleta mabadiliko. Akisema, “kupitia mradi kama huu wa dreams kwa kuwa wanapata elimu kwenye vikundi inazidi kuwapa vijana upeo dhidi ya mazingirea hatarishi.” 

Aidha Dkt. Steward Kilumile Serikali iongeze msisitizo ufikishwaji wa elimu hii kwa Vijana, na vijana wengi wa Tanzania wanaishi vijijini, na hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa elimu ya afya ya uzazi inawafikia pia katika maeneo haya. Hii inaweza kufanyika kwa kutoa semina na mikutano katika vijiji, na hata kuongeza vitengo maalumu kwa vijana kwenye vituo vya afya katika maeneo ya mbali.

Kujumuisha Wazazi na Walezi: Wazazi na walezi wanaweza kuwa sehemu muhimu ya mchakato wa kutoa elimu ya afya ya uzazi. Kuwajumuisha katika mafunzo na kampeni kunaweza kusaidia kuunda mazingira bora ya kujadili masuala ya afya ya uzazi nyumbani. Kutoa Elimu Kwa Kuzingatia Utamaduni: Elimu inapaswa kuendana na utamaduni na mila za eneo husika. Hii itawezesha kukubalika kwa elimu hiyo kwa jamii na kupunguza unyanyapaa.

Jonathan Mwashilindi.

Jonathan Mwashilindi ni Mkurungezi wa shirika hilo la Tumaini anasema wasichana wenye umri mdogo kutokana na kukosa muongozo mzuri ndipo wanajikuta wanapata ujauzito wakiwa bado watoto wadogo na hawajui hao watoto watakaozaliwa watawatunza kwa namna gani. Kwa msingi huo anatoa wito kwa kila mtu katika jamii kushiriki katika kusaidia “ili hawa mabinti ndoto zao waweze kziishi baadaye.” 

Mfuko wa rais wa Marekani wa harakati za kupambamba na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania umekuwa ukisaidia serikali ya Tanzania kuboresha sekta ya afya kwa ujumla wake hasa katika kupambambana katika kupunguza maambukizi ya vvu nautoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana balehe, jitihada hizo zimeendelea kujidhihilisha kupitia miradi mbalimbali inayo husu afya.

Njia za Kutoa Elimu ya Afya ya Uzazi

Ndg. Jonathan Mwashilindi  Anapendekeza hatua zifuatazo zikifanyika kwa uhakika na kwa ushirikiano wa kila sekta zinaweza kutoa matokeo mazuri. Shule, Elimu ya afya ya uzazi inaweza kuingizwa kwenye mtaala wa shule ili kufikia vijana wa shule kwa ufanisi.

Makongamano na Semina,Kuandaa makongamano na semina kwa vijana wa balehe inaweza kuwa njia nzuri ya kutoa elimu ya afya ya uzazi, Vyombo vya Habari, Matangazo kwenye redio, televisheni, na mitandao ya kijamii yanaweza kutumiwa kutoa taarifa kwa vijana, Vituo vya Afya, Vituo vya afya vinaweza kuwa vituo vya kutoa elimu ya afya ya uzazi na kupima VVU.

Katika ulimwengu wa sasa, teknolojia inaweza kutumika kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa njia ya programu za simu na tovuti. Hii inaweza kufanya elimu kuwa inapatikana kwa vijana kwa urahisi na kwa njia inayowafikia.

Elimu ya afya ya uzazi ina jukumu kubwa katika kuzuia maambukizi ya VVU miongoni mwa vijana wa rika la balehe nchini Tanzania. Kwa kutoa elimu hii kwa njia inayofaa na kuongeza ufikiaji wake, inaweza kusaidia kubadilisha tabia za vijana, kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yao ya uzazi, na hatimaye kupunguza maambukizi ya VVU. Ni jukumu la pamoja kwa serikali, mashirika ya kijamii, wazazi, na jamii kwa ujumla kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata elimu hii muhimu na wanaweza kuwa na maisha yenye afya na mafanikio.

 

Post a Comment

0 Comments