Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

LEILO: MWALIMU WA UJASIRI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA

 


Na, John Kabambala: 

Mwangaza wa matumaini ulikuwa ukibadilika kuwa giza kwa msichana mmoja mdogo tulie mpa jina la Leilo. Alikuwa na miaka kumi na tatu tu, lakini ndoto zake zilikuwa kubwa kama anga la usiku lenye nyota nyingi. Leilo alitamani kuwa daktari, kutoa matibabu kwa watu wa kijiji chake, na kuifanya dunia kuwa mahali bora.

Kwenye makala hii utakao wasoma na walio shiriki kuelimisha jamii kupitia visa na ushauri wao ni pamoja na, Leilo, Bakita Andrea, Maria Mussa  na Kijana wa kiume Kassima.

Lakini, kwenye njia ya Leilo kuelekea ndoto zake, kulikuwa na kivuli kikubwa kinachoitwa Kassima hata hilo sio jina halisi. Kassima, kijana mwenye umri wa miaka ishirini na tano, alijulikan kwa kuwa na tabia mbaya kwenye kijiji hicho. Alijaribu kumvuruga Leilo, akimtisha na kumfuata kila mahali. Alitumia maneno machafu na vitisho vya kikatili, akimwonyesha uovu wa ulimwengu.

Leila alijawa na hofu na machungu. Alikuwa amefungwa katika lindi la aibu na udhaifu. Hakuwa na uhakika wa kufichua mateso yake kwa mtu yeyote, na alihisi ange mueleza mtu mwingine angeweza kutupwa kando bila kupewa msaada wowote. Ndoto zake za kuwa daktari zilififia polepole, kama jua linalofifia magharibi.

Ndugu msomaji wa makala hii, wakati nafanya nae mahojiano kuhusu kisa hiki, fahamu zangu zilikuwa zinakija na kuondoka mara baada ya kuuvaa uhusika wa msichan huyu “Leilo”.

Lakini siku moja, Leilo aliamua kusimama kwa ujasiri na kutoa mapambano. Aliamua kuzungumza na dada yake mkubwa, Amina, kumwelezea kila kitu. Amina alimsikiliza kwa makini, akimtia moyo kwa upendo na kumweleza kuwa yuko tayari kusimama naye bega kwa bega.

Kwa pamoja, Leilo na Amina walifanya uamuzi wa kuwasiliana na wazazi wao na walimu wao kuhusu mateso ya Kassima. Walitoa sauti yao dhidi ya ukandamizaji huu. Walikuwa sauti ya haki na usawa, na walitafuta msaada wa jamii yao.

Sauti ya Leilo na Amina ilisikika kote kijijini. Kiongozi wa kijiji alisikia kilio chao cha ujasiri na aliamua kuchukua hatua. Kassima alikamatwa na kushtakiwa kwa ukatili wa kijinsia. Alipelekwa mahakamani na hatimaye alihukumiwa kutumikia kifungo.

Baada ya tukio hilo, Leilo alianza kurejesha ndoto zake. Alishiriki masomo yake na kuchukua hatua kuelekea kuwa daktari mwenye bidii. Kwa mara nyingine, aliona jua la matumaini likichomoza.

Ikumbukwe kwamba nchini Tanzania umri wa balehe ni kipindi kinachoambatana na hatari zaidi kwa wasichana, hasa kwa wale waishio katika mazingira magumu, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuongeza na kuendeleza uimarishaji wa uelimishaji kuhusu usawa wa kijinsia, haki na maendeleo yao ya wasichana.

Ili kuisaidia Serikali katika kuelimisha kundi hili lililopo kwenye hatari zaidi, vyama vya kiraia, jamii, wazazi, walezi, viongozi wa dini, viongozi wa kimila, wasichana na wavulana wenyewe wanapaswa kushiriki kikamilifu kila mmoja kwa sehemu yake, ili kukabiliana na changamoto zinazo wazunguka wasichana.

Niliwatafuta na kufanya mazungumzo na baadhi ya wasichana walio katika umri wa rika balehe, kusikia wanafahamu nini kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia, Bakita Andrea mkazi wa Manispaa ya Morogoro ni msichana mwenye umri wa miaka kumi natatu (13) mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi saba saba “A” iliopo Manispaa ya Morogoro, anaelezea vitendo vya ukatili.

“Ukatili ni unyanyasaji wa kijinsia kwakuwafanyisha kazi ngumu zisizo endana na umri wao kuwapiga, kuwanyanyasa na kuwatenga, ukatili huwakuta sana watoto wakike, wengine hufanyiwa ukatili na wazazi wao, ndugu zao jamaa na marafiki n ahata walimu wao. Nakumbuka juzijuzi shule ya Mazimbu alijinyonga mwanafunzi wa darasa la tano kwa kufanyiwa ukatili na babayake aliharibika sehemu zake za siri kwasababu alikuwa akibakwa na babayake” Amesema.

Aidha Bakita anasema madhara yanayoweza kujitokeza kwa binti alie fanyiwa ukatili, “Ukatili wa namna hiyo huleta madhara kwa mtoto wakike kwa kumuharibia sehemu za siri nakumfanya awe hayupo makini darasani kwa sababu akiwa darasani mudawote nimtu wakuwaza nikirudi nyumbani usiku kazi kwa baba ataanza kuni fanyia vitendo vya ukatili”.

Bakita akapaza sauti yake kwaniaba ya wasichana wengine kwa Serikali kuhusu watu wanao fanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wakike, “Serikali ikomeshe vitendo vya ukatili na itoe adhabu kali kwa wale wanao wafanyia watu vitendo vya ukatili”.

Hata hivyo Maria Mussa yeye ni mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Uhuru iliopo katika Manispaa ya Morogoro, anaeleza anayo yafahamu juu ya ukatili wanao fanyiwa watoto hasa wakike.

“Nakumbuka kulikuwa na watoto watatu waliokuwa wakiishi na bibi, babu na binamu yao, kumbe binamu yao akawa kila siku anaingia kwenye chumba cha hao watoto watu nyakati za usiku wakiwa wamelala na kuwa fanyia ukatili kwa kuwarawiti na kuwambia wakipiga kelele nawaua”.

Maria akatoa ushauri kwa jamii hususani wazazi, “Wazazi wawe wanawalinda watoto na wawe wanakaa nao watoto karibu wenyewe kwa sababu watoto wakienda kulelewa na watu wengine ndio wanawafanyia ukatili” Amesema.    

Kassima, kwa upande wake, alipewa fursa ya kubadilisha tabia yake. Alikuwa na muda wa kujifunza kutoka kwa makosa yake na kuelewa kuwa upendo wa kweli haujengwi kwa kutumia nguvu na udhalilishaji.

Kisa cha Leilo kinatufundisha kuwa ukatili wa kijinsia unaweza kushindwa kwa ujasiri na mshikamano. Kinatufundisha kuwa tunaweza kusimama dhidi ya ukandamizaji na kuibadilisha jamii yetu kuwa mahali salama kwa kila mtu. Leilo alionyesha ujasiri wa kutoka kwenye giza na kuongoza njia kuelekea mwangaza wa matumaini.

Post a Comment

0 Comments