Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

LISHE BORA NI MTAJI: NIMUHIMU KUWEKEZA KWA WATOTO,FAO:

Wanafunzi wa shule ya msingi Muungano wakifuatilia darasa la mapishi Mwanga Community Centre iliopo Mkoani Kigoma:

Na, John Kabambala.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) liliamua kufanya kitu kikubwa nchini Tanzania kwa siku ya Chakula Duniani. Walitaka kuleta mabadiliko katika maisha ya watoto na historia isio futika kwenye maisha na familia zao kwa kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa lishe bora. FAO iligundua kuwa njia bora ya kufanya hivyo ilikuwa kuanzisha programu ya kufundisha watoto mapishi ya vyakula vyenye lishe.

Kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na wadau wengine wa maendeleo, FAO ilianza kutekeleza wazo hili la kipekee. Kupitia miradi yake mbali mbali ambayo hutekelezwa nchini Tanzania ilinayo husika na kilimo pamoja na masuala ya lishe kama vile mradi wa AGRI-CONNECT unao tekelezwa katika mikoa ya Tanzan ia bara na Zanzibar, unao husisha shule za msingi.

Stella Kimambo ni afisa lishe kutoka Fao Tanzania, kupitia siku ya chakula duniani ambayo ilifanyika kitaifa Mkoani Kigoma anaeleza  umuhimu wa vyakula vya protini kwa familia na hasa watoto, tazama na kusikiliza kupitia video hii hapa >>>>


HALI ILIKUWAJE AWALI:

Ukosefu wa Elimu ya Lishe: Mara nyingi, watu katika jamii wanaweza kukosa uelewa wa kutosha kuhusu lishe bora. Wanaweza kutokuwa na habari au ufahamu wa vyakula vyenye lishe au jinsi ya kuandaa vyakula hivyo. Hii inaweza kuwa tatizo kubwa, kwa sababu ili uweze kufundisha watoto, unahitaji kwanza kuwa na elimu sahihi.

Upatikanaji wa Vyakula Vyenye Lishe: Katika maeneo fulani, upatikanaji wa vyakula vyenye lishe unaweza kuwa mdogo au gharama zake zinaweza kuwa juu sana. Lakini sio kama hapa kwetu Tanzania, mfano hapa Mkoani Kigoma vyakula vingi vya asili vinapatikana tena wanavilima wahapa hapa, hii inafanya iwe rahisi kwa familia kufundisha umuhimu wa  vyakula vyenye lishe kwa watoto wao.

Maadili na Mila za Kitamaduni: Baadhi ya jamii zinaweza kuwa na mila na desturi ambazo zinaweza kuzuia mabadiliko katika mlo wa kila siku. Kwa mfano, vyakula vyenye lishe vinaweza kutazamwa kama "vyakula vya kigeni" au kuwa nje ya utamaduni wa eneo hilo, na hivyo kutothibitika kutumika kwenye milo mezani, lakini ndio maana  shirika la FAO kupitia mradi wake wa lishe tumeanza kuwafundisha watoto kuelewa umuhimu wa vyakula hivyo.

Elimu ya Kupika na Lishe Katika Shule: Katika mfumo wa elimu, mara nyingine, masomo ya lishe na kupika havipewi uzito wa kutosha. Hii inaweza kuacha pengo katika elimu ya lishe kwa watoto. Kwa mkutadha huo tunaendelea kuishauri serikali na wadau wengine wa maendeleo kuhamasisha na kuchangia elimu na utoaji wa mlo shuleni.

HALI IKOJE SASA:

Picha ya Alfonsina Paul akifundishwa ya vyakula vya asili:

Kwa kuzingatia sababu hizi, shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa FAO limeweza kutoa mafunzo na rasilimali kwa jamii ili kusaidia kuondoa vikwazo hivi na kufundisha watoto jinsi ya kuandaa na kula vyakula vyenye lishe.

Miongoni mwa watoto walio hudhulia mafunzo hayo ni Alfonsina Paul mwanafunzi wa darasa la nne kutoka shule ya msingiMuungano iliopo Mkoani Kigoma, anasema mwalimu aliewafundisha alikuwa mwema sana, ambaye aliwafundisha jinsi ya kupika vyakula vyenye lishe na vya asili kama vile maharage, dagaa, maziwa ya ng’ombe, kunde na njegele na samaki waliopatikana katika ziwa Tanganyika pamoja na kutumia matunda na mboga kuandaa juisi.

Baada ya mafunzo hayo kwa vitendo, Alfonsina Paul alijifunza mambo mengi. Alijifunza umuhimu wa lishe bora na jinsi ya kutumia vyakula vya asili katika njia bora zaidi. Alifurahi kugundua kuwa vyakula vyenye lishe vinaweza kuwa vitamu natiba na vyenye kuvutia vyakula vinavyo toka viwandani, aidha anaishukuru fao kupitia siku ya chakula duniani kufundisha namna ya kuandaa mlo kwa kutumia vyakula vya asili na umuhimu katika afya.

Kwa maneno ya Alfonsina Paul mwenyewe, "Mafunzo ya FAO yamenibadilisha na kunitia moyo kusambaza ujuzi wa lishe bora nyumbani kwetu na kwa wenzangu. Kila mtoto anapaswa kuwa na fursa ya kupika na kula vyakula vyenye lishe bora ili kuwa na afya njema. Mimi ni mfano wa mabadiliko, na nataka kuleta mabadiliko katika familia yetu na hata kwa familia za marafiki zangu, kwani kunawatoto wengine hadi wanafikisha umri wa miaka 13 hawjui bado kupika, nitawafundisha kila kitu" Alisema.

Kupitia jitihada za FAO na serikali ya Tanzania, watoto wengi walipata fursa ya kujifunza na kufurahia vyakula vyenye lishe bora, na hivyo kwa njia hii inaweza kusaidia kupunguza tatizo la utapiamlo na kuimarisha afya ya taifa. Hii ni makala nzuri inayo onesha jinsi shirika la FAO linavyochangia kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watoto wa Tanzania kupitia elimu ya lishe na siku ya Chakula Duniani, lakini pia kupitia mradi wake wa Agriconect unaotekelezwa nchini Tanzania kwa ufadhili wa umoja wa ulaya Eu.

Zena Mshana kulia ambae alikuwa mkufunzi wa mafunzo ya mapishi jikoni akionesha watoto aina ya vyakula watakavyo pika. 

Taasisi ilio ratibu mafunzo hayo ya mapishi ni PELUM Tanzania ya mjini Morogoro kwa kushirikiana na mkufunzi Zena Mshana na hapa anasema “Kwenye darasa la mafunzo ya mapishi kwa watoto na wanawake vijana hakika wamefurahia sana kwa sababu wamejifunza namna ya pekee sana ya kuandaa milo yao nyumbani au shuleni kwa kutumia vyakula vilevile ambavyo vinapatika sokoni kwao, wanavyo lima wenyewe isipokuwa tu mbinu za kuandaa ilikupata vitamin na protini kutoka kwenye vyakula hivyohivyo.

Miongoni mwa madarasa yalio ongoza kwenye siku ya chakula duniani kwa kuto pungukiwa nawatu ni darasa letu hili, hasa watoto ambao ndio mojawapo ya kundi tunalo lilenga kufundisha kuhusu masuala ya lishe bora na kwa sababu hapa tulikuwa tukijifunza kwa vitendo, vyakula vinapo iva tunapakua tunakula darasa zima”.

Aidha Bi, Mshana anaeleza miongoni mwa sababu kuu zinazo changia jamii kushindwa kuandaa vyakula vyenye ilishe bora kuwa ni ukosefu wa elimu au ufahamu wa kutosha kuhusu lishe bora. Watu katika jamii wanaweza kutokuwa na habari sahihi juu ya vyakula vyenye lishe au jinsi ya kuyatumia kwa njia inayofaa. Bila ufahamu wa lishe, itakuwa vigumu kufundisha watoto masuala ya mapishi ya vyakula vyenye lishe.

Mila na Tamaduni za Kitamaduni: Katika jamii nyingine, mila na tamaduni za kitamaduni zinaweza kuathiri chakula cha kila siku. Vyakula vyenye lishe vinaweza kutazamwa kama "vyakula vya kigeni" au kuchukuliwa kuwa nje ya utamaduni wa eneo hilo. Hii inaweza kuzuia watu kujifunza na kufundisha jinsi ya kutumia vyakula hivyo kwa njia inayofaa. Pia elimu ya lishe na upishi haijapewa uzito wa kutosha katika mfumo wa elimu. Hii inaweza kusababisha watoto kushindwa kupata elimu sahihi juu ya lishe na upishi katika shule.

SULUHISHO LAKE NI:

Kampeni za Elimu: Kuanzisha kampeni za elimu katika jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora na jinsi ya kupika vyakula vyenye lishe. Hii inaweza kufanywa kupitia mikutano ya jamii, semina, na matangazo katika vyombo vya habari. Mfumo wa Elimu: Kuimarisha elimu ya lishe na upishi katika shule. Shule zinaweza kuanzisha programu za kujifunza jinsi ya kupika na vyakula vyenye lishe, na kuwaelimisha watoto kuhusu umuhimu wa lishe bora.

Mashindano ya Upishi: Kuandaa mashindano ya upishi kwa watoto na vijana katika jamii. Hii inaweza kuwahamasisha kujifunza jinsi ya kupika na kutumia vyakula vyenye lishe kwa njia ya ubunifu. Mifano Mzuri: Kuwatumia watu wenye ujuzi katika upishi na lishe katika jamii kama mifano mzuri kwa watoto. Watoto wanaweza kujifunza kutoka kwa watu wanaojali lishe bora.

Ushirikiano wa Jamii: Kuhamasisha ushirikiano wa jamii kwa kuanzisha vikundi vya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika maandalizi ya vyakula vyenye lishe bora.

Michezo ya Kuelimisha: Kuanzisha michezo ya kuelimisha kwenye shule na jamii ambayo inaweza kufundisha watoto kuhusu lishe bora kwa njia ya kucheza na kujifurahisha. Usimamizi wa Wazazi: Kuwahamasisha wazazi kuchukua jukumu la kuelimisha watoto wao kuhusu lishe bora na kushiriki nao katika maandalizi ya vyakula vyenye lishe.

Kwa kutumia mbinu hizi zinaweza kusaidia kujenga ufahamu wa lishe bora na kuwapa watoto stadi za maisha kuhusu jinsi ya kuandaa na kula vyakula vyenye lishe bora. Kwa kufanya hivyo, jamii inaweza kuchangia kuboresha afya na ustawi wa watoto wao.

Kaulimbiu ya mwaka huu siku ya chakula duniani ilikuwa ikisema "MAJI NI UHAI MAJI NI CHAKULA"

 


Post a Comment

0 Comments