Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MBINU ZA MALEZI YENYE MWITIKIO KWA WATOTO WACHANGA NA WADOGO

 


Na, John Kabambala:

Malezi yenye mwitikio (responsive parenting) ni mbinu ya malezi inayolenga kutoa mazingira mazuri kwa watoto ili kuwasaidia kukua na kuendeleza ustawi wao wa kimwili, kihisia, kijamii, na kiakili. Nchini Tanzania, kama ilivyo katika maeneo mengine duniani, malezi yenye mwitikio ni muhimu sana katika kujenga msingi mzuri wa maisha ya watoto na jamii kwa ujumla.

Malezi yenye mwitikio yanaangalia mahusiano ya karibu baina ya mzazi/mlezi na mtoto, ikizingatiwa kuwa ushahidi unaonesha umuhimu wa mwitikio wa mahitaji ya watoto kulingana

na ishara watakazo onesha katika kuchangia ukuaji wao. Utaratibu wa kujumuisha huduma za malezi jumuishi kwenye huduma zilizopo kama vile afya na lishe bado ni dhana mpya, hivyo inasababisha ufikiaji mdogo kwa walengwa.

Mifano michache ya huduma jumuishi ambazo hutekelezwa na wadau katika maeneo mbali mbali nchini hujumuisha uchangamshi wa awali na afya, lishe na ulinzi wa mtoto. Afua zilizopo ni chache na zipo kwenye mfumo wa miradi au utafiti zikitekelezwa kwa kiwango kidogo na kujumuishwa moja kwa moja

katika program za Afya na Lishe zinazoendeshwa katika vituo vya Afya na ngazi ya jamii. Kwa hivyo hakuna takwimu za taifa au afua katika kipengele hiki cha MMMAM kinacholenga watoto wenye umri wa miaka 0-3.

Malezi kwa Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto:

Malezi kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto (CCD) ni mkoba ulioandaliwa wenye mbinu zilizothibitishwa na Shirika ya Afya Duniani (WHO) na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa ajili ya watoa huduma za afya ili kutoa unasihi kwenye michezo na mawasiliano kwa wazazi/walezi wenye watoto wa wenye umri wa miaka 0-3 wakati wa utoaji wa huduma za afya.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kupitia WAMJW kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto imeanza kuwekeza kwenye malezi yenye mwitikio kwa kujumuisha mbinu za malezi kwa makuzi na maendeleo ya mtoto pamoja na mafunzo ya ufuatiliaji wa ukuaji na maendeleo ya mtoto. Mpaka sasa rasimu ya Mwongozo wa Malezi kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto na mkoba wa Malezi kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto vimeandaliwa. Lengo la Mwongozo wa Kitaifa wa Malezi Kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto ni kuhakikisha huduma za malezi yenye mwitikio zinafika nchi nzima kupitia mfumo wa afya. 

Mkoba wa mafunzo ya Malezi Kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto kinawajengea uwezo wahudumu wa afya wa vituoni na wa kwenye jamii kujumuisha jumbe za uchangamshi wa awali na malezi yenye mwitikio kwenye huduma za afya. Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto kimeonesha jitihada ya kutanua wigo wa matumizi ya mkoba wa Malezi Kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto kwa kufanya majaribio kwa kuunganisha mkoba wa Malezi Kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto na Ufuatiliaji wa ukuaji na Maendeleo ya Mtoto katika mafunzo kazini.

Pia, Mkoba wa MMMAM unaonekana katika Mwongozo wa Taifa wa huduma kwa watoto wenye umri chini siku 28 na uanzishaji wa kitengo cha matunzo ya watoto wenye umri wa chini ya siku 28. Miongozo hii inatambua umuhimu wa mawasiliano na mtoto kuanzia ujauzito, mtoto mchanga na mtoto mgonjwa. Pia, mwongozo wa huduma kwa watoto wenye umri chini ya siku 28 unatambua ustawi wa mama kwa mahusiano bora na mtoto na ukuaji wake41 . 

Ingawa huduma za malezi yenye mwitikio zinaweza kuonekana kuwa mbinu mpya nchini, ni muhimu kutambua mila na desturi nzuri zilizopo zikiwemo za malezi ya watoto ambazo zinaweza zikaendelezwa na kuboreshwa pale inapowezekana. Aidha, wazazi, walezi na familia washawishiwe kutumia stadi na uwezo wa kutengeneza vifaa vya michezo vinavyopatikana kwenye jamii kwa kutumia malighafi zenye gharama ya chini, mfano chupa 41

https://www.medbox.org/document/national-guideline-for-neonatal-care-and-establishment-of-neonatal-care-unit#GO

tupu, nguo, vifuu na michanga. Kwa kutumia malighafi hizo familia wanaweza kutengeneza, magari, mwanasesere, chekeche, vitabu na vingenevyo. Huduma za Afya na Lishe zilizopo nchini zinatoa fursa ya kutoa huduma za malezi jumuishi. Hii inajumuisha uwepo wa mkakati wa Huduma za Afya kwenye Jamii ili kusaidia Watoa Huduma za Afya Kwenye Jamii (WAJA) kutembelea kaya na huduma za malezi jumuishi.

Hii inajenga mazingira ya watoa huduma jumuishi za malezi yenye mwitikio, uchangamshi wa awali, ulinzi wa mtoto, pamoja na huduma za afya na lishe. Vilevile, kupitia Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe, shughuli za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto zimejumuishwa pamoja na programu ya lishe ambapo inajenga nafasi ya kuenea kwa huduma hizi nchini.

Pia, kuna nafasi ya kuunganisha na kusambaza programu na vifurushi vya mawasiliano vilivyopo ambavyo vimejumuisha vipengele vya malezi jumuishi kama vile mradi wa malezi ambao unatekelezwa na Shirika la EGPAF mkoani Tabora; Programu ya kuharakisha kupunguza udumavu inayotekelezwa kupitia Shirika la Kimataifa la kuhudumia Watoto katika mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe; na utafiti wa afua za kuwahusisha kina baba katika Huduma bora za Lishe unaofanyika na Shirika la PCI Mkoani wa Mara.

                     

AJENDA YA KITAIFA YA MALEZI

Ajenda ya Kitaifa kwa Malezi na familia Tanzania (Familia Bora, Taifa Imara) kwa watoto kuanzia miaka 0-18 ina nguzo za malezi bora (Lea –Linda – Wasiliana) ambazo zinajitosheleza katika mbinu za malezi yenye mwitikio. Ajenda ya Kitaifa ya Malezi inatoa nafasi ya kushughulikia taratibu za malezi kwa watoto na kuzishughulikia katika programu za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto za kisekta.

https://download.ei-ie.org/Docs/WebDepot/Report%20Tanzania_UB.PDF

FURSA ZA UJIFUNZAJI WA AWALI

Kujifunza huanza tangu ujauzito na sio shule ya awali, na unaendelea katika maisha yote ya binadamu, Ujifunzaji wa awali ni uwezo anaojengewa mtoto kupitia mwitikio wa mlezi ambapo mtoto anapata ujuzi, sifa na uwezo kupitia vitendo rahisi mfano kutabasamu, kutazama machoni, kuzungumza, kuimba, kutoa mifano kwa vitendo, kuigiza, na michezo rahisi ili kuhakikisha mafanikio ya kuzoea mabadiliko kwa haraka yakiwemo ya kujenga mahusiano na watu wengine. Hivyo, ujifunzaji sahihi wa awali ni muhimu kwa makuzi ya mtoto kiakili, kijamii, kijinsia, kimwili na katika maandalizi na utayari wa elimu ya baadae.

Elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogo Mchana

Nchini Tanzania watoto wenye umri wa miaka 3-4 hawafikiwi na programu za malezi na makuzi ya mtoto. Mkanganyiko katika sera na Sheria za elimu ya awali unachanganya watekelezaji na wadhibiti katika utoaji wa huduma katika kundi hili. Wakati Sera ya Elimu inasema watoto hawa wanaweza kupata elimu ya awali, Sheria ya Mtoto inatoa mamlaka kwa Kamishina wa Ustawi wa Jamii kusimamia huduma jumuishi za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto chini ya miaka 5.

https://www.google.com/search?q=43+Ministry+of+Education+Science+and+Technology+(MoEST)+Education+and+Training+Policy+2014.&oq=43+Ministry+of+Education+Science+and+Technology+(MoEST)+Education+and+Training+Policy+2014.&aqs=chrome..69i57.1169j0j7&sourceid=chrome&ie=UTF-8

Hata hivyo mtaala na upimaji wa maendeleo kwa elimu ya awali unalenga watoto wa miaka 5. Aidha, kuwepo kwa changamoto ya mlundikano na mchanganyiko wa umri katika mikondo ya elimu ya awali imepelekea kupunguza uandikishaji wa watoto wa miaka 3-4. Vilevile kama hakuna programu za kitaifa zinazolenga watoto wa umri wa miaka 3-4, wengi wa watoto hawa wanakosa fursa za elimu ya awali. Hii pia ina maana kuwa hakuna programu rasmi ya kitaifa inayoendana na maendeleo ya kundi hili, hivyo kupelekea watoto hawa wanapojiunga na vituo vya kulelea watoto wadogo mchana huishia katika mfumo wa kufundishwa badala ya kujifunza kupitia michezo na kutumia zana kulingana na mazingira yao.

https://download.ei-ie.org/Docs/WebDepot/BEST2016FINAL2SEPT2016-FINALPRINTING-2.pdf

Wakati shule binafsi na shule za madhehebu ya dini zikiongeza kutoa elimu ya malezi na elimu ya awali hata hivyo huduma hizi hufikia asilimia 5 tu ya watoto wote wenye umri huo, mathalani wengi wao wakiwa maeneo ya mijini42. Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imewekeza katika mipango mbalimbali ya kutatua changamoto hii ikiwa ni pamoja na kuandaa kiongozi cha mlezi cha kuwezeshea watoto chini ya umri wa miaka mitano kujifunza kwa njia ya michezo.

 

Post a Comment

0 Comments